Sikumteua Lowassa kirafiki - Kikwete

Katika hiyo "Biography" yake ameeleza ni mademu wangapi alio-du nao na kuwaachia lile tatizo linalomfanya kutwa kucha awe ughaibuni akiangaika kubadili dam.... au amegusia ni kwa nini alimfunga babu seya....
 
tuacheni chuki na ukasuku. Hivi ukiambiwaa ueleze ufisadi wa lowasa, utauelezea upi? Na kwa ushahidi upi? Avoid dogmatic..

pesa zake anapewa na rafik zake imekaaje? Lowasa ni fisadi mkubwa hata kama hakuiba ila akakubali kutolewa sadaka kumnusuru jk huo ni ufisadi,sasa tunaona jk anavyoanza kumpigia kampen yan wamepanga we gombea leo mi kesho wizi huo, watz hatutak kuongozwa na fikra za watu wawili tu,lowasa ni mwizi mkubwa anayejisafisha makanisan, kama sio mwiz aseme zile mil 150 zilizokuwa zinapotea kila siku chin ya usimamiz wake nan kachukua? Je kakamatwa? Je kahukumiwa? Lowasa mwizi, ila ccm wampitishe cdm tushinde bila hata kampen.
 
"Sikiliza. Ni kweli kwamba Lowassa ni rafiki yangu na nimemfahamu kwa muda mrefu. Lakini pia ninawafahamu watu wengi zaidi kwa muda mrefu, wanasiasa na wasiokuwa wanasiasa na sikuwachagua kuwa Waziri Mkuu." - kikwete

Logically speaking, jibu lako halina maana kwasababu nafasi ya uwaziri mkuu ni moja so husingeweza kuteua zaidi ya mtu mmoja lakini cha muhimu zaidi kwa wafuatiliaji wa mambo ya siasa wanafahamu kuwa 1995 mlitangaza nia yenu pamoja,mlikodi ndege ya kuzunguka mikoani mkiwa pamoja huku ikiwa imebaki chini ya wiki moja kabla ya deadline ya urudishaji form kiasi kwamba mlimkera sana Mwalimu NYERERE ndipo aliposea IKULU nimekaa miaka 27,naijua vizuri sana, IKULU hakuna biashara sasa hao wanaofadhiliwa watarudishaje fadhila ikiwa ikulu hakuna biashara?? Na akawapiga chini vibaka wote wawili the so called BoyzII men - sasa tunajua alikuwa anamaanisha nini!!!


"Nilikuwa natafuta mtu ambaye atafanya kazi kwa ufanisi na kutekeleza sera zangu. Lowassa alijitokeza vizuri kama mtu anayeweza kutokana na uzoefu wake," - kikwete

kikwete nataka nikukumbushe, inawezekana haulielewi hilo kutokana na "urefu" wa akili zako - SERA zinazopaswa kutekelezwa ni SERA za CCM si sera zako maana wewe SI MFALME na nchi si mali yako na mtoto wako ridhiwani(small letters are intended!!!) unalisahau hilo ndio maana unaendesha nchi KIHUNI na kuwateua mashemeji,marafiki na vimada wako katika nafasi muhimu serikalini maana hiyo ndiyo sera yako na matokeo yake ni kuwa Watanzania sasa wanainyea CCM in protest to your misconduction.

Upofu wako unaokuaminisha kuwa sera ni za kwako kwasababu nchi ni ya kwasko ndio uliotufikisha kuwa na Judges ambao hawana sifa hata ya kuwa Mahakimu katika mahakama zetu za mwanzo simply kwasababu ni marafiki zako au wa mtoto wako, IGP ambaye katika ranking za Kipolisi hakuwa na sifa wala uwezo wa kshika nafasi uliyompa, na ulimpatia hiyo nafasi SIMPLY KWASABABU NI SHEMEJI YAKO!!! na yeye ameendeleza mtindo huo huo na kuwaweka wateule wake ambao hawana hata sifa - watu mnateua mpaka VIMADA wenu katika nafasi za serikali na Watanzania wanalazimika kuwalipa mishahara!!!

Nina hakika kuwa katika HISTORIA CHANGA YA TAIFA LETU wewe utakuwa rais wa kwanza kwenda lupango, wewe pamoja na mtoto wako bila kumsahau mke wako na vyote mlivyowaibia Watanzania mtalazimika kuvirudisha na RIBA.

