Simba sc bado inajitafuta haswa katika umaliziaji wa magoli

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,288
12,783
Ni nyota njema kwa kocha Benchikha kwa kuanza vizuri katika ligi ya Nbcpl maana Simba sc toka walipochezea kichapo Cha goli tano dhidi ya mtaani haijawahi kushinda Tena Ila ushindi mkubwa ni droo katika mechi ya ndani na kimataifa pia.

Nimewatazama Simba sc dhidi ya Kagera Sugar FC, Kuna nafasi nyingi sana zilitengenezwa lakini umakini wa kumalizia nafasi za wazi bado upo chini sana Kuna papara nyingi kwa wafungaji.

Ikumbukwe Simba sc wanakibalua kigumu Cha kimataifa dhidi ya Wydad Casablanca, Endapo Benchi la ufundi wasipoyafanyia Yafanyia kazi hayo ni hatari sana kwa timu Kama Wydad Casablanca inayokuja kuwinda point tatu muhimu.

Kocha Benchikha alitoa sababu kuwa "hatukucheza mchezo wetu tuliozoea kwa sababu ya uwanja"

Kocha alizungumza kiufundi na kwa jicho la kawaida tu inaonekana molari ya Wachezaji imeanza kurejea na Mashabiki pia watavutwa uwanjani kwenda kushuhudia mchezo wa Simba sc vs Wydad baada kuona timu Yao imeanza kufufuka.

Maoni Yangu : uwanja mbovu usiwe sababu maana Kuna nafasi za wazi kabisa zilitengenezwa na Mchezaji alibaki na kipa lakini hakufunga, Benchi la ufundi litafute Mwarobaini wa kutibu hili Kama umekosa clear chance kwa Kagera Sugar FC usitegemee kupata nafasi nyingi kwa Wydad Casablanca (timu yenye wachezaji amkini) kwa timu kubwa Kama hii nafasi huwa zinapatikana chache tu.

Nawasilisha hoja.
 
Nyie mnajua kabisa mliwaloga wachezaji wetu kwny ile match...mkawalegeza viungo mkawachapa bakora za kichawi mpk nguvu za kucheza zikaisha ndo wanaanza sasa kujirudi katika hali zao....
😆 😆 😆 😆 😆 😆 😆 😆 😆 😆 😆 😆
 
Nyie mnajua kabisa mliwaloga wachezaji wetu kwny ile match...mkawalegeza viungo mkawachapa bakora za kichawi mpk nguvu za kucheza zikaisha ndo wanaanza sasa kujirudi katika hali zao....
Mashabiki wa Makolo mnawaza kuloga tu.
 
Kama uliangalia mechi ya awali kati ya Wydad na Simba, utagundua Wydad walikuwa na makosa mengi sana kule nyuma kiasi kwamba wachezaji wa Simba wangekuwa na umakini wangepata magoli. Hivyo swala la kusema Wydad wana ukamilifu, Simba hawawezi kupata nafasi nyingi hilo siafikiani na wewe. Simba wanauwezo wa kupata nafasi tena nyingi tu ila shida itakuwa ni kuzitumia hizo nafasi.
 
Kwa tuliocheza mpira tunajua goli alilokosa Malone lilisababishwa na ubovu wa uwanja kwa yeye kutotegemea mpira uendelee kudundadunda ukampoteza timing nzuri ya kuupiga matokeo yake akapaisha.

Pia ule uwanja una sakafu ngumu, ni kama wanachezea kwenye sakafu ya sementi na siyo majani yaliyo kwenye udongo, ule ukijani usikudanganye. Kwa hiyo mchezaji kama hajauzoea, anticipation yake ya kupiga mpira na kuupokea inavurugika na pia kutokana na ugumu wa sakafu miguu inachoka haraka. Ni suala la kiufundi zaidi.
 
Kwa Nini waendelee na hiyo kosa kosa na ndiyo maana nikatoa maoni upatikanaji wa nafasi siyo kila siku siku mzee, wajirekebishe (one chance one goal).
 
Ndio maana nimetoa maelezo kuwa tatizo ni kushindwa kuzitumia nafasi, na sio Simba pekee hata Yanga wamekuwa na tatizo hilo hilo kwenye hizi mechi za hatua ya makundi.

Wewe umesema Wydad hawatoa mianya kufanya Simba wapate nafasi nikakurekebisha kuwa kwa mechi iliyopita Wydad walifanya makosa mengi tu na ile mechi Simba wangekuwa makini katika kutumia nafasi wangeondoka na point. Mapungufu kwa timu zote mbili za Tanzania ni kuzitendea haki nafasi zinazopatikana.

Wydad wanafungika vizuri tu kama uliangalia first leg kule Morocco.
 
Mimi nimesema mianya ipo lakini usitegemee nafasi Kama walizotoa Kagera Sugar FC.
 
Timu ya simba itachukua misimu mingi sana mbele ili kuufikia ule utulivu walioupata misimu kadhaa iliyopita.

Na tatizo lao kubwa lipo kwenye kubadilisha makocha kila mwaka, na hivyo kuuvuruga kabisa mfumo wa timu kwa ujumla wake.
Kweli mkuu wachezaji papara zimekua nyingi.
 
Ni nyota njema kwa kocha Benchikha kwa kuanza vizuri katika ligi ya Nbcpl maana Simba sc toka walipochezea kichapo Cha goli tano dhidi ya mtaani haijawahi kushinda Tena Ila ushindi mkubwa ni droo katika mechi ya ndani na kimataifa pia.

Nawasilisha hoja.
Simba 1
Wydad 2
nipo paleeee
 
Kwa tuliocheza mpira tunajua goli alilokosa Malone lilisababishwa na ubovu wa uwanja kwa yeye kutotegemea mpira uendelee kudundadunda ukampoteza timing nzuri ya kuupiga matokeo yake akapaisha.

Pia ule uwanja una sakafu ngumu, ni kama wanachezea kwenye sakafu ya sementi na siyo majani yaliyo kwenye udongo, ule ukijani usikudanganye. Kwa hiyo mchezaji kama hajauzoea, anticipation yake ya kupiga mpira na kuupokea inavurugika na pia kutokana na ugumu wa sakafu miguu inachoka haraka. Ni suala la kiufundi zaidi.
Na bahati mbaya sana kabla mchezo, hizi kasoro za Uwanja tulikua hatuzijui, tumeshtukizwa tu.
 
Back
Top Bottom