Simba kuwa mabingwa wa champions league Afrika

Watani zangu 100 Likes , toxic9 , Krizy Beat , Sanchez magoli , Van pebles Mtoto halali na hela King Ngwaba , Sesten Zakazaka hivi mmepita hapa naona mwenzenu kanogewa huku anajua mtateremka tu hadi ubingwa. Lol.
Sio kama tutateremka, tunajua fika kua njia ya ubingwa ni ngumu maana timu zote zilizofuzu ni vigogo haswaa vya soka la Afrika

Tunachosema hao ndio size yetu sisi mabingwa wenzao. Kama walivyokufa wale wa Swaziland, wakafuatiwa na Nkana na wengineo basi hata kwenye kuusaka ubingwa wembe na moto ni uleule.

Hamkuamini kama tungevuka hatua ya makundi kwahiyo sishangai kama msipoamini kua uwezekano wa kubeba ndoo upo kwa SSC
 
Aggregate mngewatoa Soura peke yake
Hizo ndio mbinu za mashindano mkuu. Kwenye ligi tunahesabu points. Hata utumie nguvu kiasi gani na ukaifuka timu pinzani magoli hata kumi usipofanya vizuri katika mechi zingine itakugharimu kama ilivyowagharimu AS Vita. Tangia awali Simba waliweka wazi kua wanatafuta points zao tisa kwa michezo ya hapa nyumbani na wakazipata

Game plan Simba wa Lunyasi kwenye michezo ya mtoano itabadilika na litapigwa soka la kimtoano. Na hilo pia SSC wanaliweza. This is.............
 
Ooh. Haya bana Mtani japo mlipo sasa ni Mtoano na kwa ule mwendo wa 5,5 sijui kama hapo mnapopaita kaburini zinaezekana kurudishwa na ushindi kupatikana. Labda mfungwe chache ugenini yaezekana ikawa kweli hiyo ndoto kubwa.
Inawezekana, tupe support yako, ni kutuombea tushinde na sauti yako kwenye kushangilia, hayo tu ndio tunahitaji kutoka kwako
 
Back
Top Bottom