Simba na Yanga ni kikwazo cha kukua kwa Soka Tanzania...

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
1,946
..kama wengi tulivyotarajia timu yetu ya Taifa imeangukia tena pua. Kwa wale wenye umri kama wangu au zaidi yangu watakumbuka vikosi vya miaka ya 80 vya kina Juma Pondamali, Marehemu Kajole, Jellah Mtagwa, Mohamed Adolph "Rishard", Peter Tino, Mohamed Salim, Omar Hussein, Hussein Ngulungu, Salim Ameir "Bwana Mipango" na wengineo (walicheza fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Lagos).

Japo wengi wa wachezaji hawa walitoka Simba na Yanga, tofauti ya Simba na Yanga za wakati ule na sasa ni kuwa matokeo hayakuwa ya kununua kama ilivyo sasa. Wachezaji walijituma na kushinda uwanjani SIO NJE YA UWANJA - kwa kununua marefa na wachezaji wa timu pinzani ili wacheze chini ya kiwango.

Ugonjwa huu wa kununua ubingwa hapa nchini na kuabishwa Kimataifa uliasisiwa na Azim Dewji na mwenzake (sasa ni marehemu) Abbas Gulamali wakijiita "wafadhili wakuu". Tangu hapo timu yenye pesa ndio hupata ubingwa. Matokeo yake hata timu ya Taifa haipati wachezaji madhubuti.

Maoni yangu:
Tufanye kama Gen Buhari aliezipiga marufuku kwa muda kushiriki ligi "Simba na Yanga" za Nigeria (Enugu Rangers na Ibadan Shooting Stars). Matokeo ya soka la huko tumekuwa tunayaona kwa miaka mingi sasa. Simba na Yanga zikisimamishwa kucheza kwa miaka japo mitatu zitakaporudi hoja ya Usimba na Uyanga unaotawala maamuzi na uendeshaji wa soka letu hautakuwepo na soka letu litakua.
 
Soka la Tanzania lina matatizo mengi sana,baadhi yao ni yafuatayo
  • Maandalizi duni ya wachezaji
  • Wachezaji hawajitumi
  • Uongozi mbovu wa soka
 
Mpira wa sasa ni pesa huwezi fungia simba na yanga cos ya matokeo ya kununua,kama inawezekana wakopwe marefa kutoka nchi nyingine,timu ya taifa ya sasa wachezaji wengi wanatoka nje na azam na sio simba na yanga,ukifungia simba na yanga kuna timu zitashindwa jiendesha mfano african lyon wanategemea kulipa wachezaji wake kwa mapato ya mlango kwenye mechi ya simba au yanga,walicheza african lyon na villa mapato ni laki moja na ushehe,utake usitake simba na yanga ndizo zinazoendesha ligi hata tff wanajua,mechi ya simba na yanga inaingiza hadi mil700,jawabu hapa ni tff kuwa wakali kwa waamuzi wa soka,pil tff ndio chanzo cha matatizo yote haya tff walianzisha academy kuendeleza vipaji nackia imeshakufa,uozo wa kamati ya ufundi wa tff ndio matokeo mabovu ya timu ya taifa,tujipange na tupate watu wenye dhamira ya dhati na timu yetu ya taifa tutafika tu,mpira umebadilika timu kibao maarufu hazijafuzu wap nageria,cameron,africa kusin,misri sembuse ss
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom