Simba inahitaji mageuzi katika aina ya wachezaji

Ndugu zangu wa simba, shida siyo wachezaji! Shida ni GSM anatuharibia ligi yetu. Hata kule kufungwa na Al Masry, chanzo ni GSM! Hili jambo hatutakiwi kulisahau hata sekunde moja. GSM anadhamini timu 7 kwenye ligi yetu.
Yanva inayocheza local ikashindwa international 😀😀
 
Ni dhahiri Sisi mashabiki wa Simba tuna mapenzi makubwa na timu yetu na tunatamani kuona mafanikio endelevu. Katika kutafakari mwenendo wa timu, ni muhimu kuangalia kwa jicho la tatu aina ya wachezaji ambao watatufikisha kwenye malengo yetu.

Wakati tunawashuhudia wachezaji wengi wa Simba wakitumia nguvu, kasi, na kujituma uwanjani, kuna wasiwasi kuhusu uwezo wao wa kufanya maamuzi sahihi na kuwa na ubunifu katika eneo la mwisho. Mara nyingi, tunaona juhudi kubwa zinazokosa umakini na maarifa yanayohitajika ili kuleta madhara kwa timu pinzani.

Tunahitaji kukiri kuna pengo katika akili ya soka kwa baadhi ya wachezaji wetu. Tunashuhudia wachezaji ambao wanategemea zaidi nguvu na mikimbio kuliko uwezo wa kufikiri na kupanga mashambulizi kwa ufanisi. Matokeo yake, tunajikuta tukipoteza nafasi nyingi na kushindwa kuvunja ulinzi wa wapinzani kwa urahisi.

Ni wakati sahihi kwa uongozi wa Simba kuweka mkazo katika kusajili wachezaji wenye akili kubwa ya soka, kama tunavyoona kwa Clatous Chama, Pacome, Maxi, Fabrice , e.tc . Wachezaji wenye uwezo wa kuona nafasi, kupiga pasi zenye uhakika, na kufanya maamuzi sahihi chini ya presha ndio watakaotupeleka kwenye mafanikio makubwa.

Tusipuuze umuhimu wa kuwa na wachezaji wenye uwezo wa kufikiri na kutumia akili zao uwanjani. Ni muhimu kuwekeza katika wachezaji ambao wanaweza kuleta ubunifu na mbinu mpya katika safu yetu ya ushambuliaji.

Tunahitaji timu ambayo ina mchanganyiko wa nguvu na akili. Kuwa na wachezaji wenye uwezo wa kufikiri na kutenda kwa usahihi ndio tutaweza kushinda mechi na kufikia malengo yetu.

Simba inahitaji mageuzi katika aina ya wachezaji ili kuhakikisha tunakuwa na timu imara na yenye uwezo wa kushindana katika ngazi zote(Yanga) . Ni wakati wa kuwekeza kwenye akili ya soka kwa manufaa ya timu yetu.
Yaani wachezaji wanaocheza robo fainali eti sio wazuri bali wachezaji walioishia ngazi ya makundi ndio wazuri? Haki ya Mungu Tanzania SIHAMI hata Trump akinipa Green Card aliyoisaini personally!!
 
Hivi hii timu ya simba ina recruitment staff ?
Hivi huwa wanaangalia profiles za players wanaoendana na system of playing ya timu au huwa wanasajir tu?
 
Simba tunajifariji sana lakini kiukweli hii timu bado sana. Tunatakiwa mwanza kupata mtu mwenye utaalam wa kusajili wa chezaji. Hata kocha bado hatuna. Bora tumpe timu kaseja
 
Ni dhahiri Sisi mashabiki wa Simba tuna mapenzi makubwa na timu yetu na tunatamani kuona mafanikio endelevu. Katika kutafakari mwenendo wa timu, ni muhimu kuangalia kwa jicho la tatu aina ya wachezaji ambao watatufikisha kwenye malengo yetu.

Wakati tunawashuhudia wachezaji wengi wa Simba wakitumia nguvu, kasi, na kujituma uwanjani, kuna wasiwasi kuhusu uwezo wao wa kufanya maamuzi sahihi na kuwa na ubunifu katika eneo la mwisho. Mara nyingi, tunaona juhudi kubwa zinazokosa umakini na maarifa yanayohitajika ili kuleta madhara kwa timu pinzani.

Tunahitaji kukiri kuna pengo katika akili ya soka kwa baadhi ya wachezaji wetu. Tunashuhudia wachezaji ambao wanategemea zaidi nguvu na mikimbio kuliko uwezo wa kufikiri na kupanga mashambulizi kwa ufanisi. Matokeo yake, tunajikuta tukipoteza nafasi nyingi na kushindwa kuvunja ulinzi wa wapinzani kwa urahisi.

Ni wakati sahihi kwa uongozi wa Simba kuweka mkazo katika kusajili wachezaji wenye akili kubwa ya soka, kama tunavyoona kwa Clatous Chama, Pacome, Maxi, Fabrice , e.tc . Wachezaji wenye uwezo wa kuona nafasi, kupiga pasi zenye uhakika, na kufanya maamuzi sahihi chini ya presha ndio watakaotupeleka kwenye mafanikio makubwa.

Tusipuuze umuhimu wa kuwa na wachezaji wenye uwezo wa kufikiri na kutumia akili zao uwanjani. Ni muhimu kuwekeza katika wachezaji ambao wanaweza kuleta ubunifu na mbinu mpya katika safu yetu ya ushambuliaji.

Tunahitaji timu ambayo ina mchanganyiko wa nguvu na akili. Kuwa na wachezaji wenye uwezo wa kufikiri na kutenda kwa usahihi ndio tutaweza kushinda mechi na kufikia malengo yetu.

Simba inahitaji mageuzi katika aina ya wachezaji ili kuhakikisha tunakuwa na timu imara na yenye uwezo wa kushindana katika ngazi zote(Yanga) . Ni wakati wa kuwekeza kwenye akili ya soka kwa manufaa ya timu yetu.
Kama utadhani ni wachezaji ndio wenye shida utakuwa umekosea.
Tatizo hapo ni kocha.
Mwalimu hapo ndipo kazi yake ilipo.Kutengeneza mifumo ya kutoa nafasi kwa wachezaji kuonesha uwezo wao.

Akili tu ya mwalimu ndiyo inatakiwa
 
5imba inahitaji watu makini na wenye maono kama Hersi na Arafat, kumtegemea Magori awasajilie wachezaji ni vituko 😀
 
Yanga inasajili Max nzengeli, Aziz ki, Pacome, Mzize nk. Wenzetu mkasajili Jean ahoua chapombe, Elias mpanzi mikimbio, Mukwala na Ataiba aliyepewa jina la messi 😀 Ngoja tuone
 
Na mkafurushwa pia mkiwa kwenu.
😂😂😂😂😂😂
 
Yaani wachezaji wanaocheza robo fainali eti sio wazuri bali wachezaji walioishia ngazi ya makundi ndio wazuri? Haki ya Mungu Tanzania SIHAMI hata Trump akinipa Green Card aliyoisaini personally!!
Akili yako haina akili. Hivi, umeshindwa kutuliza kichwa na kusoma kilichoandikwa na ukaelewa?
 
Wewe ndio huna akili. Wachezaji wa Simba kwa Afrika wanalinganishwa na wachezaji wa Alhaly, Mamelodi, Wydad na Esperance. Yaani wakubwa wenzie! Usirudie tena!!
 
Unaweza ukaniletea source ya taarifa yako?
 
Back
Top Bottom