Simba yatimua wachezaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simba yatimua wachezaji

Discussion in 'Sports' started by Mpita Njia, Sep 23, 2008.

 1. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Imewatimua Ramadhan wasso na Emmanuel gabriel, kisa? wanaihujumu timu
   
 2. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ...Wamo pia Mussa Hassan Mgosi na Haruna Moshi (Boba) ni Utaratibu wa kiswahili wa kuendesha soka.Siamini sana kama wachezaji hao wanaweza kuhujumu timu ikafanya vibaya lazima kuna tatizo la msingi ambalo viongozi wanalikwepa kulitafutia ufumbuzi. Mara nyingi Simba wamekumbwa na tatizo la kushindwa kulipa mishahara wachezaji kwa wakati. Hufikia wakati mwingine wachezaji kudai malimbikizo ya mishahara
  yao kwa miezi mpaka 4. Na mchezaji atakaeonekana yuko mstari wa mbele katika kudai haki yao huonekana ni msaliti huishia kufungiwa kwa madai ya utovu wa nidhamu.

  Viongozi wanasahau kuwa wachezaji ni binadamu wenye familia zao na kazi yao ni kucheza mpira kushindwa kuwalipa mishahara ni kinyume na sheria za kazi. Na umaarufu na sifa wanazopata viongozi hutokana na juhudi za wachezaji uwanjani. Mimi ni shabiki sana wa Simba lakini nimepoteza mapenzi na timu hiyo kutokana na uendeshaji mbovu wa timu. Nina imani maendeleo ya soka Tz na hasa kwa timu hizi mbili Simba na Yanga yatakuwa ni ndoto kama mfumo wa uendeshaji timu hautabadilika. Timu mpaka leo inategemea ufadhili wa kikundi cha watu au mtu fulani sidhani kwa mtindo huo ufadhili utakuwa endelevu..
   
 3. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Ndio tabu ya viongozi wa soka wasiokuwa na ofisi. Yaani klabu kama Simba ina makao makuu mtaa wa Msimbazi ambao uko katikati ya eneo la kibiashara la Kariakoo, inakuwa na jengo lisilokarabatiwa kiasi kile. Ofisi ziko kwenye mifuko ya plastic ya viongozi wanaoishi Mwananyamala na Buguruni, umbeya, majungu, kubweteka na kila aina ya uswahili vimewajaa.

  Wapenzi wa Simba naomba kuwasilisha maombi yangu rasmi kuhamia timu ya Azam kwa muda, nikajifunze jinsi ya kuanzisha timu yangu mwenyewe badala ya kuwa mdhamini ya timu iliyojaa watu ambao hawaambiliki!!!!!!!!!!!!!!!
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Simba sasa yaituhumu uchawi yanga


  Na Erasto Stanslaus

  UONGOZI wa klabu ya Simba umesema kuwa, mchawi namba moja wa kuihujumu timu yao ni mchezaji mmoja wa Yanga ambaye anatumika kuwashawishi wachezaji wao kutokana na ukaribu wake na wachezaji wa klabu hiyo.

  Simba imekuwa na matokeo mabaya katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara na matokeo hayo yanahusishwa na hujuma kupitia kwa baadhi ya wachezaji.

  Kutokana na hali hiyo, inadaiwa timu hiyo imewafukuza wachezaji wake wawili, Emmanuel Gabriel na Ramadhani Wasso huku ikiwaweka katika wakati mgumu wengine watatu Henry Joseph, Mussa Hasan 'Mogosi' na Amani Simba wakisubiri kujadili adhabu ya kupewa.

  Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo, mchezaji huyo amekuwa akitumiwa na watani wao wa jadi kuwashawishi wachezaji hao kwa lengo la kuihujumu timu yao.

  Chanzo hicho kilisema kwamba, tatizo hilo wameligundua na kuchukua hatua ikiwa pamoja na kuwafukuza wachezaji wawili na wengine wakiendelea kuchunguzwa kabla ya kutolewa adhabu.

  Chanzo hicho kiliendelea kupasha kuwa, lengo kubwa la watani wao wa jadi ni kutaka kuivuruga timu yao ambayo imeonekana kuwa na uwezo mkubwa kulinganisha na wao ili kutoweza kuchukua ubingwa katika msimu huu.

  "Ujanja wao tumeugundua na hawatafanikiwa kwani tayari tumeng'oa mizizi yao kwa kuwaadabisha wachezaji hao na malengo yao hayatatimia," kilisema chanzo hicho.

  Baada ya kumaliza matatizo hayo, kikosi chao kinatarajiwa kuwa katika hali nzuri ya ushindani kama walivyokuwa katika michezo ya mwanzo

  Simba waligundua hujuma hizo kabla ya mchezo dhidi ya Polisi Dodoma ambapo wachezaji walioihujumu timu hiyo walikuwa wamepangwa katika kikosi cha kwanza siku hiyo walivuliwa jezi muda mfupi kabla ya mchezo kuanza.

  Majira 24 sept 08
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Simba mmemaliza la Simba wa yuda sasa mnalianzisha lingine...kazi ipo...
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tatizo kubwa ni uongozi, niliwahi kumsikia dalali akisema kuwa hang'oki hata kwa katapila, ina maana kuwa ameamua kuwa dikteta kwani hata wanachama wasipomtaka yeye hatong'oka.
  Viongozi wengine wanataka kuangalia kazi za kocha kiasi kwamba hata upangajiw a timu nalo linakuwa jukumu la viongozi
   
Loading...