Shule ya sekondari yenye wanafunzi chini ya mia moja ukigawa asilimia zilizotolewa katika mwongozo wa matumizi zipo shule hazitaweza kujiendesha. Kwa mfano shule yenye wanafunzi chini ya mia moja inapokea kiasi kisichozidi laki 3 kwa mwezi. Pesa hii ilipe posho ya walinzi wawili, itengeneze madawati, ilipe mwalimu au mkuu wa shule kwenda benki na wilayani kusainisha hundi kwa afisa elimu, inunue chaki na madaftari ya maandalio ya masomo ya walimu, shule nyingi vijijini zimeajiri vijana waliomaliza kidato cha sita kufundisha masomo ya fizikia, biolojia na kemia masomo haya walimu waliajiriwa na serikali hawatoshi. Na matumizi mengine yote mliyoainisha kwenye mwongozo wenu. Shule hazitaenda.