Simile motokari yangu Samia

Simile motokari yangu Samia

kaputula

Senior Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
173
Reaction score
223
Kwa wale wakongwe tulisoma shule ya msingi vile vitabu vya Someni kwa Furaha tunakumbuka. Kuna ile hadithi mtoto anamwambia mwenzake simile motokaa yangu.

Anamtahadharisha asimuharibie kigari chake cha kuchezea.
Nalinganisha hiyo na namna Samia anakuja kuiondoa CCM kwenye madaraka. Wale wenye kufuatilia na kuelewa watakumbuka jinsi Samia alivyojinasibu kama mwanademokrasia wa kweli na kwamba akishindwa uchaguzi atakua tayari kuachia madaraka.

Alivyoingia tu akawaandama vijana wanamapinduzi kama Sabaya na kuunganika na fisadi waliyokua na visasi na kina Sabaya. Akapendwa na wapinga maendeleo na maajenti wa ubeberu kama kina Tony Blair wakapiga hodi ikulu bila shaka kumuonya aachane na umagufuli.

Inaelekea anataka kutimiza ahadi yake ya kuiondoa CCM madarakani kwa kuifanya ichukiwe. Nguvu ya ccm ni kukubalika na umma. Sera zake za kuweka mbele maslahi ya umma na kujali usawa kijamii na kiuchumi kitaifa na demokrasia ndani ya chama ndio nguvu yake.

Inaelekea Samia ndiye atakayeitenganisha CCM na umma wa wananchi. Jinsi anatumia ubabe hadi kujiweka mgombea urais wakati siye wanaccm wanamtaka ndio italeta mgawanyiko na kukiondoa chama madarakani. Samia hakua makamu wa rais ili awe mgombea urais. Alikua rais kutokana na katiba ya jamhuri.

Wanaccm wanataka haki yao kumchagua mgombea urais maana wanataka mtu mwenye sifa kuongoza nchi kufuatana na itikadi ya ccm. Wanaccm na wananchi kwa wingi wana hasira. Samia tuliona akiwarudisha wapinga maendeleo walio msengenya magufuli kwa dharau kwa kua anaipenda Tanzania na watanzania kuliko nafsi yake na wakamwita mshamba.

Chondechonde Samia.
Simile motokari yangu.
 
Hili swala la mgombea maelezo na utaratibu apewe nani hasa?, je kwa walio mpitisha? na wanataka kweli agombee muda huu?, au shida ipo kwa yeye? pamoja na mazingira yaliyo wekwa?, haya mambo ni mawili, isije watu wakalalamika huku nnje una itishwa mkutano una shangaa mtu wa meza kuu ana pendekeza tena jina sawa na ilivyokuwa mwanzo, halafu watu wakapokea na wengine kugomea kulipokea. Ama wajumbe wana codependency?
 
  • Thanks
Reactions: Fbn
Angefuata katiba na mwenyewe na wanachama wengine wanaotaka kugombea urais wangechukua fomu na kupita mikoani kupata wadhamini kama katiba inavyotaka. Angepita mchakato na kuteuliwa pasingekua na neno. Wanaompinga wangefunga mdomo.
 
Angefuata katiba na mwenyewe na wanachama wengine wanaotaka kugombea urais wangechukua fomu na kupita mikoani kupata wadhamini kama katiba inavyotaka. Angepita mchakato na kuteuliwa pasingekua na neno. Wanaompika wangefunga mdomo.
Mzee Kaputula nadhani kama yeye hana makosa sana kwenye hili, issue ni wajumbe waliokuwepo muda ule wakati wa kikao, maana sote tumeshuhudia mambo mazito yana ongelewa watu wamesha inuka na mabango mbele meza kuu aaah aaah kwanini tena waonekane au?

pili haya mambo tunayo sikia ni vema vijana wa sasa hasa wajumbe waeleweshe umuhimu wa kuwa katika hivyo vikao huenda hawajui kwa sasa maamuzi ya nchi yana anzia kupikwa hapo a slight of mistake may take the country to a big thing, kwanini..

Naongea hivi kwasababu ukirejea vifungu alivyokuwa ana tamka mjumbe wa kike alivipindisha na sijui kama kuna mtu alidiriki kulisema hili na alipo pindisha ni kwa kusema wanatakiwa angalau majina matatu, na jina moja ni kati ya matatu, kwahiyo wampitishe...

Kwa katiba ya Chama na maelezo ya mjumbe kweli alikosea kwasabu kiwango cha chini kabisa cha majina yanayo hitajika ni matatu na sio jina moja hasa kwa huu mwaka ambao miaka kumi imesha pita.

