Mtoboasiri
JF-Expert Member
- Aug 6, 2009
- 5,101
- 1,946
..kama wengi tulivyotarajia timu yetu ya Taifa imeangukia tena pua. Kwa wale wenye umri kama wangu au zaidi yangu watakumbuka vikosi vya miaka ya 80 vya kina Juma Pondamali, Marehemu Kajole, Jellah Mtagwa, Mohamed Adolph "Rishard", Peter Tino, Mohamed Salim, Omar Hussein, Hussein Ngulungu, Salim Ameir "Bwana Mipango" na wengineo (walicheza fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Lagos).
Japo wengi wa wachezaji hawa walitoka Simba na Yanga, tofauti ya Simba na Yanga za wakati ule na sasa ni kuwa matokeo hayakuwa ya kununua kama ilivyo sasa. Wachezaji walijituma na kushinda uwanjani SIO NJE YA UWANJA - kwa kununua marefa na wachezaji wa timu pinzani ili wacheze chini ya kiwango.
Ugonjwa huu wa kununua ubingwa hapa nchini na kuabishwa Kimataifa uliasisiwa na Azim Dewji na mwenzake (sasa ni marehemu) Abbas Gulamali wakijiita "wafadhili wakuu". Tangu hapo timu yenye pesa ndio hupata ubingwa. Matokeo yake hata timu ya Taifa haipati wachezaji madhubuti.
Maoni yangu:
Tufanye kama Gen Buhari aliezipiga marufuku kwa muda kushiriki ligi "Simba na Yanga" za Nigeria (Enugu Rangers na Ibadan Shooting Stars). Matokeo ya soka la huko tumekuwa tunayaona kwa miaka mingi sasa. Simba na Yanga zikisimamishwa kucheza kwa miaka japo mitatu zitakaporudi hoja ya Usimba na Uyanga unaotawala maamuzi na uendeshaji wa soka letu hautakuwepo na soka letu litakua.