SIMBA SC na Mipango ovyo ya usajili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SIMBA SC na Mipango ovyo ya usajili

Discussion in 'Sports' started by KIM KARDASH, Sep 17, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  SIMBA SC itaiwakilisha Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani na kwa sasa inakabiliwa na jukumu kubwa la kutengeneza timu yake hadi kufika Januari wawe wamekamilika.
  Pilika za kutosha na vurugu ndani yake zinafanyika kwa sasa Simba katika kile unachoweza kukiita kujenga timu- wachezaji wanasajiliwa kwa mamilioni baada ya wiki mbili wanafukuzwa, baada ya kucheza mechi moja au mbili.
  Lino Masombo, Patrick Kanu Mbivayanga, Mussa Mudde na Danny Mrwanda ni baadhi ya wachezaji waliosajiliwa kwa fedha nyingi, lakini wakatemwa hata kabla ya msimu kuanza.
  Usajili wa wachezaji wote hawa wanne unakadiriwa si chini ya Sh. Milioni 100, lakini fedha hizo ‘zimetupwa jalalani’ na sasa unaweza kuhisi hali fulani kutokea tena ndani ya Simba SC.
  Kelele zimekwishaanza juu ya wachezaji waliosajiliwa baada ya kutupiwa virago akina Mudde, Mbivayanga na Masombo, ambao ni Komabil Keita, Paschal Ochieng na Daniel Akuffo kwamba nao ni magalasa.
  Angalau Akuffo hazungumziwi sana kwa sababu katika mechi nne za kirafiki alizoichezea Simba amefunga mabao matatu, lakini mabeki Keita na Ochieng kwa sababu timu hiyo inaruhusu sana mabao kipindi hiki, wao wameingia kwenye ‘zengwe’.
  Nimesoma gazeti la Mwanaspoti jana, Kocha wa zamani wa Yanga, Kenny Mwaisabula anahoji Keita na Ochieng wamefuata nini Simba na kwa kuwa huyu kwa sasa ni Mwandishi wa habari za michezo na mchambuzi na kwa jinsi ambayo viongozi wa sasa wa Simba wanapenda kufanya kazi kupitia vyombo vya habari, nina shaka na mustakabali wa wachezaji hao katika klabu hiyo.
  Magazeti yanaandika Simba ilifungwa na Sofapaka ya Kenya mabao 3-0 Alhamisi katika mchezo wa kirafiki kwa sababu ya kupwaya kwa Keita na Ochieng wanaocheza pamoja katika beki ya kati.
  Tayari huo unachukuliwa kama mwendelezo wa makosa ya Simba katika usajili wa wachezaji wa kigeni, baada ya akina Lino Masombo, Mbiyavanga na Mudde.
  Mara nyingi nawaambia watu, kusajili wachezaji wazuri ni jambo moja na kuwa na timu nzuri ni jambo lingine- timu nzuri ni ile inayotayarishwa taratibu baada ya usajili.
  Mfano mmoja ni jinsi ile timu B ya Simba iliyochukua Kombe la BankABC mbele ya vikosi vya Ligi Kuu vya timu za Azam FC na Mtibwa Sugar- kwa sababu imekaa pamoja muda mrefu na wachezaji wamezoeana.
  Sasa leo Simba inasajili wachezaji wawili kutoka timu na nchi tofauti, inataka ndani ya wiki moja tu wacheze pamoja kwa maelewano, jamani hicho kitu hakiwezekani.
  Miezi miwili iliyopita wakati wa michuano ya Klabu Bingwa Afrka Mashariki na Kati, Kombe la Kagame watu walianza kumkosoa Felix Sunzu- bahati kwake hayupo kwa sasa, lakini kama angekuwepo na matokeo haya, zengwe lingeendelea na upande wake pia.
