Simba yatolewa kwa penati 4 - 3 | Orlando Stadium

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Kabumbu la Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF Confederation Cup (CAFCC), hatua ya robo fainali kuendelea kutimua vumbi leo April 24, 2022 ambapo wenyeji Orlando Pirates anapambana na Mnyama Mkali Mwituni Simba SC, katika mchezo wa mkondo wa pili, kwenye dimba la Orlando Stadium Nchini Afrika Kusini.

Ni mchezo muhimu kwa timu zote mbili kuweka mazingira safi ya kufuzu hatua ya Nusu Fainali, ambapo Orlando wakihitaji ushindi tu huku wakizuia Simba wasipate bao. Na Simba SC anaingia kwenye mchezo huu akihitaji sare ya aina yoyote kuweza kusonga mbele kwani tayari ana mtaji wa bao moja alilopata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa April 17, 2022 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kocha Pablo Franco Martin amesema kuwa wanakwenda uwanjani kujaribu kushinda mchezo huo ili kuweza kutinga hatua ya Nusu Fainali huku Kiungo Left Footer Magician, Rally Bwalya akisema wanajua umuhimu wa mchezo huo.

"Umepita muda mrefu tangu timu kutoka Tanzania kutinga hatua ya Nusu Fainali ya mashindano ya Afrika. Tunajua umuhimu wa mchezo huu. Hautakuwa rahisi kwakuwa Orlando Pirates wapo nyumbani. Lakini Sisi tuna faida ya ushindi wa nyumbani ila hatutatumia kigezo hiki kwenye mchezo huu hivyo tunahitaji matokeo ya ushindi ambayo ni muhimu kuliko kitu chochote". amesema Rally Bwalya.

Simba SC ikishinda mchezo, Tanzania nayo imeshinda mchezo. Kila la heri wawakilishi pekee kutoka Tanzania kwenye michuano ya Kimataifa Simba SC.

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1: 00 Usiku [TZ] saa 12: 00 Jioni [SA] Usikose Ukaambiwa..Jopo zima la Wanasimba Na Wengine na Wadau wa Soka wote tuwepo hapa ubaoni JF.

Kulipewa Mwana Kulitaka Mwana

....... Ghazwat.......


View attachment 2198524

==========================

Kikosi cha Simba SC Kinachoanza

Manula, Israel, Hussein, Onyango Wawa, Henock, Kapombe, Mkude, Mugalu, Kanoute, Sakho.

Akiba

Beno, Kennedy, Nyoni, Mzamiru, Banda, Lwanga, Kagere, Kibu.

=======================

Wakati wowote mpira utaanza kwenye Dimba wa Orlando Stadium michuano ya CAFCC

00' Naaam mpira umeanza | Orlando Pirates Vs Simba SC l dakika 90 za jasho na damu kwa pande zote mbili.

04' Manula anafanya kazi ya ziada kupangua shuti kali kutokana na free kick iliyopigwa na mchezaji wa Orlando.

08' Henock anaokoa mpira ambao ulikuwa hatari lango la Simba, yupo chini baada ya kupata rabsharabsha.

12' Orlando wanashambulia lango la Simba, wanapata kona ambayo haikuzaa bao.

15' Shambulizi la kwanza kutoka Simba lakini Sakho anashindwa kutuliza na mpira unatoka nje..!

17' Manula yupo chini akipatiwa matibabu baada ya kugongana na Pepreh, ameinuka anaendelea | Wawa anaonyeshwa KADI ya Njano

25' Orlando Pirates 0-0 Simba SC.. AGG 0-1, mpira ni mkali kila timu imejipanga kucheza kwa nidhamu.

27' Hotto anapiga free kick lakini mpira unatoka nje ya lango, ilikuwa nafasi nzuri kwa Orlando, salama kwa Simba.

30' Simba wanapata Free Kick, Hussein anapigaa lakini Orlando wanaokoa, Mugalu anaonyeshwa KADI ya Njano | Orlando 0-0 Simba SC..AGG 0-1

40' Hakuna bao huku kila timu ikicheza kwa tahadhar kubwa kuhakikisha hakuna madhara yoyote.

45+3' Kuelekea kuwa mapumziko, wanakwenda Orlando, anapiga shutii, lakini Manula anadaka bila wasiwasi, ilikuwa hatari lango la Simba.

