Simba mtumieni victor costa kama kiungo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simba mtumieni victor costa kama kiungo

Discussion in 'Sports' started by MTAZAMO, Jul 6, 2012.

 1. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,554
  Trophy Points: 280
  Mimi ni mmoja wa watu tunaoamini Victor Nampoka Costa ni beki mwenye kipaji cha hali ya juu sana na pengine ndiye beki mwenye kipaji kuliko wote hapa tanzania kwa kizazi hiki.

  Majeruhi yameshusha sana kiwango chake lakini hivi karibuni amejitahidi kurejea tena lakini bado hajafikia kiwango chake tunachokijua.Pamoja na yote hayo bado ukiangalia uchezaji wake anaweza kumiliki na kupiga pasi za uhakika kuliko wachezaji wengi sana wa Tanzania ya leo.uwezo wa kukaba ni mzuri pia(ingawa si kama alivyokuwa mwanzo hadi akaitwa "Nyumba").

  Nimeshangazwa na Simba kutaka kumuacha Costa wakati huu kiwango chake kikirejea kwa kasi.naamini wakimtumia kama kiungo atawapa matunda bora zaidi kuliko kucheza namba 5.

  Maoni yangu tu wadau wa Simba.
   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,554
  Trophy Points: 280
  Costa anajua halazimishi soka hata wachezaji wenzake wanamkubali na bado siamini kwamba umri wake ni kikwazo maana mtu kama Juma Nyoso kwa wafuatiliaji wa soka amecheza muda mrefu kuliko Costa mechi za kiushindani ingawa kuna watangazaji wanaamini Costa ni mzee zaidi.
   
 3. T

  TUMY JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kaka timu haipangwi ili kujaza nafasi 11 zinazotakiwa ila lazima comination sahihi itafutwe hivi kweli unaweza mpango Beki Victor Costa kama kiungo, wachezaji huwa wanabadili namba ila huwezi mpanga costa kama kiungo HAIWEZEKANI na kama wewe unajua mpira kweli unaweza kuliona hilo.Ungesema namba zingine kati ya 2 ahdi 5 labda angeweza kuswitch ila si kiungo.
   
Loading...