Simba bajeti Shs1.5 bil, usajili 375m | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simba bajeti Shs1.5 bil, usajili 375m

Discussion in 'Sports' started by kilimasera, May 3, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  UONGOZI wa klabu ya Simba unaandaa bajeti ya shilingi 1.5 bilioni huku ikipanga kutumia sh.375 milioni kwa usajili msimu ujao, huku wakitoa saa 48 kwa wapangaji wao kusaini mkataba mpya.

  Akizungumza na wanahabari jijini jana, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema kuwa kwa sasa wanataka klabu hiyo ijiendeshe yenyewe na majengo hayo ya mchango mkubwa katika kufikia bajeti hiyo ya mwaka na kufanikisha wa usajili wa wachezaji wapya ambao bajeti yake ni sh.375m.

  Alisema kutokana na matatizo yalitokea mwanzoni ya kutoheshimu mkataba wa majengo yao uliofanywa na uongozi uliopita kwa kuchukua fedha kinyume na utaratibu. Simba imeshatoa saa 48 kuondoka kwa wapangaji hao.

  ''Nataka klabu ya Simba ijiendeshe yenyewe iweze kusajili wachezaji kwa fedha zao wenyewe siwezi kukubali kuona mali za Simba zinateketea kinyuma na utaratibu huo kama kuna mpangaji yoyote ataamua kuingia mkataba na uongozi wangu basi ndani ya saa 48 awe amefanya hivyo na wamepanga kwenda mahakamani ili waweze kupewa oda ya kuwatoa wapangaji hao,'' alisema Rage.

  Rage alisema fedha hizo zinatosha kusajili wachezaji wazuri na wenye uwezo wa kuipa mafanikio Simba.

  Juu ya uchaguzi mkuu wa klabu hiyo ambao utafanyika Mei 15, alisema kuwa mwanachama yeyote ambaye hajalipia kadi yake ya uanachama mpaka siku ya mkutano huo hataruhusiwa kuingia kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay.

  Alisema wanachama wote wanatakiwa kulipia kadi zao katika benki ya CRDB na risiti wanatakiwa kuipeleka klabu kwa ajili ya kupata kadi ambayo ndiyo kibali cha kuingia katika mkutano huo, kwani hadi sasa wanachama waliolipia ni 45 tu na wanatakiwa kulipia 12,000 ya kadi na 20,000 ya uwanja kama walivyokubaliana katika mkutano uliopita.

  Rage alisema katika mkutano huo, wakaguzi wa hesabu za Simba watakuwepo kwa ajili ya kutoa ripoti yao na wao kama uongozi utawasilisha bajeti yao ya mwaka kwa wanachama wao ambayo ni Sh 1.5 bilioni na wanachama na wao ndio wataamua kama inafaa au la.

  Mwenyekiti huyo alizungumzia pia ujio wa mabingwa wa Kombe la Ligi Birmingham kwa ajili mechi mbili za kirafiki dhidi ya Simba na Yanga hapo Julai 7 na 12.

  Alisema kuwa viongozi wawili wa timu hiyo ambao ni kocha msaidizi Andy Watson na daktari Johnlan MC Guinness watawasili nchini Mei 9 kwa ajili ya kukagua hoteli ya Kempinski na uwanja.

  "Timu hiyo ikiwa na kikosi kipya walichokisaji pamoja na mashabiki wao 1,000 watatua nchini Julai 5 na kucheza dhidi ya Simba hapo Julai 7 na siku tano baadaye watacheza na Yanga.

  Wakati huo huo, Rage ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini, alisema wameingia mkataba wa miaka miwili na kocha Moses Basena, lakini atakuwa chini ya uangalizi wa miezi sita.

  "Basena ametia saini na amerudi Uganda, atarejea nchini Mei 9, na timu itaingia kambini siku moja baadaye kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Kagame itakayoanza kutimua vumbi Juni 21 nchini Sudan.

  Rage pia, aliwataka wachezaji wao waliowasimamisha Kelvin Yondan na Mussa Hassan Mgosi kujieleza kwa maandishi kuwa wamekwisha tuma barua ya kuomba msamaha, lakini kamati bado hawajazipitia.
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Kwa 375mil nadhani wanaweza kumsajili hata Fabriges!
   
 3. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #3
  May 3, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Sasa nimeamini tz tunaanza kuviendesha vilabu vyetu kibiashara!

  Hongera rage idumu simba
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  mh! kumbe hizi timu zina esa ya kutosha eeenh. angetaja na mishahara ya wachezaji basi tuone km wanalipwa vya kutosha au ndo ubabaishaji ule ule tu
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli kama mipango itaenda kama Rage anavyoelezea basi simba tunakoelekea ni kuzuri mambo ya njaa njaa yataisha....
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Mkuu haiwezekani cheki anavyolipwa Pounds 110000 kwa wiki sasa ukiileta kwa makaratsi ya kibongo ni 273,949,542.75 TZS si tutaumia, wakati hapa bongo tunaweza sajili kina nsajigwa ishirini kwa hiyo?
  Nenda hapa Cesc Fabregas and the secret deal! Arsenal paid captain £3m to stave off Barcelona interest | Mail Online

  Ila nimekubali Simba wana hela ukilinganisha na timu nyingine za Africa mashariki (Sijajua Yanga na Azam)
   
 7. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  B_E Fabregas yupi huyo wa thamani hii?

  Kama ni yule wa Arsenal nisaidie ili nipande dau nimsajili kwenye timu ya mtaani kwangu inaitwa "Ganja United"
   
Loading...