Naaam mpira ni mapumziko ambapo hakuna Timu imeona lango | Orlando Pirates 0-0 Simba SC..AGG 0-1

Kipindi cha pili kimeanza dimba la Orlando Stadium, dakika za kuamua mchezo huku Orlando wakifanya mabadikio..Ametoka Abel Mabaso na ameingia Mntambo.

52' Orlando wanacheza nusu ya lango la Simba, lakini Simba wapo imara

55' Chris Mugalu anaonyeshwa KADI Nyekundu, kwa kumchezea madhambi mchezaji wa Orlando, Simba wapo pungufu, na Daktari wa Orlando pia KADI Nyekundu baada ya kumsukuma Mugalu wakati akitoka uwanjani.

60' Gooooooal... Orlando Pirates wanapata bao la kwanza likifungwa na Kwane Peprah kwa kichwa, hata baada ya mfungaji kuonyesha alikuwa Offside | Orlando Pirates 1-0 Simba SC.. AGG 1-1

67' Simba wanafanya mabadikio ametoka Sakho na Israel na nafasi zao zimechukuliwa na Lwanga na Kagere.

76' Mhango anaingia badala ya Peprah upande wa Orlando Pirates mchezo ni mgumu, Orlando wanaliandama lango la Simba SC.

87' Mabasa anafanya faulo lakini refa anapotezea, mchezo unaendelea, pamoja na kuongoza lakini Orlando wamepanik..!

90+4' Kuelekea kumalizika kwa mchezo huu, Orlando wanapata Kona lakini golikipa manula anadaka..Ilikuwa hatari sana

Orlando wanamiliki mpira kule mbele inapigwa looo njeee, golikipa Manula yupo chini akipatiwa matibabu baada ya kuumia, hata hivyo refa anamuonyesha KADI ya Njano kwa kupoteza muda.

Mntambo anaonyeshwa KADI ya Njano kwa kumchezea madhambi Kagere, presha ni kubwa kwa pande zote.

FT: CAFCC.. Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Orlando anatoka akiwa mbele kwa bao moja kwa bila | Orlando Pirates 1-0..AGG 1-1


==========================


CAF: SIMBA YATOLEWA SHIRIKISHO KWA PENATI 4-3

Timu ya Simba imekwama kufuzu Hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa kwa penati 4-3 katika mchezo wa Robo Fainali dhidi ya Orlando Pirates uliochezwa kwenye Uwanja wa Oralndo Nchini Afrika Kusini.

Katika dakika 90 za kawaida Orlando ilishinda bao 1-0 hivyo matokeo ya jumla kuwa 1-1 kwa kuwa Simba ilipata ushindi katika mchezo wa awali katika hatua hiyo.

Penati za Simba katika mchezo huo ambao straika Chirs Mugalu alipata kadi nyekundu katika dakika ya 58, zilifungwa na Shomari Kapombe, Meddie Kagere na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ wakati Jonas Mkude, Enock Enonga walikosa.

.......Ghazwat.......
 
Ni siku muhimu sana kuweka historia nyingine kwa Lunyasi Simba SC

Kila la kheri Mnyama Mkali Mwituni
Ikiwa tunataka kufuzu, sehemu pekee ambayo Simba Sc inapaswa kuwa SOLID ni eneo la kiungo. Pale kati inabidi watu wacheze mchezo wa jasho na damu ili kuzuia njia zote.

Huku nyuma ikiwa mashambulizi hayatakuwa ni ya mara kwa mara basi kazi haitakuwa ngumu.

Sema unaweza kushanga Pablo akaanza na nyoni,kwa jinsi alivyo kiande.
 
Unajua hata sikuile tunapigwa 4 na Kizer tuliutawala sana mchezo na hata possesion ya team ilikuwa ni kubwa kuliko ile ya Kizer, shida yetu kubwa ilikuwa ni kupanda kupita kiasi ilhali hatuna beki wenye speed ya kuendana na counter attacks na ndiomaana goli zote nne ilikuwa ni matokea ya COUNTER ATTACKS na SET PIECES.

Leo tutulie tucheze mpira kila mchezaji akisimamia eneo lake pila kutoka, katika game ya leo sioni umuhimu wa full backs kupanda juu kabisa. Kapombe na Hussein watulie nyuma, kupanda juu liwe ni jukumu la wingers pekee. Hapo katikati viungo wakabe kwelikweli na sio kwa macho kama ambavyo huwa wanafanya.

Kiufupi, twende na ile approach tuliyoitumia wakati tunacheza na As vita away msimu uliopita, ingawa vikosi ni tofauti.
 
Back
Top Bottom