Silaha za sumu sasa basi

Silaha za sumu sasa basi

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,485
Poleni wanadamu wenzangu,

Kwa janga hili la Corona Ni Kama Dunia imevamiwa,maana kila nchi Ni vilio.

Kama ningekua na uwezo wa kuzishauri nchi kubwa kivita zinazo shindana kutengeneza silaha za maangamizi hasa silaha za kikemikali,ningeshauri Sasa Basi,waachane kabisa na mipango hiyo,kwa sababu Corona imetufundisha kuwa ama imetengenezwa ama haijatengenezwa lakini Ni ugonjwa ambao umeshindwa kudhibitiwa,Tena umeshindwa kudhibitiwa na mataifa makubwa yenye nguvu,matajiri,yenye sayansi na teknolojia ya Hali ya juu Sana.

Hivyo madhara yake Kama imetengenezwa yameweza kufika hata kwa nchi zisizokua na hatia.

Silaha za maangamizi ya halaiki hazifai hapa Duniani.

Katika maisha yangu ndio nasikia kwa Mara ya kwanza kuwa wanakufa watu 500 katika nchi moja kwa siku moja kwa ugonjwa na Inatokea hivyo siku nyingine kwa nchi nyingine.

Inatisha,hebu fikiria familia nzima,yaani baba,mama na watoto kwa pamoja wote wanakufa na Ni kwa Kaya zaidi ya moja.
Hivyo kwa Hali hiyo,silaha za kikemikali zipigwe marufuku,hazifai.

Siku korona ikihamia kwa wanyama,dunia ndo imekwisha.
Zuia silaha za kikemikali.
 
Uchina kashinda vita III ya dunia bila kurusha risasi hata moja hewani.
Nalog off
 
Back
Top Bottom