Sikuwahi kudhani kama Rais huyu mstaafu ananung'unika ila nilipenda wosia wake nilipomtembelea kwake

Tunavuna tulivovipanda baada ya kukaa maonyo ya waliotangulia.Cha msingi kila MTU Kwa nafsi yake amuombe Mungu atusikie kilio chetu atuondolee hii dhahama.Soma juu ya utabiri wa Nabii Bushiri youtube juu ya nchi yetu 2015 yote yametokea japo mm si Muumini wa tabiri za manabii,alitabiri juu ya tetemeko LA ardhi,alitabiri juu ya mshindi yupi atapewa leseni ya kutuendesha,ujio wa wasiojulikana akisema ameona anga la Tz limejaa damu kila MTU shahidi, uchumi wa nchi kufa yaani hali itakuwa mbaya kila mwaka nyoote mu shahidi.Yote haya ni mapigo tumemwacha Mungu tuna muhitaji Mungu sana ili aondoe laana maana ardhi yetu imelowa damu na ardhi ikilowa damu hakuna chochote kitakachopandwa kitastawi.
Taarifa njema Mungu ameyasikia maombi Na vilio vyetu anakwenda zipundua meza za watesi wetu Na kuzishusha chini atujamkosea Mungu kupita kiasi hata atuache hivo.
 

Attachments

  • Screenshot_2019-05-24-19-15-19.png
    Screenshot_2019-05-24-19-15-19.png
    514.6 KB · Views: 48
Hahaha Yan unipe mwaliko au Mimi nikupe mwaliko?
Kuna siku nitakuaminisha niko Ulaya. Nataka hiyo siku tunakuwa wote mimi na wewe tuko online, halafu unaniambia unataka nipige picha kitu au sehemu yoyote huku nimeweka karatasi iliyoandikwa Macho-Mdiliko kama sehemu ya picha. Hata sasa ningeweza kupiga kwani bado jua halijazama (ni kipindi cha summer) lakini nina shughuli naifanya ndani.
 
Kuna siku nitakuaminisha niko Ulaya. Nataka hiyo siku tunakuwa wote mimi na wewe tuko online, halafu unaniambia unataka nipige picha kitu au sehemu yoyote huku nimeweka karatasi iliyoandikwa Macho-Mdiliko kama sehemu ya picha. Hata sasa ningeweza kupiga kwani bado jua halijazama (ni kipindi cha summer) lakini nina shughuli naifanya ndani.
Kwan hiyo karatasi ukiiandika ndio verification?
 
Britannica acha wizi wa taarifa. Taja chanzo halisi cha taarifa yako; usijifanye wewe ndiye chanzo cha hiyo taarifa huku ukijua kuwa huo siyo ukweli. Huo ujumbe wako umechakachua mahali. Ni ujumbe watu wametumiana sana kwenye makundi ya Whatsapp na chanzo cha huo ujumbe siyo hicho ulichotaja kwenye andiko lako. Linda heshima yako, chomoa huu uzi.
Umeulinganisha mkuuuu
 
AIBU KUBWA UNAPOIBA ANDIKO LA MTU NA KULIFANYA LAKO. HUONI HATA AIBU ? Huo ni wizi mkubwa mtu na wa kutia aibu sana


Nakumbuka wakati wa likizo nimekutana na Binti mdogo tu nikiwa Nyumbani kwa mzee mmoja ambaye ni rais mstaafu tukiongelea ishu ya uwekezaji na mradi wa ufugaji unavyoendeshwa nchini sweden, tukiwa jijii Dar es salaam. Huyo binti aliuliza maswali ambayo saa nyingine yanaibua tafakuri nyingi zaid , Tafakuri hizo zinatokana na jinsi alivyojiboiwa maswali aliyouliza,

Aliuliza hivi, '' Kweli Mungu anaruhusu vipi au kwanini anaruhusu matetemeko ya ardhi na mafuriko, mauaji, utekaji wa watu na upigwaji wa risasi kwa wanasiasa na raia kuikumba nchi yetu wakati Mungu ana uwezo wa kuyazuia? Yule mzee alojawa na busara ambaye sitapenda kumtaja akatoa ufafanuzi na jibu ambalo limejaa umakini mkubwa, akasema "Ninaamini Mungu anasikitishwa sana na mambo haya, kama yanavyotuhudhunisha sisi, Lakini chakusikitisha zaidi kwa miaka mingi sana tumekuwa tukimwambia Mungu asijishughulishe na mambo yetu kama shule zetu, asijishughulishe na serikali na taifa letu, na mbaya zaidi asijishughulishe na maisha yetu. Sasa kwa kuwa Mungu wetu niwa hekima na msikivu, naamini kabisa ameamua kutuacha.

