Simba S.C: Msimu wa 2015/2016 Vs Msimu wa 2016/2017.

sembo

JF-Expert Member
May 25, 2011
4,350
3,451
Msimu wa 2015/2016: Vs Msimu wa 2016/2017:.

Kombe la mapinduzi.
2015/2016: Nusu Fainali.
2016/2017: Mshindi wa 2. Ila ni kwa taabu saana, maana nasikia “ndugu zetu” Azam baada ya mechi walilala na viatu kwa muda wa siku 3 mfululizo.

Kombe la Azam Federation.
2015/2016: Robo Fainali.
2016/2017: Bingwa. Na katika hili suala Tanzania inajua na Dunia inajua kua Simba S.C walistahili kukabidhiwa kombe lake mapema kabisa.

Ligi Kuu.
2015/2016: Mshindi wa Tatu.
2016/2017: Mshindi wa 2 katika makaratasi. Ila katika nafsi za wapenda soka wote Duniani, Simba S.C ni Bingwa wa VPL msimu huu wa 2016/2017.

Kwa Takwimu zaidi;
1. Idadi ya Mechi 30.
2. Jumla ya Point; 2015/2016: ni 62 na 2016/2017: ni 68.
3. Magoli ya Kufunga; 2015/2016: ni 47 na 2016/2017: ni 50.
4. Magoli ya Kufungwa; 2015/2016: ni 24 na 2016/2017: ni 17.
5. Idadi ya mechi tulizofungwa; 2015/2016: ni 6 na 2016/2017: ni 4.
6. Idadi ya mechi tulizoshinda; 2015/2016: ni 19 na 2016/2017: ni 21.
7. Idadi ya mechi tulizotoka sare; 2015/2016: ni 5 na 2016/2017: ni 5.

Japo hatujatimiza malengo yetu ya kubeba mataji 3 katika msimu huu, wapenzi na wanachama wenzangu wa Simba S.C tusihuzunike, tutembee vifua mbele kwani;
1. Ukiangalia takwimu hizo kwa umakini mkubwa, utagundua kua Simba S.C ya msimu huu ilikua ni moto wa kuotea mbali.
2. Ukilinganisha na takwimu za wapinzani wetu, utagundua Simba S.C ya msimu huu, si ya nchi hii.

Shukrani Shiza Kichuya.

Ndala tukutane Julius Nyerere International Airport.
 
Umenena vyema chief, Simba taifa kubwa!!..

ombaomba fc, Jana walkuwa wanazimia jamhuri Dodoma as if wao ndio waoligongwa...yaani tumfunge mbao, ombaomba wazimie......vyura bhana!

kwa kikosi hiki cha SIMBA, sina wasiwasi kabisa msimu ujao ndoo ya premier league tunaondoka nayo mapema sana.....

hao ombaomba a.k.a matonya fc, watasubiri sana
 
Umenena vyema chief, Simba taifa kubwa!!..

ombaomba fc, Jana walkuwa wanazimia jamhuri Dodoma as if wao ndio waoligongwa...

yaani tumfunge mbao, ombaomba wazimie......vyura bhana!

kwa kikosi hiki cha SIMBA, sina wasiwasi ndoo ya premier league tunaondoka nayo.....

hao ombaomba a.k.a matonya fc, watasubiri sana

Haha.. Umenena vyema sana Mkuu. Msimu ujao hakuna wa kutukamata.
 
Naona ile ban unayojipiga kila msimu imeisha,tunasubiri mbwembwe zako tena mwanzo wa msimu
 
Haaaaa simba mnajisifu wakati mliongoza ligi kwa tofauti ya point 8 amsemi zimepotelea wapi na mnajisifu kwa magoli kwani bingwa mwaka huu kaamuliwa na nini?
 
