Simba yaidai Azam bilioni 1.5/-

Simba yaidai Azam bilioni 1.5/-

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,393
Mabingwa wa Tanzania Simba inaandaa barua ya kudai fidia ya Sh. bilioni 1.5 toka timu ya Azam kutokana na kitendo cha club hiyo kuwashitaki wachezaji 4( agrei morris, erasto nyoni, said morad na deo munishi) kwa madai walipokea rushwa ya sh. Milioni 7 kucheza chini ya kiwango mechi dhidi ya Simba. Hii inatokana na TAKUKURU kusema wachezaji hao hawana hatia.
Mwenyekiti wa Simba Aden Rage amesema tayari klabu imewasiliana na mwanasheria wake ili kuandaa madai kisheria.
Rage anaendelea kusema ni jambo la kuidhalilisha Simba na wana msimbazi wote hatuwezi kuliacha hivihivi.
Source: nipashe
 
Ingagawa mimi si mpenzi wa Simba lakini kitendo cha kusingiziwa wametoa rushwa kuwaonga wachezaji wa timu pizani waliyocheza nayo si kitu kidogo kuachwa kiende hivi hivi. Kwa muono wa kisheria hawa watu wana haki ya kudai haki ya kudhalilishwa na kisheria wana haki ya kudai findia.
Tuje kwa wachezaji wenyewe nao wana haki ya kudai fidia kusingiziwa kuongwa. Maana kipindi wako nje wameadhirika kisakolojia, wamekosa kazi ambayo wanaitegemea siku zote ya kucheza mpira ambayo ndiyo inayowapa kipato. Na kama walikuwa wanalipwa posho (mshahara wa kila mwezi) bado kuna mapato mengine ambayo wamekosa kwa mfano posho ya kusafiri kwenda nje mfano Mnrovia Liberia etc etc.
Mimi ningeshauri nao waone nini nini wafanye japo najua uonga na njaa ya wachezaji wataona wanaharibu kibarua chao cha kila siku, lakini wao kama wachezaji wana haki ambayo inawalinda kisheria
 
Rage hana lolote zadi ya kutaka kurudisha imani ya wapenzi na mashabiki wa Simba.
Wenye haki ya kudai fidia toka kwa Azam walikuwa ni wachezaji na wala sio Simba SC.
Walichofanya Azam ni kuomba wachezaji wao wachunguzwe kwa mujibu wa Sheria za mambo ya rushwa.
Ila sio kwamba waliwapeleka mahakamani kwa mashtaka ya rushwa.

Hivi kama kweli ingethibitika kwamba wachezaji hao walihongwa, Rage angetuambiaje?
 
Huo ni ubabaishaji tu, walie na kujitayarisha kuanguka kwa daraja.

Sorry Simba SC.
 
Tukizipata hizo zinaweza kutufaa sana hasa kipindi hiki ambacho tuna mpango wa kuanza kutengeneza pitch yetu kule Boko.
 
Rage hana lolote zadi ya kutaka kurudisha imani ya wapenzi na mashabiki wa Simba.Wenye haki ya kudai fidia toka kwa Azam walikuwa ni wachezaji na wala sio Simba SC.Walichofanya Azam ni kuomba wachezaji wao wachunguzwe kwa mujibu wa Sheria za mambo ya rushwa.Ila sio kwamba waliwapeleka mahakamani kwa mashtaka ya rushwa.Hivi kama kweli ingethibitika kwamba wachezaji hao walihongwa, Rage angetuambiaje?
kwaiyo we unataka simba wasichukue hatua yoyote wakati jina lao limechafuliwa? Apo rage anamakosa gan? Acha izo ukwel unabidi usimame
 
