Silaha ni nini?

Silaha ni nini?

mwengeso

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2014
Posts
9,286
Reaction score
6,727
Mwaka 2015 Bunge lz Tanzania lilipitisha Sheria mpya inayoiwezesha Serikali kudhibiti umiliki na utumiaji wa silaha na risasi.

Siyo nia ya bandiko hili kurejea mahudhui ya sheria hiyo. Ila kilichonigusa ni swali la Mbunge mmoja, leo Bungeni, kipindi cha maswali na majibu alipouliza ni nini maana ya SILAHA!.

Kwa matukio ya siku hizi ya uhalifu wa kwa kutumia silaha, watu wanahoji usalama katika jamii ulivyo na mashaka, je, maana ya silaha ni nini haswa! Je, maana inabaki ile ile ya silaha ya moto?

Sura ya 322: Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi (Sheria Kuu), inatoa Tafsiri ya neno Silaha kuwa ni pamoja na silaha ya moto.

Gazeti la Mwananchi la Jumatano, Octoba 30, 2013, kwenye makala yake SILAHA HARAMU: JANGA LINALOITESA TANZANIA, ililipotiwa kwamba zaidi ya silaha haramu 500,000 zinazagaa katika nchi za Afrika Mashariki. Na kwa hapa Tanzania hali pia si nzuri, kiasi kwamba wakati huo Serikali iliangamiza silaha zipatazo 30,000 ambazo zilikamatwa katika matukio tofauti ya uhalifu. Lakini pamoja na kuwepo mikakati mbalimbali za kutokomeza silaha haramu, bado tatizo hilo libaonekana kuwa kubwa nchini.

Uchunguzi uliofanywa na Shirika la Uchunguzi wa Silaha Ndogo Ndogo, Small Arms Survey (2013), na Shirika la Kitaifa la Kushughulika na Silaha Nyepesi, Kenya National Focus Point on Small Arms and Light Weapons, kwa usaidizi kutoka kwa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Denmark, ulibainisha kuwa kuna mapungufu katika uwezo wa Kenya kudhibiti silaha ndogo ndogo.

Nimejaribu kutafuta kwenye mitandao, kama uchunguzi wa aina hiyo umefanyika Tanzania sijafanikiwa. Kama kuna mwanaJF anajua hilo, atujuze.

Kuna masuala ya msingi katika bandiko hili, la nini ni maana halisi ya silaha, ya kujadiliana, kwa lengo la kuongeza usalama wa maisha yetu na mali zetu:
1) Utoshelevu wa sheria yetu ya Umiliki na matumizi ya silaha, kwa usalama wa raia na mali zake.
2) Hatua za kupunguza kupatikana kwa silaha.
3) Hatua za kuwashughulikia wamiliki wa silaha.
4) Hatua zenye misingi za kuratibu shughuli za kimaendeleo kufanyika kwa usalama.
5) Mengineyo.

NAWASILISHA
 
Kwa tanzania silaha ni neno mtambuka sana. Mfano mmasai kutembea na sime mjini ni utamaduni lkn mtu mwingine akiwa nalo ni silaha na anaweza kukamatwa
 
Nlitaka kujua mfano silaha za kuwindia kama crossbow na air gun kama airriffle je hizi kumiliki inakuaje ?kama air gun ni bunduki za kuwindia wanyama wadogo kama sungura na ndege.na zinatumia pressure ya upepo. je hizi nazo kumiliki tz ni sawa au
Kwa tanzania silaha ni neno mtambuka sana. Mfano mmasai kutembea na sime mjini ni utamaduni lkn mtu mwingine akiwa nalo ni silaha na anaweza kukamatwa
 
Back
Top Bottom