Simba kutumia mbinu za APR kuivaa Mazembe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simba kutumia mbinu za APR kuivaa Mazembe

Discussion in 'Sports' started by kilimasera, Jan 5, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MWENYEKITI wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amesema kikosi chake kitatumia mbinu za timu ya APR ya Rwanda kuifunga TP Mazembe ya DR Congo endapo watapata nafasi ya kucheza na mabingwa hao wa Afrika.

  Katika michuano hiyo Simba imepangwa kuanza kampeni yake kwa kuikabili Elan de Mitsoudje ya Comoro na endapo itaiondosha itakumbana na TP Mazembe.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Rage alisema kuwa historia inaonyesha kuwa APR ndiyo timu pekee ambayo imekuwa ikiisumbua sana TP Mazembe, hivyo watatumia mbinu zao kuikabili.

  "Sina wasi wasi najua TP Mazembe pamoja na umaarufu wao pia wana wababe wao ambao ni APR.

  "Historia inaonyesha kuwa hawa jamaa huwa wanawaweza sana, hivyo nasi tutatumia mbinu zao kuwafunga endapo tutakutana nao,"alisema Rage.

  Alisema kuwa ili kufanikisha azma yao watahakikisha wanacheza mechi ya kirafiki na APR baadaye mwaka huu ikiwa ni kwa kuifuata timu hiyo ya Rwanda ama kuileta nchini.

  "Tupo katika mikakati ya kuhakikisha tunaifuata APR kwao au kuileta hapa nchi kwaajili ya kucheza nayo mechi ya kirafiki nafikiri itatusaidia sana,"alisema Rage.

  Kwa mwaka 2010 pekee, rekodi zinaonyesha ARP na TP Mazembe zilikutana mara tatu ikiwa ni mara mbili katika michuano ya klabu bingwa Afrika na mara moja katika michuano ya kombe la Kagame huku APR akishinda mara mbili kati ya tatu.
   
 2. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  yaani mtoto hajaanza kutambaa teyari wameanza kufikiria kutembea :)
   
Loading...