nilipita pale saa mbili giza liliharibu furaha ya watu lakini njemba moja likamwambia mhudumu awaongezee kila mtu kinywaji anachokunywa na amwambie bei yeye anataka kwenda kumalizana na mpenzi wake ambaye ni shabiki wa Simba,nilicheka sana sijui shemeji yetu aliahidi kutoa nini leo lol!
wadau hata mimi nimeshaiona hii pub..,ila sielewi kwanin owner ametumia hili jina,au anautani na washabiki wa Simba,kibiashara ikoje hii,.jamii imelipokeaje hilo jina +picha yake?
Kibiashara haina noma yoyote. Simba SC hana chake pale, endapo Simba SC angekuwa amesajili hiyo picha ama jina 'SIMBA kapakatwa' kama trade marks pale BRELA basi angeweza kufikisha mahakamani jambo hili. Kwa sasa sidhani kama hata hiyo nembo ya Simba SC kama imesajiliwa, anaweza akaibuka mtani siku moja akachumpa pale BRELA na kuisajili rasmi hiyo nembo yao kisha kuwageuzia kibano Simba waache kuitumia nembo hiyo usishangae!