Simba SC Kushushwa daraja isipolipa deni la Donald Mosoti

mkolaj

JF-Expert Member
Mar 24, 2014
3,020
1,087
LATEST: Simba imepewa amri na FIFA kuhakikisha inalipa deni la Sh64milioni za Mkenya Donald Mosoti ndani ya siku 30 kuanzia leo, vinginevyo itapokonywa pointi na kushushwa daraja.

TFF nayo ikishindwa kusimamia amri hiyo inafungiwa kushiriki michuano ya kimataifa.

Walifurahia kuyachota Mamilioni ya Etoel du Sahel sasa kibao chawageukia wao.
====================
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), limeipiga faini ya Franc 2,000 za Uswisi (sawa na Sh 4,582,000 za Tanzania), Klabu ya Simba baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupuuza maagizo ya Idara ya Utatuzi wa Migogoro (Desputes Resolution Chamber) ya shirikisho hilo.

Kamati ya idara hiyo iliyokutana na Aprili 20, 2016 huko Zurich, Uswis ilitumia Franc 500 (sawa na Sh 1,145,500) hivyo Simba pia imeagizwa kuzilipa ikiwa ni gharama za kikao cha kufuatilia utekelezaji sakata la mchezaji huyo, raia wa Kenya.

Simba imeelezwa kupuuza kumlipa mchezaji Donald Musoti Omanua kwa wakati tangu mkataba wake uvunjwe. Musoto aliyesajiliwa na Simba msimu wa 2014/15 na kuachwa alilalamika FIFA ambayo iliona ana hoja na hivyo Simba kutakiwa kumlipa dola 29,250 (sawa na Sh 62.8 milioni) na kiasi kingine anachodai ni Dola 600 (Sh 1,290,000) zilizobaki katika usajili ambapo jumla yake ni Sh 64.2 milioni. Pia Mosoti anamlipa Mwanasheria wake dola 2,000 (Sh 4.3 milioni) kwa ajili ya kusimamia kesi hiyo.

Felix Majani, Mwanasheria wa Musoti, ambaye pia ni mmoja wa wanasheria wa FIFA, alifungua kesi katika shirikisho hilo kuwashitaki Simba kwa kukiuka makubaliano ya mkataba na mteja wake.

Kwa kosa hilo Simba inatakiwa kulipa faini ya kiasi hicho cha fedha ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya kupokea barua hiyo ya FIFA iliyoandikwa Mei 3, mwaka huu na kufika Tanzania leo Mei 6, 2016. TFF imekuwa nakala na maagizo kuisimamia Simba inalipa kiasi hicho cha fedha.

Simba imeagizwa kulipa stahiki zote za Mosoti ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya kupokea barua hiyo ya FIFA iliyoandikwa Mei 3, mwaka huu na kufika Tanzania leo Mei 6, 2016.

Katika barua hiyo ambayo TFF ina nakala yake, Simba imepewa amri ya kuhakikisha inalipa na isipotekeleza agizo hilo mara moja itakatwa pointi tatu katika mechi zake Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara –VPL.

FIFA imekwenda mbali zaidi ikisema ikiwa klabu hiyo kama haitalipa katika muda uliopangwa yaani siku 30 kutoka sasa, FIFA itaishusha Simba daraja kutoka Ligi Kuu Tanzania Bara hadi Ligi Daraja la Kwanza au zaidi.

Kwa upande wake, TFF imagizwa kuhakikisha uamuzi huo unasimamiwa vema utekelezwaji wa maagizo hayo vinginevyo itachukuliwa hatua stahiki ikiwamo kuiondoa Tanzania katika mashindano ya kimataifa.
 
Labda kati ya hawa mkuu Mdakuzi Masuke grafani11
Hata JF founder ni mwana msimbazi pia...
Huyu grafani 11 si alipotea mara tu baada ya lile kundi la Ushangiliaji la Simba Ukawa lilipopata ajali. Sijui kama huyu member yu hai. Natamani kuona tena michango yake hapa Jf.
Masuke huyu nadhani anaona aibu tu kuingia humu maana sasa Simba imekuwa kama Jamvi la wageni.
 
dah labda mo awasaidie watani zetu, ina maana dar es salaam derby itakuwa na azam dah! wanatia huruma masikini, tujichange wanayanga wenzangu hata buku-buku
 
dah labda mo awasaidie watani zetu, ina maana dar es salaam derby itakuwa na azam dah! wanatia huruma masikini, tujichange wanayanga wenzangu hata buku-buku
Yule Makofia atazitoa za mfukoni mwake halafu mapato ya uwanjani ya Msimu wote wa Mwaka 2016/2017 atachukua yeye. Makofia anacheza na fursa yule Mzee.
 
Huyu grafani 11 si alipotea mara tu baada ya lile kundi la Ushangiliaji la Simba Ukawa lilipopata ajali. Sijui kama huyu member yu hai. Natamani kuona tena michango yake hapa Jf.
Masuke huyu nadhani anaona aibu tu kuingia humu maana sasa Simba imekuwa kama Jamvi la wageni.
Simba ukawa bado tumo wewe, mnyama for life, ndala goli 5-0 sijui watarudisha lini?
 
Yule Makofia atazitoa za mfukoni mwake halafu mapato ya uwanjani ya Msimu wote wa Mwaka 2016/2017 atachukua yeye. Makofia anacheza na fursa yule Mzee.
Ndiyo mbinu zake kuwakopesha ili walipe na riba humo humo. Pia hawawezi kumtimua maana kila wakati anawadai.
 
LATEST: Simba imepewa amri na FIFA kuhakikisha inalipa deni la Sh64milioni za Mkenya Donald Mosoti ndani ya siku 30 kuanzia leo, vinginevyo itapokonywa pointi na kushushwa daraja.

TFF nayo ikishindwa kusimamia amri hiyo inafungiwa kushiriki michuano ya kimataifa.

Walifurahia kuyachota Mamilioni ya Etoel du Sahel sasa kibao chawageukia wao.
Wana hela za Samatta na Okwi. Teh Teh
 
Jamani Simba hadi wanatia huruma,sasa wakishuka daraja hata ndondo cup si wataikosa?

Maana sioni namna wanayoweza kulipa hizo pesa.
Labda wapitishe bakuli.
simba kwa sasa wana hela nyingi walizopata kutoka kwa okwi na samata
hizi hela kwao ni kidogo. sana watalipa. tu.
 
Simba ukawa bado tumo wewe, mnyama for life, ndala goli 5-0 sijui watarudisha lini?
Huyu jamaa vipi!!!!! Hiyo Simba ukawa ipo wapi! mbona hatuioni au mnashangilia kwa kuvizia siku hizi!! Subir Fifa wawashushe daraji ili mkashitiki Dr. Mwaka Ndondo Cup
 
Mmmh!!! Simba ingekuwa Top kwenye msimamo wa ligi ungesema haya!! Mwaka simba ikifanya vibaya basi tanzania hakuna mpira ikifanya vizuri sifa kedekede.
Team Mikia bwana mna kazi

Sina mapenzi na mpira wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom