Silaha 13 za Wasonjo, Wamasai zakamatwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Silaha 13 za Wasonjo, Wamasai zakamatwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mdau wetu, Oct 26, 2011.

 1. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  POLISI Mkoa wa Arusha imekamata silaha 13 zikiwemo za kivita na risasi 449 zilizokuwa zikitumiwa na makabila ya Wasonjo na Wamasai katika mapigano ya kikabila hivi karibuni wilayani Ngorongoro, na kusababisha mauaji ya watu saba na wengine kujeruhiwa.

  Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa alisema silaha hizo zilikamatwa katika operesheni ya Polisi inayoendelea katika vijiji kadhaa wilayani humo.

  Alisema kuwa silaha hizo zimekuwa zikimilikiwa na wenyeji isivyo halali na pia zimekuwa zikitumika katika matukio ya ujangili na uporaji yaliyokuwa yakiripotiwa kutokea wilayani hapo.

  Katika operesheni hiyo, watu saba ambao ni wakazi wa vijiji vya Magaidulu, Olorien, Mgongo Mageri na Wasso wilayani Ngorongoro, wanashikiliwa Polisi wakihusishwa na matukio ya kumiliki silaha hizo kinyume cha sheria.

  Mbali na tuhuma hizo, watuhumiwa hao pia wanakabiliwa na makosa ya kuhusika katika mauaji na kuchochea mapigano ya kikabila.

  Alisema polisi inaendelea na upelelezi zaidi juu ya tukio la mauaji na watuhumiwa waliokamatwa watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

  Wakati watu sita wanashikiliwa kwa kosa la kukutwa na mihadarati aina ya mirungi na bangi.

  Kamanda Mpwapwa alisema watuhumiwa hao walikamatwa katika operesheni ya Polisi inayoendelea katika kijiji cha Mesereni wilayani Monduli na watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi wa Polisi kukamilika.
   
Loading...