Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 8,274
- 25,322
Beki kisiki wa Mtibwa Sugar, Salim Mbonde
Beki kisiki wa Mtibwa Sugar, Salim Mbonde ametoa siri kwamba amegoma kujiunga na Klabu ya Simba kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo kwa kuwa viongozi wa klabu hiyo kongwe nchini wanataka avunje mkataba wake na wakatamiwa wa Manungu, Turiani ili wamsajili.
Mbonde aliyeonesha kiwango cha juu msimu huu akiwa na kikosi cha Mecky Mexime cha Mtibwa Sugar, alikiri jana kuzungumza na baadhi ya viongozi wa Simba kwa lengo la kutua katika klabu hiyo ya Msimbazi lakini ametia ngumu baada ya kubaini wanataka kumchukua kwa njia 'panya' (zisizo halali).
"Ni kweli Simba wamekuwa wakinihitaji kwa muda mrefu. Nimekataa kwa sababu wananilazimisha mimi ndimi nivunje mkataba na timu yangu wakati taratibu haziko hivyo, ninaweza kucheza timu yoyote kama taratibu za uhamisho wangu zitakamilika kwa kufuata misingi iliyopo, alisema Mbonde.
Mbonde bado ana mkataba wa mwaka mmoja na nusu na vinara hao wa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na taratibu za soka zinakataza klabu kuzungumza na mchezaji ambaye bado ana mkataba na mkataba na klabu nyingine, vinginevyo uwe umebakisha muda chini ya miezi sita.
Simba inayonolewa na Mzambia Patrick Phiri, inasaka beki wa kati na wa pembeni watakaoungana na nahodha, Joseph Owino, Hassan Isihaka na Joram Mvegeke katika kuimarisha safu ya ulinzi iliyotikisika baada ya kuondoka kwa Mkenya Donald Musoti.
Chanzo: Nipashe