Simba: Mchezo wetu wa kesho na Al Ahly utakuwa ni wa kupambana ili kulinda heshima

Job Richard

JF-Expert Member
Feb 8, 2013
3,865
2,176
Afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amesema licha ya kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika, lakini mchezo wao wa kesho Aprili 9, 2021 dhidi ya Al Ahly ya Misri utakuwa ni wa kupambana kupata matokeo mazuri ili kulinda heshima.

Barbara amesema “Cha msingi mechi yetu ya Ijumaa ni mechi ya heshima ni kweli tumeingia robo fainali lakini tunahitaji kutoka na alama hapa Cairo tutalinda heshima yetu na kulinda ukubwa na uzito wa timu yetu na pia inawatengeneza soka la wachezaji wetu”.

“Cha msingi wachezaji wapambane kama fainali” Akamalizia Barbara.

Simba ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika, itacheza mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly Ijumaa ya kesho ikitaraji kuwa saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki kwenye dimba la Al Salaam ni si uwanja wa Cairo International.

Akizungumzia mabadiliko hayo ya uwanja, CEO amesmea:

“Leo tumeongea na mratibu mkuu ametoa sababu kwamba kwenye uwanja wa Cairo, klabu ya Zamalek watakuwa na mchezo Jumamosi uwanja wa Cairo , siku moja kabla ya mechi lazima waufanyie mazoezi maalum.

“Kwahiyo walikubaliana kwa pamoja nani atacheza wapi na Al Ahly wameamua na watu wa CAF wahamie uwanja wa Al Salaam ili kusiwe na mgongano kwenye kufanya mazoezi”.

Simba ni kinara wa kundi lake, kundi A akiwa na alama 13, Al Ahly ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 8 zote zikiwa zimefuzu ilhali AS Vita ya DR Congo ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama 4 na Al-Merrik inashika mkia ikiwa na alama 2 huku zikishindwa kufuzu robo fainali.
 
tunatengeneza simu aina zote pamoja na computer, Tunapatika Kariakooo karibu kabisa na stand ya mwendo kasi GEREZANI 0715 378899
Ensemble-cran-tactile-lcd-super-amoled-avec-ch-ssis-pour-Samsung-galaxy-A50-A505F-DS-A505F.jpg
 
Mechi haina presha ni vema tuingize full mkoko iwe kipimo sahihi kwa mechi zijazo
Unaingiza full mkoko kutafuta nini wakati tumeshafuzu?

Ukiingia full mkoko wachezaji wako wakapata majeraha au kadi si itakuwa imeshakupa damage tayari mechi zinazofuata
 
Unaingiza full mkoko kutafuta nini wakati tumeshafuzu?

Ukiingia full mkoko wachezaji wako wakapata majeraha au kadi si itakuwa imeshakupa damage tayari mechi zinazofuata
bora kuingiza full mkoko maana mechi kama hii ya kukamilisha ratiba ukipigwa 5 sijui 4 huko utaonekana haupo seriouz na ni mwepesi tofauti na tunavyodhaniwa tuweke full mkoko ili tujue..
 
bora kuingiza full mkoko maana mechi kama hii ya kukamilisha ratiba ukipigwa 5 sijui 4 huko utaonekana haupo seriouz na ni mwepesi tofauti na tunavyodhaniwa tuweke full mkoko ili tujue..
Utaonekana vipi hauko serious wakati umeweka kikosi ambacho siyo kilichokuwa kinakupa matokeo ?

Kama tunahitaji heshima hata kikosi cha Kina Duchu na Ally Salim kinaweza kupata sare dhidi ya Al Ahly hii
 
Ghafla tu unamsikia mtangazaji anapiga makelele "Khamsa, khamsa, khamsa",!! Ujue tayari, kimenuka.

Kila la heri chama langu simba. Mbele ya Mugalu, hakuna kitakacho shindikana.🥵
 
Utaonekana vipi hauko serious wakati umeweka kikosi ambacho siyo kilichokuwa kinakupa matokeo ?

Kama tunahitaji heshima hata kikosi cha Kina Duchu na Ally Salim kinaweza kupata sare dhidi ya Al Ahly hii
Simba wanahitaji kuweka record ya timu isiyofingwa ambayo Mamelodi ameshindwa kuimantain mpaka sasa. Hivyo mpaka sasa ni Simba pekee ndiyo aliyebaki kuweka hiyo recod ama nae kushindwa kumantain. Hii mechi ina umuhimu wake pia
 
Back
Top Bottom