Ukiangalia vizuri mkanda huo ..mfungaji alipopata mpira kuna wachezaji wa Simba walikuwa wamevuka mstari nwa ngome ya Setif na alipoanza kuambaa nao na kuwalamba chenga walinzi setif wakijirekebisha ..halafu alipoachia kombora mchezaji wa Simba alisubiri mpira ukampita ndo akautokea. lakini tayari shuti la mfungaji lilishatoa jibu...Hongereni Simba!!!
Kuna ndugu mmoja kwenye uzi kasema " foreign legion imnewaokoa simba... nadhani aangalie ligi zingine duniani... Messii wa Barcelona (Hispania), van Parsie wa Arsenal,( England) Eto wa Makhakhachala ( Urusi) na wengine...kwenye Klabu mbali mbali duniani... si wazawa wa nchi hizo lakini wameajiriwa na timu hizo kuzipigia kibarua cha kucheza na kufunga magoli.. kamwe mabao wanayofunga si ya nchi walizotoka bali ya Klabu zilizowaajiri.... Nchi wazilotoka hazina pesa walizozifuata kwenye kalbu wanazochezea!!!!!!!!
Hivyo hivyo Klabu nyingine zinamilikwa na raia wa nchi nyngine.lakini wamiliki hao hawawezi kuzihamishia kwenye nchi walikozaliwa... bado zinabaki ni Klabu za nchi zilipoanzishwa na kusajiliwa... Mpango huu ndo unaoleta hamasa(PASSION) kwenye mchezo na Kuleta raha na UMOJA na MSHIKAMANO na Kufanya Dunia kuwa MOJA!!!