Ingagawa mimi si mpenzi wa Simba lakini kitendo cha kusingiziwa wametoa rushwa kuwaonga wachezaji wa timu pizani waliyocheza nayo si kitu kidogo kuachwa kiende hivi hivi. Kwa muono wa kisheria hawa watu wana haki ya kudai haki ya kudhalilishwa na kisheria wana haki ya kudai findia.Tuje kwa wachezaji wenyewe nao wana haki ya kudai fidia kusingiziwa kuongwa. Maana kipindi wako nje wameadhirika kisakolojia, wamekosa kazi ambayo wanaitegemea siku zote ya kucheza mpira ambayo ndiyo inayowapa kipato. Na kama walikuwa wanalipwa posho (mshahara wa kila mwezi) bado kuna mapato mengine ambayo wamekosa kwa mfano posho ya kusafiri kwenda nje mfano Mnrovia Liberia etc etc.Mimi ningeshauri nao waone nini nini wafanye japo najua uonga na njaa ya wachezaji wataona wanaharibu kibarua chao cha kila siku, lakini wao kama wachezaji wana haki ambayo inawalinda kisheria
100% mkuu
 
kwaiyo we unataka simba wasichukue hatua yoyote wakati jina lao limechafuliwa? Apo rage anamakosa gan? Acha izo ukwel unabidi usimame

Rage anataka kutumia kivuli cha Azam kuwasahaulisha washabiki wasiendelee na ajenda yao ya kumng'oa madarakani kama alivyowasahaulisha kipindi kile kwa ile rufaa iliyowaondoa TP Mazembe. Kama kweli anachukia club yake kuhusishwa na rushwa mbona alikaa kimya kwa issue ya Ulimboka Mwakingwe kumuhonga Kado wakati wa Simba na Mtibwa? Endeleeni kucheka na Nyani muone mnavyovuna mabua, mtapigwa nyingi mpaka mtie akili.
 
Mtani komaa ulipwe chako...naona msomali anachekelea amepata pa kuwasahaulishia wana Simba
 
Mabingwa wa Tanzania Simba inaandaa barua ya kudai fidia ya Sh. bilioni 1.5 toka timu ya Azam kutokana na kitendo cha club hiyo kuwashitaki wachezaji 4( agrei morris, erasto nyoni, said morad na deo munishi) kwa madai walipokea rushwa ya sh. Milioni 7 kucheza chini ya kiwango mechi dhidi ya Simba. Hii inatokana na TAKUKURU kusema wachezaji hao hawana hatia.
Mwenyekiti wa Simba Aden Rage amesema tayari klabu imewasiliana na mwanasheria wake ili kuandaa madai kisheria.
Rage anaendelea kusema ni jambo la kuidhalilisha Simba na wana msimbazi wote hatuwezi kuliacha hivihivi.
Source: nipashe
hivi hili kimb.a bado lipo Simba luwala??
 
Rage mjanja sana, anajua sana kuwachezea akili wana chama wa simba.....

wanasimba mtaisubiri sana hiyo 1.5 billion
 
Jamaa kashapigia mahesa hela ya kampeni hapo, kwani kwenye mgao wa Dowans hayumo?
 
hapo ni uongo tu unamsumbua huyu msomali na kitu kingine hao kina aggrey mbona awaongei sababu walipewa kweli ndio maana wakakubali kusimamishwa wangekuwa hawakuchukua wangeondoka azam kwanini wamekubali kurudi chukua hatua usikurupuke kama msomali wenu..
 
mkuu naona umekurupuka wakina agrey hawajakubali kurudi azam mpaka wasafishwe
 
mkuu naona umekurupuka wakina agrey hawajakubali kurudi azam mpaka wasafishwe

hakuna kitu hapo mkuu wale mi nawaonea hurumu wasitegemee kitu kama hicho trust me ni sawa na mawazo waliyonayo kina rage..
 
Mi namjua Rage kuliko hata majority ya Wanachama wa Simba....mfano wakati Simba ikivurunda na Rage kukimbilia India ksbb alizozidai ni za kimatibabu si Wanachama wa Simba walikuwa wakijiapiza kuwa akirudi tu wanampiga chini,sikuwaambia kuwa watasukuma gari lake.....nafikiri wote mliona yale yaliyotokea pale JK Nyerere Airport,huyo ndiye Ismael mAden ya mahaRage
 
subiri uitwe mnazi wa yeboyebo tu..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom