Simba na Nyoso | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simba na Nyoso

Discussion in 'Sports' started by FILOMBE, Jun 8, 2012.

 1. F

  FILOMBE Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari wana JF, nafuatilia kwa makini kipindi hiki cha usajili wa wachezaji wa timu zetu kuelekea msimu mwingine wa ligi kuu ya Tanzania kwa timu zetu hizi za Bongo. Ukifuatilia kwa kina utaona vyombo vingi vya habari vinatupia macho klabu kubwa za Yanga na Simba na sasa kwa kiasi fulani klabu ya Azam.

  Nimesoma na kusikia kwamba klabu ya Simba ina mpango wa kumtupia virago beki wake wa kata Juma Nyoso. Mie, kwa mtizamo wangu naona kama Simba hapo watakuwa wamechemsha kabisa, sababu kubwa wanatoa ni kwamba beki huyu wa kati amekuwa akiigharimu timu. Naomba niseme mie nimekuwa nafuatilia michezo mingi ya klabu ya Simba dhidi ya timu pinzani na sijaona kama Juma Nyoso anastahili kutupiwa vilago.

  My take:

  Klabu za Simba na Yanga ni chanzo cha kuharibu vipaji kwa wachezaji chipukizi, kumbuka suala la Athuman Idd na sasa Kevin Yondan. Jamani wachezaji muwe makini.

  Naomba tujadili.
   
 2. M

  Masuke JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Ni kweli Nyoso ni mzuri ila ni kweli pia Nyoso amekuwa akipata red card rahisi sana na kama viongozi wamepata mbadala mwingine la labda hayupo kwenye mipango ya kocha sioni ubaya wowote wakimalizana naye kwa amani.
   
 3. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mara nyingi issue za aina ya saga la Nyoso na Simba hutokana na falsafa ya Mwalimu husika,inavyoonekana type ya uchezaji wa Nyoso iko tofauti na falsafa ya Mwalimu wa Simba anayoitaka team icheze ndo maana wanaona kama hatawafaa lkn kwa mtazamo wangu kama ni suala la kuigharimu team Nyoso ameisaidia zaidi Simba kuliko kuigharimu,ukichukulia amecheza mechi karibu zote za Simba kwa msimu huu uliomalizika,isitoshe ukichanganya na hili suala la Yondan kuelekea Yanga, Simba watakuwa wamefanya bonge la mistake kama watampoteza Nyoso
   
 4. N

  Ngarna JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,975
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Anselm kazi ya ofisa habari wa Simba itakuwa wazi mkataba wa Kimwanga unaelekea kwisha.Ungefaa kwa kazi
  hiyo kwani ama upo addicted na Simba au wewe ni Simba in disguise.Nasema haya kwa sababu cheki habari zinazohusu
  Simba kwenye posts zako utakuta ni asilimia kubwa sana.
   
 5. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mkuu Ngarna,
  Kama ilivyo kwa Mtanzania yeyote yule,katiba inaniruhusu kutoa maoni yangu kitu ninachokifanya hapa,Simba mimi hawawezi kuniajiri ksbb Mshahara wangu hawatauweza,kama walikuwa wanamlipa Yondani Gross ya Laki 4,mimi wataweza wapi?
   
 6. M

  Masuke JF-Expert Member

  #6
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Huendi kuchukua nafasi ya Yondani utachukua nafasi ya Ezekiel Kamwaga.
   
 7. m

  mmteule JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,004
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280

  nimefurahi sana kwa uzi wako huu... hata mechi ya shandy nyoso hakuwepo ndio maana simba iko nje, ukweli ndio huo watake wasitake. mimi kama shabiki wa simba huwa nina msimamo wangu na kundi langu... kama nyoso angeachwa ktk usajili tungekaa mechi nne bila kwenda uwanjani kuishangilia simba kama maombolezo ya kuondokewa na Nyoso. habari ndiyo hiyo
   
Loading...