Zamazamani
JF-Expert Member
- Jun 13, 2008
- 1,903
- 828
Mkuu,
Salamu kwako,
Napenda kuleta malalamiko yangu kuhusu utendaji wa TANESCO. Ingawa najua siyo habari mpya ila hii inanishangaza sana! Pale mtaani tunapokaa, maeneo ya Victoria, mtaa wa Uporoto kuna tatizo la umeme ambalo limedumu zaidi ya mwaka sasa! Yaani huwa unakatika karibu kila siku na mafundi wakija wanabadilisha kifaa fulani kwenye transfoma then unawaka.
Lakini kesho yake au baada ya muda mfupi tatizo linajirudia. Hali hii imekuwa ikiendelea kila siku! Tumejaribu kuulizia wanasema load imeongezeka nk.
Sasa swali linakuja; ina maana kadhia hii haina mwisho? Mbona imechukua muda mrefu sana kupata ufumbuzi? Tukipgiga simu pale kitengo cha dharura, wanatuambia kwamba wakubwa wanajua na wamekuwa wakiwaeleza! Sasa tupo kwenye Dilemma kuu, hatujui hatma ya hii kitu manake vifaa vyetu vya umeme vimeungua mpaka basi, Inakatisha tamaa!
Naomba uweke siasa pembeni, sasa imekuwa ni ajabu ukiona umeme haujakatika kwa siku mbili, yaani tunashangaa!
Mheshimiwa Waziri, umeshaongea mengi kuhusu kuboresha utendaji tangu umeingia hapo wizarani, Hebu acha mambo ya Siasa. Hebu tunaomba ufanye kitu hapo TANESCO mkoa wa Kinondoni.
Mungu akuongoze!