Ni ishara dhahiri kwamba Simba haiko makini kwenye usajili kama inavyotaka watu waamini. Ikiwa benchi la ufundi la Simba ndio limependekeza jina la Ngassa liingizwe kwenye orodha ya usajili, basi Simba haina benchi la ufundi. Hakuna benchi la ufundi litaloharibu nafasi moja ya usajili kwa kun'gan'gania mchezaji asiye mapenzi nayo. Ikiwa benchi la ufundi halikushirikishwa, maana yake ni kuwa benchi hilo ni boya tu, maamuzi yote ya kiufundi yako kwa uongozi wa timu. Kama ndio hivyo, timu itafika kweli?