Simba wa Lisbon (Celtic ya Mwaka 1967)

C9trix

JF-Expert Member
Oct 26, 2015
213
185
THE LISBON LIONS

Mnamo mwaka alfu tisa mia sitini na saba ndani ya jiji la lisbon nchini Ureno, mabingwa wa soka wa kombe la ulaya mwaka huo Celtic, japo kwa sasa kombe hili hufaamika kama kombe la klabu bingwa barani ulaya.

Walibatizwa jina la simba wa lisbon baada ya kuonesha uwezo mkubwa katika kulisakata kabumbu mithili ya simba aliyejeruhiwa mbugani.

Kikosi hicho cha celtic kiliundwa na nyota kama kapteni wao Billy McNeill, Bobby lennox, jim craig, Bobby Murdoch, Tommy Gemmell, John clark, Willie wallace, Stevie chalmers na Bertie Auld huku Ronnie Simpson akisimama katikati ya milingoti mitatu. Kamanda mkuu wa kikosi hicho alikuwa kocha Jock stein Akisaidiwa na Sean Fallon.

Katika Fainali iliyochezwa tarehe 25 mwezi 5 mwaka 1967, celtic walikutana na intermazionale milan katika mchezo uliomalizika kwa jumla ya mabao mawili kwa moja na celtic kutwaa ubingwa huo.

Intermilan ndio walikuwa wa kwanza kukwamisha mpira kimiani kupitia kwa Alesandro Mazzola dakika saba tu baada ya mchezo huo kuanza, goli hilo lilpatikana kwa kupitia mkwaju wa penati, kunako dakika ya sitini na tatu ya mchezo Tommy Gemmell aliwasawazishia celtic na baadae dakika ya themanini na tatu stevie chalmers aliandika goli la ushindi kwa celtic na kuzamisha jahazi la waitaliano wa Nerazzurri.

Celtic walitumia mfumo maarufu kipindi hicho wa 4-2-4, Yaani mabeki wanne viungo wawili na washambuliaji wanne. Katika mfumo huo viungo wawili hufanya kazi zote mbili kuzuia na kushambulia.

Kwa lugha raisi mfumo huu unafanya team kuwa na washambuliaji sita wakati wanashambulia na mabeki sita kipindi ambacho team inashambuliwa.

Katika kikosi hiko cha celtic, bobby murdoch na Bertie Auld walifanya kazi kubwa wakiwa kama viungo wawili ndani ya mfumo huo wa 4-2-4, mfumo huo pia ulihitaji mabeki kuwa na uwezo mkubwa wa kukaa na mpira, kutembea na mpira na uwezo mkubwa katika upigaji pasi.

Kwa sababu mabeki walitakiwa kuwa na utulivu mkubwa baada ya kupokonya mpira na walitakiwa kuanzisha mashambulizi.

Kwa upande wa waitaliano wa nerazurri baada ya kupata goli dakika ya saba walirudi katika mfumo wa kujilinda wa cenataccio ambao ulitumia wachezaji wote kumi kujilinda.

Cenataccio (1-3-3-3) wachezaji wote watatu waliojipanga katika mistari mitatu wanatengeneza ngome ngumu kwa wapinzani kupenya, na mchezaji mmoja anabaki nyuma ya hizo safu tatu kwa ajili ya kuondoa mipira yote itakayodondoka nyuma ya ukuta.

#Cp succes
 
Back
Top Bottom