Simba SC mbona mmechoka mapema ? hakuna dalili ya ubingwa ..

pilau

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
1,595
450
Kwa mtiririko huu mnaokwenda nao katika mechi mbali mbali kadri ligi inavyoendelea na usajili wenu huu wa kubahatisha usiokuwa na malengo ..... na uongozi huu mbovu ambao haujawahi kutokea uongozi usiokuwa na ufahamu hata wa kujua mchezaji gani wa kumuondoa katika timu mpaka mnafukuza Tambwe, Musoti, mnafukuza Elias Maguli ... mnamwacha Kipa Mapunda na kuharibu kabisa system ya wachezaji vijana waliochipukia akina chanongo, Singano na wenzao..... ubingwa sahauni kabisa mnatia simanzi sisi wapenzi ... kwa hali yoyote uongozi wenu umefikia mahali ambapo hamna tena mbinu za kiuongozi wa mpira kwa kweli tunajuta kuwachagua
 
Simba karibia itasahaulika katika historia ya mpira wa Tanzania,hawana tena hadhi ya kuitwa watani wa Yanga,mchangani kumewanogea.
 
Uongozi huu ni mbovu sana, NAMKUMBUKA SANA AL HAJJ RAGE, angalau tulikuwa tunafurahi mashabiki, ubingwa bila kufungwa na yanga alikuwaga mteja na kimataifa tulikuwa si haba!
Hawa jamaa wa sasa wanaitumia simba kufanya madili yao machafu!
Apewe Mo Dewji timu, sisi tunataka raha ya mafanikio, kubeba vikombe vingi iwezekanavyo! HATUTAKI MIJIHELA YAKE. Tunataka RAHA ya timu yetu kushinda. Nina uhakika timu ikibeba vikombe maana yake kambi ina amani na wachezaji wanatunza vizuri, simba hii ya uongozi wa Aveva hamna kiti kabisa!
NAILILIA SIMBA YANGU.
 
KWA KWELI SIMBA YANGU INANINYIMA RAHA. TATIZO KUBWA VIONGOZI WOTE WAJUAJI. KAMA MDAU ALIVYOSEMA HAPO JUU KITENDO CHA KUWAACHA TAMBWE, MAGULI, IVO NA KUSHINDWA KUZUIA SINGANO ASIONDOKE NA MCHEZO WA KUBADILISHA MAKOCHA KILA WAKATI ITAIGHARIMU SIMBA KWA MUDA MREFU SANA UJAO.
 
Matatizo ya Simba ni mengi. Mimi ni mpenzi mkubwa sana wa Simba lakini sasa hata kuangalia game za Simba katika runinga siwezi kabisa. Nilikuwa sikosi popote Simba inapocheza labda niwe nimebanwa mno na majukumu muhimu. Lakini kwa sasa nimeamua kutokanyaga uwanjani na kuitazama pia.
Kwa wanaoijua Simba miaka 5-10 nyuma wanalijua hili. Simba ya sasa haieleweki hata kidogo.
 
Bundi katua msimbazi, ni bora timu auziwe Mo ili iendeshwe kisasa na tupate matokeo mazuri! La sivyo kwa hali hii tutaisoma namba kweli kweli
 
Back
Top Bottom