  Sijui hata hao wanaojiita wachambuzi huwa wanachambua nini- maana tatizo la Simba hivi sasa linaonekana wazi na litahitaji muda kidogo.
  Kifo cha Patrick Mutesa Mafisango ndio kinaitesa Simba kwa sasa- hajapatikana kiungo mbadala wake wa kuiongoza timu. Jamaa alikuwa ana mchango mkubwa sana kwenye timu enzi za uhai wake na kwa kiasi kikubwa ubingwa wa Ligi Kuu ulitokana na yeye.
  Tulikuwa tunaishuhudia Simba inacheza ovyo, inapoteana kabisa msimu uliopita ilipocheza bila Mafisango. Wakati Simba ikiwa inajiandaa na mchezo wa marudiano na ES Setif ya Algeria ilimsimaisha Mafisango kwa utovu wa nidhamu na ilipocheza mechi ya Ligi Kuu na African Lyon bila kiungo huyo, iligundua haiwezi kwenda bila mtaalamu huyo (R.I.P.).
  Ilicheza ovyo na kushinda ‘kizali zali’ 2-0 na baada ya hapo ikamrejesha kundini Mafisango akasafiri na timu Algeria. Huyu ndiye alikuwa mfungaji bora wa timu msimu uliopita kwa mabao yake 10.
  Alikuwa anajua kuichezesha timu- sasa hayupo na bahati mbaya zaidi klabu haijampata kiungo mpya mkabaji, hivyo safu ya ulinzi inakuwa na mzigo mkubwa.
  Katika soka, kitaalamu mabeki wakiwa wanamrudishia mipira mingi kipa basi kuna tatizo kwenye kiungo pale chini katika kuiunganisha timu na hilo ndilo linalojitokeza kwa sasa katika Simba.
  Simba inacheza vizuri ikiwa na mpira, kwa sababu ina viungo wengi wachezeshaji, lakini tatizo linakuja mpira unapohamia kwa wapinzani- wanapita kiulaini na safu ya ulinzi ya klabu hiyo inafikiwa mno, tena kwa urahisi.
  Mipira inapenyezwa mno kwenye eneo la hatari la Simba- sasa wazi hapa kabla ya kuanza kuwatazama mabeki, Simba waimulike safu yao ya kiungo.
  Pamoja na hilo, kubwa ni kwamba bado timu haijazoeana na hilo limetokana na ile wachezaji wanasajiliwa, wanafukuzwa- maana yake kila siku timu inaanza upya na sasa tushukuru pazia la usajili limefungwa hadi Januari, timu haitabomolewa tena.
  Amri Kiemba na Jonas Mkude ndio viungo pekee wakabaji katika Simba kwa sasa ambao siku za karibuni hawapangwi- mi nitabaki kuwa mwandishi na mchambuzi, lakini Profesa Milovan Cirkovick ni kocha na mtaalamu, hivyo anajua anachokifanya.
  IIa nachoweza kumshauri tu, babu huyo wa Kiserbia apunguze kujiamini kwa sababu, maamuzi mengi ya viongozi wa Simba hutokana na presha ya mashabiki au vyombo vya habari.
  Mwandishi mnazi kwa hasira zake, timu yake imefungwa anaweza kuandika kwa jazba bila kuzingatia vigezo wala utaalamu akaponda timu na wachezaji na kiongozi asiye mweledi kesho akafukuza mchezaji. Hiyo ndio soka ya bongo.
  Sasa kama hawa wanaowaponda Ochieng na Keita mapema yote hii, ni kwa sababu ya zile bao tatu za Sofapaka- ila kama Wakenya hao wangepoteza nafasi zote hizo na Simba wakatumia japo nafasi moja kati ya tatu walizopata, mabeki hao leo wasingekandiwa.
  Ufike wakati sasa Simba wakajifunza kuwa na subira. Wakajifunza kutokana na makosa, kwani msimu uliopita walimfukuza Derrick Walullya wakiamini ni galasa, ila alikuja na URA kwenye Kombe la Kagame Julai mwaka huu akacheza soka baab kubwa, udenda ukawatoka.
   