Sasa inakuwaje tunatarajia atupe baraka zake na ulinzi wake wakati tumemwacha na tumemwambia asishughulike na mambo yetu?

Kwa mfano kwa matukio yalitokea hivi punde kama mashambulio mbali mbali,Kupotea kwa watu, Kupigwa risasi kwa baadhi ya wanasiasa, kupigwa hadi kuuwawa kwa wanafunzi mashuleni na n.k. Nafikiri yameanza wakati wa karibuni zaid miaka hii ya 90 haya yote ni kwakuwa tumeomba Mungu asijihusishe kabisa na mambo yetu . Na sote tulikubali kuondoa maombi mashuleni, kwenye taasisi mbali mbali na nakumbuka Wengine wakasema kusiwe na masomo ya Biblia mashuleni. Wengine wakasema kwamba hii inatuvurugia ratiba za kazi ,

Lakini Biblia ndio inafundisha ikisema "Usiue", "Usiibe" na mpende jirani yako kama nafsi yako. Na sote tulisema sawa mafundisho ya Biblia yaondolewe mashuleni. Misaafu na quraan pia inakataza kuua kuiba kusingizia hata kutamani,

Pia kuhusu malezi kuna viongozi walisema tusiwaadhibu watoto wetu wanapokosa kwasababu kwa kufanya hivyo tunaathiri utu wao na kuwavunjia heshima zao (chakusikitisha zaid wakosoaji wa serikali au wa watawala wanapewa adhabu kali zaid ya viboko vya mashuleni ). Tulisema watalaam wanatambua nini wanachozungumza. Na wote tukaridhia tukaacha kuwaadhibu watoto. hii imefukuza hata uwezpo wa Mungu maana walisema tusiwaadhibu wakati vitabu vtakatifu vinaelekeza kuwaadhibu watoto wanapokosea,

Lakini sasa tunajiuliza maswali kwanini watoto wetu hawajitambui wala hawawezi kutofautisha jema na baya, kwanini hawana hofu ya kuua watu wengine, ama wanafunzi wenzao, au kujiua wenyewe.

Yamkini, kama tukifikiria kwa makini, tunaweza kugundua tatizo liko wapi. Ila nadhani hali hii inatokana na dhana kwamba "TUNAVUNA TULICHOPANDA"

Inasikitisha ilivyorahisi watu kudharau na kumwacha Mungu, na kushangaa kwanini dunia inaenda jehanamu. Inasikitisha kwa jinsi tunavyoamini kinachoandikwa katika magazeti, lakini tunahoji kilichoandikwa kwenye Neno la Mungu.

Inasikitisha ilivyorahisi kutuma habari za utani/ mzaha kwa kutumia mitandao ya kijamii kama barua pepe, na zinasambaa kwa haraka utadhani moto wa nyikani, lakini kutuma habari zinazomhusu Mungu unasitasita kutuma kwa wengine.

Inasikitisha kuona jumbe zenye maneno ya kashfa, matusi, kejeli, dharau, zisizo na staha zinavyoweza kutumwa katika mtandao kirahisi, wakati huo huo majadiliano ama mafundisho ya Neno la Mungu kwenye jamii yanazuiwa na kuwekewa vikwazo yasifanyike mashuleni, na maeneo ya kazi... Unacheka?

Inasikitisha kuona jinsi viongozi baadhi wanavyosita na pengine kuacha kutuma muda wao kuwakanya viongozi wenzao wanachoweza labda ni kuungana nao kama kuna sehem kama fursa ya kuwaibia wananchi,
KUNA MAENO HAPA MENGINE YANAUMA SANA SITAYASEMA NIMEACHA MISTARI UJUE NI MAZITO............................................................................................................................................................................................................................................................................................................................ ANAENDELEA CHINI RAIS WANGU MSTAAFU WA AWAMU FLANI
Inasikitisha tunavyoweza kuwa na wasiwasi na woga juu yetu na watu wa taifa letu wenyewe kuogopa kuokotwa kwenye viroba, kuogopa kukatwa mapanga, kuogopa kubambikiwa kesi na pengine kuambiwa mali zako zina ukakasi ilihali nao wanazo zisizosemwa hadharani


Hakuna Taifa ama mtu yeyote anayeweza kuwa salama ama kufanikiwa bila kumshirikisha Mungu. maana hapo ndo tutapata Viongozi imara, wasio madikteta, wasio na majivuno, wasiojikweza, wasiowaonea wengine, wasiotumia madaraka vibaya''


ujumbe huu ulinigusa sana sana sana aisee nikaona tuupate hapa,

Mungu akubariki na tafadhali weka maoni yako alafu mtag member unaye hisi ujumbe huu utamgusa na rafiki zako na watu wengine.

Britannica Encyclopedia
 
Back
Top Bottom