Simba - chelsea/liverpool atafuna mzee dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simba - chelsea/liverpool atafuna mzee dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lutala, Mar 9, 2011.

 1. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Aliyejeruhiwa na simba adai aliponzwa na fulana nyekundu
  NA MOSHI LUSONZO
  8th March 2011
  B-pepe
  Chapa
  Maoni

  Hatimaye mtu aliyejeruhiwa kwa kushambuliwa na simba katika eneo la Mbagala, jijini Dar es Salaam, Hamisi Yasin, maarufu kwa jina la “Tumbo” (40), amesimulia mkasa mzima na kusema fulana nyekundu ndiyo iliyomponza hadi akashambuliwa na mnyama huyo.
  Hata hivyo, katika tukio hilo lililotokea asubuhi ya Jumapili iliyopita, Tumbo alijeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kulazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
  Akizungumza akiwa wodi ya Mwaisela, alisema katika tukio hilo, alifanya jitihada kubwa za kujiokoa kutoka katika mdomo wa simba aliyedhamiria kumuua kwa kumvunja shingoni.
  Alisema siku ya tukio alikuwa miongoni mwa watu waliokwenda kushuhudia kuwapo kwa simba huyo mtaani kwao, lakini alipofika eneo hilo alikumbana na tukio hilo la kushambuliwa na simba huyo jike.
  Alisema kipidi hicho alikuwa amevaa fulana nyekundu yenye maandishi ya ‘Mancherster United’, hivyo wakati anasogea karibu na wenzake waliokuwa wamesimama, ghafla Simba aliruka na kuanza kumfuata kwa kasi.
  Baada ya kuona hali ya hatari, alikimbilia katika kundi la watu, lakini simba huyo aliwaacha watu wengine na kumfukuza yeye kwa kasi.
  Alisema jambo hilo lilimfanya akimbilie kwenye mti wa mnazi, ambako alianza kuzungushana yeye akiwa mbele na simba nyuma hadi alipopigwa na mkono wa simba huyo na kuanguka chini. Alisema baada ya kuanguka chini, mnyama huyo alisimama juu yake na hapo ndipo alipoanza harakati ya kutaka kumng’ata shingoni, huku yeye akiweka mikono yake kumzuia.
  “Niliona bora aniue kwa kunitafuna sehemu nyingine na wala sio shingoni. Tulishindana kwa muda wa dakika tano, huku nikiwa pale chini. Aliniparua makucha sehemu ya mkono ili niachie, lakini sikuachia,” alisema.
  Alisema kutokana na kelele walizokuwa wakipiga watu pamoja na vurugu za watu kukimbia ovyo, alimuachia na kukimbilia maeneo ya bondeni, ambako polisi walimfuata na kumuaa kwa risasi. Afisa Uhusiano wa MOI, Almas Jumaa, alisema mgonjwa huyo kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu ya haraka.
  Hata hivyo, alisema juhudi zinafanyika kumuwekea bendeji ngumu (POP) ya kuzuia maambukizo katika sehemu zilizoonekana kujeruhiwa vibaya.
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  ''Heading-holy crappiest''
   
Loading...