 2. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Tatizo sio kwa simba tuu bali kwa wote simba na Yanga kuhusu usajili wa wachezaji. Kocha wa Yanga hakumtaka Mbuyi twite, ila mashabiki wa timu walimtaka. Ona sasa palivyo na ushindani wa mabeki waki. Jana simba haikumpanga keita wala Ocheng kwa sababu za wasiwasi wa kufungwa. Je hao walikuwa chagua la kocha?

  Hivi vilabu vya simba na yanga badala ya kutilia mkazo kujaza pesa katika kendeleza timu zao za watoto, wao humwaga mapesa katika kusajili wachezaji wenye majina makuu kutoka nje ya nchi. Kama simba na Yanga ikiwa na Tamaa ya kuwa timu kali barani africa kama vile ilivyo TP Mazembe, Tamaa yao wataishi kushuka daraja. Mimi sikuona sababu ya yanga kusajili kavumbagu wakati bahamuzi na tegete walifanya vizuri katika komba la Kagame. tena hata Kelvin Yongani alionesha mpira mzuri, hivyo kumtorosha Mbuyi kutoka usajili wa simba , halikuwa Jambo la maana sana kwa kuimalisha timu. Matokeo yake mchezaji kama Hamisi Gumbo anajikuta nashuka mpira kutokana na kutopangwa.

  swala moja limejitokeza katika kamati za usajili la timu hizi mbili. Baada kuwapata wadau wakuu wa kumwaga mapesa mengi kwa wachezaji nje na ndani ya nchi, naona kuna uroho wa kupata ten percent kutokana na kusajili wachezaji wazuri. Wewe abgalia tuu Yanga ina mabeki saba wa kati! matokeo yake wanajikuta wanacheza mchezo wa kujihami zaidi kuliko wa kushambulia. Hivi ni kweli watapara nafasi ya kuwakilisha nchi tena ktk komba la CAF?

  Simba imeonesha jana kuw aikitumia wachezaji wake wa kizalendo wa zamani wanacheza vizuri sana kuliko akiwepo Keita na Ocheng, sasa kwa nini iliharakisha kuwasajili akina keita keita na ochieng? wanyanga wa sima laziamwazimulike sana kama ti zao za usajili au sivyo safari ya kuwafikia akina super Mazembe na Chelsea arekum haitafika popote.
   
 3. M

  Masuke JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Mkuu Kim Kardash inaonekana habari za Binti Zubeiry unazipenda sana.
   
 4. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Makubwa hayo........
   
 5. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ukweli mtupu,pa'1 sana Kim
   
 6. T

  Tanzania1960 JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jeraha tumelipata sasa tubishane mpaka tutokwe damu zaidi au tutafute dawa na bandaji ili tulitibu jeraha?:nerd:
   
 7. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Namkubali(Bin Zuberi wala sio binti) kwa sababu anafanya kazi yake sio kanjanja,ni mkweli na pia ni rahisi zaidi kwangu kumfikia yeye
   
 8. Bwana Mapesa

  Bwana Mapesa JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,926
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  aibu yanga.jpg


  aishukia yanga.jpg

  HA HA HA KWELI Mapenzi ni upofu.......ukiyaendekeza umekwisha..time will tell and nature will countercheck!
   
 9. B

  Baba Kiki JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 1,368
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Uchambuzi mzuri sana. Kuna tatizo sana katika mfumo mzima wa usajili wa wachezaji. Mbaya zaidi pressure ya mashabiki ni kubwa sana hata wakati wa kuziandaa timu, hivyo naweza kukiri kuwa timu nyingi haziandalizi ipasavyo ila ki ujanja ujanja ili kupagawisha wapenzi
   
 10. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Lakini kweli mmewaacha kina mrwanda kama ilivyokuwa kwa wallulya baada ya kuwasajili kwa pesa nyingi nyie..tuweke mapenzi pembeni benchi la ufundi simba ukimuacha kocha inabidi livunjwe na kamati ya usajili imulikwe
   
 11. Bwana Mapesa

  Bwana Mapesa JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,926
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  mbona kocha wa Yanga amesema wachezaji wamelala WAWILI WAWILI....ha hii kitu imekaaje?
   
 12. Bwana Mapesa

  Bwana Mapesa JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,926
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  mbona huko kwenu kuna pesa CHAFU hutaki zimulikwe?.....kweli chongo ni mfalme wa vipofu.
   
 13. Bwana Mapesa

  Bwana Mapesa JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,926
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
Loading...