Simba vs Yanga michuano ya kimataifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simba vs Yanga michuano ya kimataifa

Discussion in 'Sports' started by Las Mas Bobos, Sep 9, 2012.

 1. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuna hii tabia ya vyombo vya habari vya hapa nyumbani kupenda kuikweza Simba inapokwenda kuiwakilisha Tanzania nje ya nchi. Utasikia watangazaji wanavyoipamba na magazeti yanavyoiandika vizuri na kuibeza Yanga kabla haijaondoka.

  Waandishi hawa wa kichaga wasiojua michezo sijui huwa wana rekodi gani ya Simba yenye kuonesha mafanikio nje ya Tanzania. "..simba ambayo imekuwa na rekodi nzuri katika kuiwakilisha Tanzania nje ya nchi inatarajiwa kuondoka kesho kwenda kukipiga na Haras Al Hadood ya Misri....."

  Wakiwa ni Yanga ndio wanatoka, utaona wakianza kuzungumzwa vibaya hata kabla ya mechi yenyewe. Sasa mimi nauliza swali: KATI YA SIMBA NA YANGA, TIMU IPI IMEWAHI KUBEBA UBINGWA NJE YA NCHI NA KUULETA NYUMBANI?

  Hapa sizungumzii kombe la Maulid linalochezwagwa Zanzibar, manake wengi wenu mnadhani Zanzibar ni nje ya nchi. Kwanza Yanga hawanaga interest na kakikombe ambako mshindi anapata laki 8 ilhali gharama za kuipeleka timu Zanzibar ni 8m.

  Naomba majibu kutoka kwa waandishi uchwara na wapenzi wa hii timu ya kina 'Jumaa' (wafanyakazi wa ndani wa wahindi) yenye maskani sokoni bila uwanja hata wa kupigia dana dana.
   
 2. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pole we Yanga. Kuwa makini na mapenzi ya hizo timu utaumia na kupata wazimu.
   
 3. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  facts and figures huwa zipo tu, hazitungwi!
   
 4. h

  handboy Senior Member

  #4
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 17, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vyombo vya habari vipo sahihi kutokama na ukweli kwamba simba huwa inatuwakilisha vizuri nje tatizo lenu mashabiki wa yanga mmeathiriwa na siasa mbovu za ccccm ie nape mnataka sifa wakati uwezo nothing acheni kufikilia kwa kutumia kucha
   
 5. adakiss23

  adakiss23 JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 3,346
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Simba alishafika fainali ya Confederation Cup mwaka 1993 na pia alishafika nusu fainali Champions League mwaka 1974 kama sijakosea. Na ni juzi 2 walikaribia kufika ktk hatua ya makundi (quarter finals) baada ya kutolewa na Al Ahly Shandy kwa penati 12_11. Nipe rekodi ya Yanga? Halafu jibu baki nalo mwenyewe..

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 6. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye RED ndio panakuombea msamaha, otherwise ungekoga matusi yangu mkuu.

  Kufika fainali si kuchukua kombe. Mimi niliuliza ikiwa mmeshawahi kubeba kitu chochote mkaja nacho nyumbani.

  Na kwa taarifa yako, Yanga ndio timu ya kwanza ya Tanzania kufika Quarter Finals za Champions League. Ni baada ya kuifunga Coffeu ya Ethiopia bao 6-0. Mechi iliyofuata haikuwa nzuri kwetu kwani tulifungwa bao 8 na Raja Casablanca ya Morocco.

  Mara 2 Yanga imekwenda ugenini na kuleta ubingwa wa Africa Mashariki na kati. Narejea swali langu, Simba ilishawahi kuja na medali toka nje?
   
 7. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sijaona ulichoeleza, imetuwakilisha vizuri vipi?

  Yanga ndio imewahi kupanda ndege na kombe, si Simba. Sasa nje wapi huko Simba ilikoenda kufanya ugomvi ikashinda, just tell me niwape saluti.

  Huo ubishi wa kiswahili mimi siuwezi maana umeanza kunichefua na jina la Nape. Hayo ya kwako na Nape endeleeni Lumbumba mnakokutanaga, mimi nauliza hivi: SIMBA AMESHAWAHI KUBEBA NDOO UGENINI?
   
 8. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #8
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,105
  Likes Received: 1,494
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kwamba simba haijawahi kuleta kombe kubwa la afrika ukiacha afrika mashariki na kati lakini imekuwa na rekodi nzuri ya michuano ya kimataifa kulinganisha na yanga mara nyingi yanga imekuwa ikitolewa hatua za awali hata na zile timu zinazooneka dhaifu afrika
  Jaribu kufatilia ushiriki wa yanga kwenye michuano ya kimataifa miaka 5 iliyopita na simba ndio utagundua ukweli
  na hata kwenye ranking za vilabu afrika Simba iko juu
   
 9. B

  Baba Kiki JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 1,366
  Likes Received: 488
  Trophy Points: 180

  Mkuu unazungumzia rekodi nzuri ya jumla kwenye mechi za kimataifa au timu iliyowahi kuchukua kombe ugenini?
   
Loading...