- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
- Tunachokijua
- Barbara Gonzalez awali alikuwa mtendaji Mkuu wa Simba SC ambaye alitangazwa na Bodi ya Wakurugenzi Septemba 5, 2020 kuchukua nafasi iliyokuwa imeachwa wazi na Senzo Mbatha ambaye kwa wakati huo alitimkia kwa watani wao Yanga.
Mwezi Desemba 09, 2022 Barbara aliandika barua ya kuachia ngazi ya uongozi huo ambayo ilitoa notisi ya mwezi mmoja hadi Januari 2023 akitaja sababu ya kupisha uongozi mpya.
"Leo nimeandika barua ya kujiuzulu wadhifa wangu kama Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, kuanzia Juanuari mwakani, nimetoa notisi ya mwezi mmoja ili nishiriki kuhakikisha kipindi kizuri cha mpito (transition) na makubaliano (handover) na manejimenti mpya." - Barbara Gonzalez, 2022.
Ipo taarifa inayosambazwa mtandaoni ikidaiwa kutolewa na Simba SC kuwa imemteua Barbara Gonzalez kuwa mtendaji mtendaji mkuu wa timu hiyo.
Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
JamiiCheck imefuatilia kwa njia ya mtandao na utafutai wa maneno muhimu na kujiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani haijachapishwa na Simba SC.
Aidha barua iliyotumika kusambaza taarifa hiyo imebainika kuwa na mapungufu kadhaa yanaoitufautisha dhidi ya barua rasmi ambazo hutolewa na Simba SC, hivyo kudhihirisha kuwa imetengenezwa na wapotoshaji. Sehemu ya mapungufu hayo ni pamoja matumizi ya fonti tofauti na ya Simba SC, pamoja uwepo wa hati mkolezo katika barua hiyo isivyo kawaida.