Swala moja ni kwamba kwa sasa taasisi zote zitengeneze watu weledi ndani ya vyama hivi ili tusije lichimbia shimo taifa letu..

Pili kama kikao kinachokuja wakipitisha jina kutokea meza kuu unadhani hali itakuaje huko mbeleni?

Na mnacho pinga wanachama ni kwamba aliepitishwa hapaswi kupatiwa tena? Au namna ya accountability yake haina uzito kwa sasa?
 
Ndugu umeelezea vyema.
Mpaka sasa bado namtafakari sana Ng'wasi Kamani na dhamira aliyokuwa nayo ya kuwakosesha wajumbe makusudi!
Huyu ilipaswa afunguliwe mashitaka ya uhaini kutokana na kosa la makusudi alilofanya kuwakosesha wajumbe wenzake na Mwenyekiti wao.
Ona sasa kosa lake linavyokighalimu chama.
 
Hahahaha nyundo nzito hizo, ila kwa sasa hakuna anae tambua chanzo nadhani wengi wataweza peleka lawama kwa mwenye meza ila huku wameacha chanzo halisi
 
Mzee Kaputula nadhani kama yeye hana makosa sana kwenye hili, issue ni wajumbe waliokuwepo muda ule wakati wa kikao, maana sote tumeshuhudia mambo mazito yana ongelewa watu wamesha inuka na mabango mbele meza kuu aaah aaah kwanini tena waonekane au?

pili haya mambo tunayo sikia ni vema vijana wa sasa hasa wajumbe waeleweshe umuhimu wa kuwa katika hivyo vikao huenda hawajui kwa sasa maamuzi ya nchi yana anzia kupikwa hapo a slight of mistake may take the country to a big thing, kwanini..

Naongea hivi kwasababu ukirejea vifungu alivyokuwa ana tamka mjumbe wa kike alivipindisha na sijui kama kuna mtu alidiriki kulisema hili na alipo pindisha ni kwa kusema wanatakiwa angalau majina matatu, na jina moja ni kati ya matatu, kwahiyo wampitishe...

Kwa katiba ya Chama na maelezo ya mjumbe kweli alikosea kwasabu kiwango cha chini kabisa cha majina yanayo hitajika ni matatu na sio jina moja hasa kwa huu mwaka ambao miaka kumi imesha pita.

Swala moja ni kwamba kwa sasa taasisi zote zitengeneze watu weledi ndani ya vyama hivi ili tusije lichimbia shimo taifa letu..

Pili kama kikao kinachokuja wakipitisha jina kutokea meza kuu unadhani hali itakuaje huko mbeleni?

Na mnacho pinga wanachama ni kwamba aliepitishwa hapaswi kupatiwa tena? Au namna ya accountability yake haina uzito kwa sasa?
Wengi wanaamini ulifanyika usanii baada mama na wapambe kuona kuna uwezekano atapingwa kwa wanachama wengine kuchukua fomu. Hebu fikiri kwa nini uitishwe mkutano kwa ajili ya kumchagua makamu mwenyekiti tu. Makamu m/kiti anateuliwa na kamati kuu na h/kuu. Mkutamo mkuu anamuidhinisha tu. Kwa mantiki sahihi na tija kwa chama mkutano mkuu ungeitishwa kuchagua mgombea urais sio kupitisha jina la makamu mwenyekiti wa ccm. Walipanga hivyo kuepa maboya kisha wakachomeka nje ya agenda na kinyume cha katiba kumchagua mgombea urais samia bila kutoa fursa kwa wagombea wengine. Samia alikua anaigiza tu kama hajui mpango mzima. Wenye kuelewa wanajua Nchimbi ni mwanamtandao wa enzi ya lowassa na jk. Hakuwekwa ukatibu mkuu na Samia bure.
 
Ndugu umeelezea vyema.
Mpaka sasa bado namtafakari sana Ng'wasi Kamani na dhamira aliyokuwa nayo ya kuwakosesha wajumbe makusudi!
Huyu ilipaswa afunguliwe mashitaka ya uhaini kutokana na kosa la makusudi alilofanya kuwakosesha wajumbe wenzake na Mwenyekiti wao.
Ona sasa kosa lake linavyokighalimu chama.
Wa kushitakiwa ni katibu mkuu Nchimbi. Yeye ameshiriki kuvunja katiba kisha amezawadiwa kua mgombea mwenza. Huyu ni kundi la wahuni anaosema Polepole. Wanamtandao wa like genge linalodhaminiwa na Rostam Azziz.
 
Back
Top Bottom