Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Habari wanamichezo waJF,
Katika halin ya kawaida katika mchezo wa soka, mwanasoka mmoja anaweza kuhama kutoka Club moja kwenda nyingine. Lakini mchezaji mzuri kukaa muda mrefu kwenye Club huleta uimara katika kikosi. Yanga kikosi chao kimekaa kwa pamoja kwa muda mrefu na sasa wanamuongeza beki huyu mahiri kutoka Msimbazi. Sasa itabidi Simba watafute beki wa kuziba nafasi yake yaani atakayesaidiana na aliyepo.
===============================
Kilichobaki kati ya Yanga na beki Hassan Kessy ni kuweka saini kwenye mkataba pekee.
Yanga na beki huyo ambaye mkataba wake Simba unakwisha, wamefikia mwafaka baada ya kukubaliana kila kitu na leo matarajio makubwa atasaini rasmi na kuwa mchezaji wa Yanga.
Si unakumbuka Kessy aliomba apewe jezi namba 25 iliyokuwa inavaliwa na Emmanuel Okwi. Sasa huenda akakabidhiwa leo rasmi.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga, zimesema baada ya kuona hana uhakika wa kubaki Msimbazi, Kessy amefanya mazungumzo na uongozi wa Yanga na wamemalizana kwa kuwa mkataba wake Simba, ‘umeisha’.
“Nakuambia kila kitu kati ya Yanga na Kessy kimeisha. Suala la kusaini ndiyo lilikuwa halijakamilika, ila Ijumaa, mambo yote yanakamilika na Kessy anasaini kuanza kuichezea Yanga,” kilieleza chanzo.
Kessy amekiri kufanya mazungumza na Yanga pia.
“Kweli lakini nafikiri meneja wangu ndiye anaweza kulizungumzia hilo,” alisema.
Alipotafutwa meneja wake, Tippo Athumani ‘Zizzou’ ambaye ni kiungo wa zamani wa Milambo ya Tabora na Coastal Union, pia alikubali.
“Kweli tuko katika hatua nzuri sana ya mazungumzo. Lakini vizuri tukimaliza, tunaweza kuwaeleza kila kitu,” alisema Tippo.