Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,504
KLABU ya Simba imeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kufanya uchunguzi sakata ka upangaji matokeo Ligi Daraja la Kwanza.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mwanzoni mwa wiki hii ilizishuda daraja timu zinazodaiwa kupanga matokeo.
Sambamba na uamuzi huo, pia TFF iliwafungia baadhi ya viongozi, wachezaji na waamuzi kwa tuhuma hizo.
Kauli ya Simba imekuja baada ya kipa wao Dennis Richard waliyepeleka kwa mkopo timu ya Geita Gold kufungiwa miaka 10 na kulipa faini ya Sh. milioni 10.
Msemaji wa Simba, Haji Manara alisema kuna kila sababu kwa Takukuru kufanya uchuguzi sakata hilo ili kubaini wahusika zaidi.
Alisema ni kosa kubwa rushwa kuingizwa kwenye michezo kwa lengo la kupanga matokeo.
"Tunaomba Takukuru waingilie kati, pamoja na suala hilo kumalizwa na TFF, lakini tunadhani adhabu zilizotolewa ni ndogo," alisema Manara wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema ili kuoandoa shaka, Takukuru wafanye uchunguzi TFF kutokana na ukweli kwamba, bado kuna mambo mengi yamejificha.
Aidha, Manara alitumia nafasi hiyo kuzungumzia suala la mchezaji Abdi Banda anayetuhumiwa kwa utovu wa nidhamu dhidi ya kocha wake.
"Ameandika barua ya kujitetea kutokana na kosa alilofanya, hata hivyo kamati ya nidhamu na maadili ndiyo itakayoamua suala lake baada ya kukutana," alisema.
Source: IPP