Askari Muoga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 6,113
- 4,655
Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limetangaza kuipoka Simba pointi tatu na mabao matatu ambazo ilipewa kutokana na mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar.
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji imetengua maamuzi yaliyokuwa yametolewa na Kamati ya Saa 72 ya kuipa Klabu ya Simba alama 3 kutokana na kile kilichodaiwa kuwa Kagera Sugar walimchezesha mchezaji aliyekuwa na kadi tatu za njano.
Maamuzi hayo yametolewa leo na kamati hiyo baada ya kuwepo kwa mvutano kwa takribani wiki moja juu ya sakata hilo, ambapo Kagera Sugar walikuwa wamekata rufaa kupinga kupokwa alama 3 walizozitapa kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya Simba. Kagera Sugar walisema kuwa Mchezaji Mohamed Fakhi hakuwa na kadi tatu za njano kama ilivyodaiwa bali alikuwa na kadi mbili.
Kamati ya Katiba ikitangaza maamuzi hayo leo imesema, kikao kilichotoza maamuzi ya kuipa Simba alama 3 hakikuwa halali kwa sababu kiliwashirikisha waalikwa ambao si wajumbe wa kamati hiyo. Kwa maana hiyo, matokeo ya mchezo kati ya Kagera Sugar dhidi ya Simba yanabaki kama yalivyokuwa awali.
Lakini pia Kamati ya Katiba imemuagiza Katibu Mkuu wa TFF, kuwapelekea katika kamati za kinidhamu na maadili baadhi ya watendaji wa Bodi ya Ligi kwa kutowajibika katika nafasi zao na kuipotosha Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi.
Jambo lingine lililoibua mvutano kati ya waandishi na kamati hiyo, ni pale waandishi walipotaka kujua kama mchezaji huyo alikuwa na kadi tatu za njano au mbili. Majibu yaliyotolewa na viongozi wa kamati hayakueleza wazi jambo hilo, na hivyo waandishi wa habari kubaki njia panda.
Aidha kufuatia uamuzi huo, kamati imesema Simba haitoweza kukata rufaa na kwamba hayo ndio maamuzi ya mwisho yaliyotolewa kwa mujibu wa kanuni. Lakini pia wamesema malalamiko yaliyopelekwa na Simba hayakufikishwa kwa kamati ndani ya muda uliotakiwa ambao ni saa 72.
Chanzo: Swahili times