Ball possesion haiwezi kuwa hiyo mkuu waambie hao Kiss FM wataje ya ukweli, hao marefa utawasingizia tu kwamba waliibeba Simba, sehemu moja tu ambayo refa alitubeba nayo ni kutompa red Haruna hata jukwaani tulipokuwa tumekaa tuliona hilo na tukasema hapo refa katubeba, lakini ile njano aliyopewa Edward, Cannavaro alisukuma na ingekuwa penati, Cannavaro kamchezea rafu nyingi sana Sunzu mara zote wakati wanawania mpira alikuwa anamsukuma na mwisho refa alikosa uvumilivu akampa red, Mwasika naye alimuchezea rafu Kazimoto lakini mbali na kutopewa kadi hata faulo tu haikupigwa, siwezi kumlaumu refa labda alikuwa mbali na matukio au makosa ya kibinadamu tu lakini huwezi kusema kwamba aliibeba Simba. Wale wasaidizi kama ulikuwa makini kuangalia utaona Bahanuzi alikuwa anabaki peke yake akisubiri kupitishiwa kwa nini asiwe offside na ulitaka mwamuzi msaidizi amwache.
kuhusu kutawala kama dakika 10 za mwisho ilichangiwa na kutoka kwa Mkude na kuingia na kuingia Haruna Moshi, kiungo kilipoteana na baada ya rafu mbaya ambayo Haruna aliifanya nayo mchezoni, kama binadamu isingekuwa rahisi afanye ile faulo halafu aendelee kucheza vizuri hata ukiangalia picha vizuri amekita ule mkuu lakini usoni anaonekana kuumia kama vile yeye ndo alikanyagwa kwa hiyo hata yeye hakuifurahia hiyo faulo ilimtoa mchezoni kiukweli.