Haaaaa simba mnajisifu wakati mliongoza ligi kwa tofauti ya point 8 amsemi zimepotelea wapi na mnajisifu kwa magoli kwani bingwa mwaka huu kaamuliwa na nini?
Hivi Mkuu umeelewa lakini nilichokiandika.. Nilichokiandika ni Tofauti ya Simba ya msimu huu ulioisha na ile ya msimu wa mwaka juzi.
 
Hivi kumbe wale walikua wanajiita wakimataifa hawatopanda ndege tena?
Mkuu Wakimataifa uchwara.. "Wanaweza" wakapanda ila, nauhakika hawatakua na safari zaidi ya 2, mana kama kawaida yao, hatua za mwanzo lazima waage mashindano.
 
Mbao nao, wanakaaaza eti waifunge Simba SC kwenye fainali.
Kwanza Refa aliwabeba sana.
Mchezaji mmoja alishikwa nje ya box akajirusha ndani ili apate penati. na hakupata kadi yoyote.
Goli lao la kusawazisha mchezaji aliotea wazi
kabisa.
Mchezaji wao anazuia mpira kwa mkono ndani ya box, hakupewa kadi ya njano.
Wali mzonga mwamuzi na hawaja onywa.
Sasa naona wameridhika pamoja na TFF kuwabeba kwa kuamua fainali ichezwe Dodoma.
Mbao toka ianzishwe.
Haijawahi kutoka sare na Simba
Haijawahi kuifunga Simba
Mbao FC wangeomba fainali wacheze na Yanga FC. vibonde wao.
Asante Simba FC kwa kuwafunga wote Mbao FC na Yanga FC. Kwenye mzunguko wa pili wa ligi.

Changia hoja usitukane.
 
Msimu wa 2015/2016: Vs Msimu wa 2016/2017:.

Kombe la mapinduzi.
2015/2016: Nusu Fainali.
2016/2017: Mshindi wa 2. Ila ni kwa taabu saana, maana nasikia “ndugu zetu” Azam baada ya mechi walilala na viatu kwa muda wa siku 3 mfululizo.

Kombe la Azam Federation.
2015/2016: Robo Fainali.
2016/2017: Bingwa. Na katika hili suala Tanzania inajua na Dunia inajua kua Simba S.C walistahili kukabidhiwa kombe lake mapema kabisa.

Ligi Kuu.
2015/2016: Mshindi wa Tatu.
2016/2017: Mshindi wa 2 katika makaratasi. Ila katika nafsi za wapenda soka wote Duniani, Simba S.C ni Bingwa wa VPL msimu huu wa 2016/2017.

Kwa Takwimu zaidi;
1. Idadi ya Mechi 30.
2. Jumla ya Point; 2015/2016: ni 62 na 2016/2017: ni 68.
3. Magoli ya Kufunga; 2015/2016: ni 47 na 2016/2017: ni 50.
4. Magoli ya Kufungwa; 2015/2016: ni 24 na 2016/2017: ni 17.
5. Idadi ya mechi tulizofungwa; 2015/2016: ni 6 na 2016/2017: ni 4.
6. Idadi ya mechi tulizoshinda; 2015/2016: ni 19 na 2016/2017: ni 21.
7. Idadi ya mechi tulizotoka sare; 2015/2016: ni 5 na 2016/2017: ni 5.

Japo hatujatimiza malengo yetu ya kubeba mataji 3 katika msimu huu, wapenzi na wanachama wenzangu wa Simba S.C tusihuzunike, tutembee vifua mbele kwani;
1. Ukiangalia takwimu hizo kwa umakini mkubwa, utagundua kua Simba S.C ya msimu huu ilikua ni moto wa kuotea mbali.
2. Ukilinganisha na takwimu za wapinzani wetu, utagundua Simba S.C ya msimu huu, si ya nchi hii.

Shukrani Shiza Kichuya.

Ndala tukutane Julius Nyerere International Airport.
eti "mabingwa kwenye nafsi za wapenzi wa soka".....huu ni ujinga wa kiwango cha gridi ya taifa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom