Simba kuweka kambi Afrika Kusini

Simba kuweka kambi Afrika Kusini

Jospina

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
2,421
Reaction score
1,395
Simba inajiandaa kuweka Kambi South
Africa kuikabili Yanga October 18,
Taarifa zinasema Simba itaweza kuondoka
kesho au keshokutwa ambapo itaweka
kambi ya muda na itarudi siku moja kabla
ya mechi.
Wachezaji wataondoka wote huku
walioachwa timu ya Taifa wataondoka
kuungana na wenzao mara baada ya mechi


phiri.jpg


Timu ya SIMBA SC inaweza kuondoka nchini kwenda kuweka kambi Afrika Kusini kwa ajili ya mpambano na mahasimu wao, Yanga SC Oktoba 18, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.



Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe yuko Cape Town na kikosi kinaweza kuondoka leo na kurejea Dar es Salaam siku moja kabla ya mechi na watani.



Wacheaji waliopo timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wataondoka Dar es Salaam baada ya mechi na Benin Jumatatu.


Emmanuel Okwi hatakwenda kabisa Afrika Kusini kwa sababu atakuwa kwenye majukumu ya kimataifa kwao, Uganda. Uongozi wa Simba SC ulikuwa unawashughulikia baadhi ya wachezaji ambao hawana pasipoti ili kuhakikisha wanakuwemo kwenye safari hiyo.
Kabumbu Website
 
Mgonjwa atabadilisha vitanda weeeee, ugonjwa utabaki ule ule labda abadishe dawa. Simba kubaki na Okwi itakuwa Simba ile ile, labda wamwingize Msoti.
 
jana jioni kwenye vyombo vya habari tajiri wa simba Zakaria Hans Pop amekanusha safari za omani na huko bondeni
 
wanatoka mbuga gani😛😛😛😛😛:what::what::what::what::what:
 
Mgonjwa atabadilisha vitanda weeeee, ugonjwa utabaki ule ule labda abadishe dawa. Simba kubaki na Okwi itakuwa Simba ile ile, labda wamwingize Msoti.

Sawa sawa lakin tatizo lingine ni wale Simba ukawa ndo source na ya haya yote
 
Klabu ya Simba ni sawa sawa na Chadema tu ambayo walitumia Chopa 3 na wakapata kata3 na Simba nao mechi tatu point3
 
Soka la bongo kweli magumashi, sasa huko south wanaenda kufanya nini au wanaenda kusajil beki!!!! mbona wameenda sana zanzibar kuweka kambi lakini game tatu wakaambulia points 3!! hata wakienda england kuweka kambi bado kichapo kinawangoja..
 
Kwa mazingira yalivyo sasa nadhani ni wazo zuri ili kuandaa vizuri timu sehemu tulivu. Kwa hizi suluhu na wakija kufungwa na yanga kitawaka ni bora wakatulia wakajiandaa kikamilifu ili washinde angalau imani ya mashabiki n morale ya wachezaji irudi
 
Simba inajiandaa kuweka Kambi South
Africa kuikabili Yanga October 18,
Taarifa zinasema Simba itaweza kuondoka
kesho au keshokutwa ambapo itaweka
kambi ya muda na itarudi siku moja kabla
ya mechi.
Wachezaji wataondoka wote huku
walioachwa timu ya Taifa wataondoka
kuungana na wenzao mara baada ya mechi

Kwani hii ni preseason? Kisa Yanga ndo iende South Africa? Je baada ya mechi ya Yanga, Simba akishinda anakabidhiwa kikombe? Uongozi wa hivi vilabu vuwili ni wa kisiasa sana! Natamani siku moja zishuke daraja hizi timu mbili labda soka la bongo litakua.
 
mi naomba kuuliza kwa mwenye uelewa simba ukawa ndo akina nani vile mfano watu wanaounda simba ukawa
 
Kwani hii ni preseason? Kisa Yanga ndo iende South Africa? Je baada ya mechi ya Yanga, Simba akishinda anakabidhiwa kikombe? Uongozi wa hivi vilabu vuwili ni wa kisiasa sana! Natamani siku moja zishuke daraja hizi timu mbili labda soka la bongo litakua.
we mbona haueleweki matatizo ya simba uijumlishe na yanga kwani na yanga naye anakwenda kuweka kambi uturuki? ama unaongea kishabibi tu? tuma bac maombi tff ili wazishushe uridhike
 
Kwa mazingira yalivyo sasa nadhani ni wazo zuri ili kuandaa vizuri timu sehemu tulivu. Kwa hizi suluhu na wakija kufungwa na yanga kitawaka ni bora wakatulia wakajiandaa kikamilifu ili washinde angalau imani ya mashabiki n morale ya wachezaji irudi
Labda wakasajili beki huenda watapata matokeo tofauti na sare vinginevyo ni kichapo tu au sare!!!!
 
Klabu ya Simba ni sawa sawa na Chadema tu ambayo walitumia Chopa 3 na wakapata kata3 na Simba nao mechi tatu point3

Hivi mbona Simba wakifanya huwa mnachonga sana. Basi mfanye nyie tu basi . Wabongo tumetawaliwa na USWAHILI SANA HATA AMBAO HATUISHI USWAHILINI.
 
Kwa mazingira yalivyo sasa nadhani ni wazo zuri ili kuandaa vizuri timu sehemu tulivu. Kwa hizi suluhu na wakija kufungwa na yanga kitawaka ni bora wakatulia wakajiandaa kikamilifu ili washinde angalau imani ya mashabiki n morale ya wachezaji irudi

viogozi wanataka kuwafariji wachezaji
 
Back
Top Bottom