Simbachawene apigwa dongo na Yaronyo Kicheere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simbachawene apigwa dongo na Yaronyo Kicheere

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sulphadoxine, Aug 3, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Katika gazeti la mwanahalisi la leo tarehe 3/8/2011 page ya 15 kuna waraka wa wiki ulio andikwa na nyaronyo kicheere kama ifuatavyo:-
  "Kwa upande wa simbachawene,ambaye mara nyingi huendesha bunge kutokana na nafasi yake ya uenyekiti na anayejiita mwanasheria mbali na kubana wabunge wa upinzani,Alhamisi iliyopita akichangia hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi,alinukuliwa akisema "law and order (watu kufuata sheria na kuwa watulivu) ni pamoja na kutii amri ya polisi na nsipotii unawashwa"Kwangu mimi kauli na matendo ya simbachawene nayafananisha na majigambo ya dereva wa mkurugenzi wa kampuni anayejiona yeye ni mkurugenzi wa maderva wote wa kampuni au vituko vya mke wa rais yeyote anayedhani naye ni raiswa wanawake wote nchini humo.Katika msimamo huu wa wanaong'ang'ania kuandamana na kupinga amri za polisi "wawashe"au kwa lugha rahisi wapigwe risasi,simbachawene hayuko peke yake.Yaelekea kada huyu wa CCM aliyedai kuwa ni mwanasheria hajui kwamba popote pale duniani watu hufuata sheria na kutii amri halali tu,na siyo mradi amri ya mkubwa.
  Law and orde inafanya kazi pale penye mfumo sahihi wa madarakana kuwepo sheria zisizo kandamizi.Inaonekana simbachawene amesahau kidogo,Waliokuwa wanawalazimisha raia weusi nchini Afrika kusini wafuate sheria na kuwa watulivu,hawakuwa na katiba halali kwa mtazamo wao?Kama ilikwapo,mbona chama cha african National Congress (ANC) kiliipinga kwa udi na uvumba hadi uhuru wa kweli ukapatikana?Je ccm na serikali yake wanaao kejeli wapinzani leo hii,hawajui kuwa sheria za makaburu zilikuwa halali kwa mujibu wa katiba yao?Je kama Nelson mandela na wapigania uhuru wenzake akiwamo Jacob zuma,Thabo mbeki ,walter sisulu,steve biko na chris Hani wangetii sheria hizo na amri zake zilizosheheni ubaguzi,afrika kusini ingeondokana na makucha ya utawala wachache?Jingine ambalo simbachawene anapaswa kuliangalia kama mfano mdogo,ni kuuawa kwa raia watatu mjini arusha wakati wa maandamano yalioitishwa na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)kwamba polisi walioua raia wanadai kutii amri ya wakubwa.Naomba radhi polisi wanijibu swali lifuatalo:Hivi kamanda akitoa amri kwamba -nyuma geuka,shusha suruali ............polisi watatekeleza amri hiyo?Hawawezi ni kwasababu amri hii ni ya mkubwa,lakini si amri halali.Hata simbachawene hawezi kutekeleza amri kama hiyo pale ambapo wabunge wenzake watakapomuamuru amri ambazo si halali"
   
Loading...