Simba SC Yamfuta kazi Kocha Mkuu, Patrick Aussems

venance7

JF-Expert Member
May 15, 2019
555
1,637
Hatimaye aliyekuwa kocha wa klabu ya Simba Mr "uchebe" ameondolewa kuifundisha klabu hiyo.Kupitia page yake ya Instagram uchebe amethibisha hayo.

ART-700x375.jpg

Kocha wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussems, kupitia akaunti yake rasmi ya Instagram leo Novemba 30, 2019 amethibitisha kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba, kupitia kwa Mtendaji mkuu wa timu hiyo, Senzo Mazingiza, imemtaarifu kwamba, kuanza sasa, yeye sio kocha mkuu wa timu ya Simba SC.
1575267211884.png
 
Mi ni simba ila naona wamekosea kumtimua kwa sababu timu haikuwa katika hali ya hatari.
Wako sahihi mkuu, matumizi ya benchi la ufundi la Simba SC ni makubwa sana ukilinganisha na mashindano waliyonayo kwa sasa.
.
Kocha Patrick aliwekewa target ya kuifikisha timu makundi ya klabu bingwa na kikawekwa kipengele kama atashindwa kuifikisha basi ajitathimini ajitathmini kivipi?
1. Afikirie kupunguziwa mshahara.
2. Afikirie kujiudhuru.
.
Kocha Uchebe aliendelea kubaki kwa sababu kuu moja aliyoitoa nayo ni kwamba wachezaji walioletwa halikuwa chaguo lake isipokuwa Shiboub pekee! Machaguo yake mengine Simba SC walishindwa kuyatimiza kwa sababu wachezaji aliowataka sokoni walikuwa wakiuzwa kuanzia 800 million - 1.5 billion TSH kwa mchezaji mmoja wakati ni pesa ya usajili wa timu nzima ya Simba.
.
Kwa hiyo akawa hana excuse kwa uongozi ndio maana akaendelea, uongozi haukumlazia damu vikao vikawa vingi na yeye kuhusu jambo la kujitathmini ila halikuamuliwa sasa amekucha kujichanganya mwenyewe kwenye hili sakata la Tottenham hotspurs.

Note: hiki ndio kitu cha kwanza kilichomleta Senzo mengine yatafuata sasa tumuunge mkono Dennis Kitambi
 
Kumpiga Chura teke ni kumuongezea mwendo, kila la heri Aussems katika safari yako mpya .
 
Kuondoka kwa Aussems kumewachoma wengi mno huko twiter ni huzuni tupu hakika alikuwa kipenzi cha wengi, mioyo inauma lakini ndio hivyo maisha lazima yendelee

images%20(7).jpeg
images%20(6).jpeg
images%20(5).jpeg
images%20(4).jpeg
images%20(2).jpeg
 
hata sisi yanga.. kuondoka kwa Mwinyi Zahera kuna wanachama wa yanga wengi hatujapenda..

timu zetu zina majungu majungu tu ndio maana hatuendelei..

last week tp mazembe wamefanya anniversary ya kuanzishwa kwake , rais wa fifa, rais wa caf, samuel etoo, kanu, yobo na majembe kibao yameuzuria sherehe...

na jumamos hii zamalek kaenda mazembe kucheza hatua ya makundi klab bingwa africa.. mazembe kashinda 3-0... klab kubwa haziendeshwi kwa majungu
 
Back
Top Bottom