Simbu aibuka na Medali ya Fedha Boston Marathon, Marekani

Simbu aibuka na Medali ya Fedha Boston Marathon, Marekani

Melubo Letema

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
431
Reaction score
433
IMG_5129.jpeg
Alphonce Felix Simbu ni mwanariadha wa kimataifa kutoka Tanzania, amechukua medali ya fedha kwa kushika nafasi ya pili kwa muda wa saa mbili, dakika tano na sekunde nne ( 2:05:04) kwenye mashindano makubwa ya Boston Marathon huko Marekani Leo, huku nafasi ya kwanza akichukua mkenya John Korir, huku nafasi ya tatu kuchukuliwa na mkenya Kotut.

Soma Pia: Simbu kupeperesha bendera ya Tanzania Boston Marathon, Marekani
 
Kwa mara nyingine kijana Alphonce Felix Simbu kaipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwenye Boston Marathon kwa kuibuka mshindi wa pili kwa kutumia muda wa masaa 02:05:04

Hatuwezi kufurahia ushindi huu wa Alphonce bila kumpongeza Rais Mama Samia kwa hamasa anayotoa kwenye michezo. Mungu mbariki Alphonce. Mungu mbariki Mama Samia.

Top ten ya wanaume.

1. John Korir (Kenya) 02:04:45

2. Felix Alphonce Simbu (Tanzania) 02:05:04

3. Cybrian Kotut (Kenya) 02:05:04

4. Conner Mantz (United States) 02:05:08

5. Edris Muktar (Ethiopia) 02:05:59
 
Mkenya John Korir alijitahidi kukabiliana na mwanzo mbaya na kumaliza mshindi wa mbio za marathon za Boston Jumatatu, akimaliza katika muda wa saa mbili dakika nne na sekunde 45.

Mshindi huyu wa marathon ya Chicago mwaka 2024 alikabiliana na hali hiyo vizuri na kuwaacha nyuma wanariadha wengine, kabla ya kumaliza mbio hizo akiwa kidedea.

Mwanariadha wa Tanzania Alphonce Simbu alimaliza wa pili katika muda wa 2:05:04, akipambana na Mkenya mwingine hadi mwisho ambapo Cybrian Kotut alikuwa wa tatu kumaliza mbio hizo.

Sisay Lemma wa Ethiopia alishinda mbio hizo za Boston mwaka 2024, akimaliza katika muda wa saa 2, na dakika 6.

Kwa ushindi huu wa Jumatatu, Korir amefanya kama alivyofanya kaka yake, Wesley Korir, aliyeshinda mbio za marathon za Boston mwaka 2012.

Kwa upande wa wanawake Mkenya Sharon Lokedi alishinda katika muda wa saa mbili, dakika 17 na sekunde ishirini na mbili. Mkenya mwingine Hellen Obiri alikuwa wa pili na mwanariadha wa Ethiopia Yalemzerf Yehualaw akamaliza wa tatu.
 
Kwa mara nyingine kijana Alphonce Felix Simbu kaipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwenye Boston Marathon kwa kuibuka mshindi wa pili kwa kutumia muda wa masaa 02:05:04

Hatuwezi kufurahia ushindi huu wa Alphonce bila kumpongeza Rais Mama Samia kwa hamasa anayotoa kwenye michezo. Mungu mbariki Alphonce. Mungu mbariki Mama Samia.

Top ten ya wanaume.

1. John Korir (Kenya) 02:04:45

2. Felix Alphonce Simbu (Tanzania) 02:05:04

3. Cybrian Kotut (Kenya) 02:05:04

4. Conner Mantz (United States) 02:05:08

5. Edris Muktar (Ethiopia) 02:05:59
Muwe mnaacha uchawa.uchawa ukizidi unakuwa ni ukosefu wa akili
 
Mwanariadha mtanzania leo aishangaza dunia baada ya kushika nafas ya pili BOSTON MARATHON 2025, kwa muda wa saa 2:05 huku akitimua mbio kwa pace ya juu bila kuonesha dalili ya kuchoka. Mnyaturu huyo kutoka SINGIDA amewacharaza vikalii wapinzani wake wenye majina makubwa ikiwemo SISAY LEMMA, EVANS CHEBET, DANIEL MATEIKO, CYPRIAN KOTUT, CONNER MANTS....etc
 
Attachments

  • GpEkCqfa0AEZqJJ.jpg
    GpEkCqfa0AEZqJJ.jpg
    226.5 KB · Views: 25
Najiuliza, hawa Wakenya wana nini cha zaidi?
Wamewekeza mno kwenye riadha. Huko Iten, Eldoret kuna kambi za kimataifa za wanariadha. Ni biashara kubwa mno inafanyika. Kimsingi wakenya walishaamua riadha ni biashara yao muhimu. Tanzania pia kuna vipaji vya hatari ila uwekezaji ni mdogo. Kina Simbu wanajigharamia pesa nyingi pamoja na sponsors ndo maana wako fit. Michezo na njaa hazikai pamoja kabisa. Simbu na wakali wengine wana nidhamu ya hali ya juu kwenye riadha ila hela ikisaidia pakubwa.
 
Najiuliza, hawa Wakenya wana nini cha zaidi?
Hawa jamaa ni kabila la KALENJIN wanatokea rift valley, wakina KIPCHOGE,KIPRUTO,KIPTOO,JEPKOSGEI,KIPTUM,JEPCHIRCHIR ukiona mjaluo au mkikuyu anakimbia uyo kavamia fani......ETHIOPIA utakuta kabila la OROMO hawa ata enzi za shule mtu hana zoezi na anapepea kama mshale...TANZANIA utawakuta SINGIDA wanyaturu wana miguu kama penseli, vijiji kama MAKIUNGU,NTEWA,MAMPANDO,IKENGA kule kuna bonde la ufa, na wengine wapo MANYARA wambulu flani, bongo ukikuta mwanariadha mchaga huyo kavamia fani..
 
Lakini mbio fupi kuna wazenji wanafanya vizuri. Na watu wa Mara pia wako poa mbio fupi zisizozidi 1500m
 
Kwa mara nyingine kijana Alphonce Felix Simbu kaipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwenye Boston Marathon kwa kuibuka mshindi wa pili kwa kutumia muda wa masaa 02:05:04

Hatuwezi kufurahia ushindi huu wa Alphonce bila kumpongeza Rais Mama Samia kwa hamasa anayotoa kwenye michezo. Mungu mbariki Alphonce. Mungu mbariki Mama Samia.

Top ten ya wanaume.

1. John Korir (Kenya) 02:04:45

2. Felix Alphonce Simbu (Tanzania) 02:05:04

3. Cybrian Kotut (Kenya) 02:05:04

4. Conner Mantz (United States) 02:05:08

5. Edris Muktar (Ethiopia) 02:05:59
Aisee wewe ni mwehu mno
 
Naam Simbu,September katuletea Gold 🏅 medal from Tokyo.

Hongera kwa kazi nzuri
 
Back
Top Bottom