Simba vs Toto Africa

Dakika ya 29: Mchezo umechangamka, Simba wanafanya mashambulizi kutafuta bao la kusawazisha.

Dakika ya 27: Awadhi Juma anakosa bao la wazi, anapata pasi kutoka kwa Lyanga, anaupiga kwa kichwa unatoa kidogo nje ya lango la Toto.





Dakika ya 23: Toto wanaongoza bao 1-0, Simba waliuanza mchezo kwa kasi ndogo, sasa wanaonekana kuanza kuchangamka.

Dakika ya 20: Toto wanapata bao, mfungaji akiwa ni Wazir Junior baada ya kupiga shuti kali nje ya 18 likajaa wazuni moja kwa moja.

Dakika ya 19: Simba wanapata faulo nje ya 18 ya Toto upande wa kulia mwa uwanja, Kessy anapiga lakini kipa wa Toto anadaka na kuupiga mbele.

Dakika ya 16, matokeo bado 0-0, timu zinashambuliana kwa zamu.

Dakika ya 12: Awadhi Juma anapiga shuti kali lakini linatoka nje.

Dakika ya 10: Toto wanapiga faulo lakini inapaa juu ya lango la Simba na kuwa goal kick.

Dakika ya 9 Toto wanapata faulo nje ya 18 ya Simba.

Dakika ya 8: Simba wanamiliki mpira muda mwingi ila bado hawajatengeneza nafasi.

Dakika ya 5: Timu zote bado zinasomana taratibu, mchezo haujawa na kasi kwa timu zote.

Dakika ya kwanza: Mchezo umeanza.

Mchezo utaanza muda wowote kuanzia sasa
 
Dakika ya 31: Kocha wa Simba analalamika kwa mwamuzi, mwamuzi anamtoa nje Kocha Mayanja.

Mayanja ameondolewa kwenye benchi na mwamuzi Ahmada kutokana na kinachoonekana wamepishana kauli.
 
Dakika ya 45+: Beki wa Toto, Yusuph Mlipili anapewa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Kiiza.

Dakika 3 za nyongeza

Dakika ya 45: Kessy anapiga krosi nzuri lakini washambuliaji wa Simba wanashindwa kuitumia vizuri.
 
Dakika ya 47: beki wa Simba, Hassan Kessy anapewa kadi nyekundu kwa kumchezea faulo, Edward Christopha wa Titit, analalamika lakini wenzake wanamtoa nje.Kipindi cha pili kimeanza
 
Dakika ya 50: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Mgosi anaingia Nimubona.

Dakika ya 49: Mohammed Hussein wa Simba napiga shuti linapiga nyavu ndogo na kutoka nje.
 
Dakika ya 58: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Mwalyanzi anaingia Ibrahim Ajib.

Dakika ya 56: Toto wanafanya mabadiliko, anatoka Jama Soud anaingia Salmin Hoza
 
Back
Top Bottom