2015 sio mbali, ilianguka Roman empire, ikaanguka Greek empire,Ottoman empire recently hata "British Kingdom" itakuwa nyie ambao in comparison ni vikaragosi wa mbao!!!!
 
Ninaomba anayejua hayo jk anayasema ni utendaji kazi mzuri wa lowasa na mengineyo tafadhali yaorodheshe hapa ndiyo tujadili. Tuache longolongo. Tunahitaji mifano halisi ya huo ufanisi ili tutathimini huo ufanisi ama uchapa kazi unaosemwa ni wa kitu gani na kime mnufaisha lnani kwa kiwango gani. Pls!
 
Lowasa ikitokea akateuliwa na magamba basi bila shaka huo ndiyo utakuwa uchaguzi Rahisi kabisa kupata kutokea nchi hii , cdm watashinda kwa kishindo tena first round , huyo jamaa ni fisadi kuliko mnavyodhani ! Hatumaanishi richmond tu , hebu angalia jengo la umoja wa vijana alikopangisha kwa miaka 99 ( alipangisha kama nani ? ) , kama kuna anayempenda akanywe naye chai , hata monduli anashinda kwa vitisho tu na kuwashughulikia wanaompinga , ukitaka kujua ukweli muulize Dr Toure , mtu pekee aliyekataa kumuabudu binadamu pale Monduli , bali cdm inakwenda taratibu kummaliza baada ya kupenyeza elimu ya kiraia moja kwa moja kwenye machungio ya ng'ombe , ataisoma namba .
 
lowassa ...waziri mkuu aliyeenda new zealand kutembelea bustani za mchicha; baadae akaenda tailand kujifunza jinsi ya kutengeneza mvua; baadaye akaja na wazo la shule za kata wanakosoma watoto wa walalahoi hata kuandika majina yao hawawezi, baadaye akaja na mradi wa kuchuuza umeme akawa analipwa milioni mia 2 kwa siku, baadaye akaja na mkakati wa kujipenyeza kwenye nyumba za ibada hadi akasilimishwa na kuitwa abdala, juzi akajipenyeza kwenye msafara wa obama sijui aliingia kwa cheo gani?

lowassa ni janga la taifa.
 
Mwizi anapojilazimishia ushujaa na kutaka waliomzunguka waanze kumuabudu, aibu...
 

Kutekeleza sera za CCM au za JK? Hapo naona alikuwa ana-underline urafiki wao. Kwa hiyo Lowassa alionyesha umahili wake kutokana na kuingia mikataba mibovu. Kwa hiyo Richmond saga ilikuwa ni sera ya JK, na Eddo alikuwa anatekeleza JK's sera.

By the way, mtunzi wa hiki kitabu ndiye yule professor wa North Carolina anayesubiri kwenda lupango?
 
Mimi huwa nawashangaa sana watu wanaosema EL ana hela sana, hela gani hizo zenye masharti ya kutolewa kanisani na misikitini?
Ni wapi Lowassa alipojenga hata nyumba ya yatima tujue ana Upendo kwa jamii?

Hizo hela za Lowassa wenzetu mnaziona wapi?...wasio waumini wanazifaidi wapi? Amejenga shule gani?, Hopitali gani? Bomba gani la maji au Kisima, Barabara gani?

Kama mtu anasema Lowassa ana hela basi ujue huyo yuko mfukoni mwake, aidha ni mwandishi wa habari au tarishi wake. Mtu wa kawaida hutakaa uone hela ya Lowassa, maana anawekeza pale atakapovuna!

Mtu ananiambia Lowassa ana POWER, power gani? Ile ya kutumia Wasomali kupiga watu?
Au ile ya kukusanya Wamaasai pale Teknico college ili wafanye ukabila?
Power gani, si mseme??

-Angekuwa na Power si angemshindisha Ubunge Mchumba wake Batilda pale Arusha Mjini 2010?

-Si angemshindisha Ubunge mkwewe SIOI SUMARI kule kwao Meru?

-Si angewashindisha udiwani wagombea wao wote hapa Arusha?
POWER ya LOWASSA mnayoiongelea ni ya aina gani?...is it some kinda supernatural or witchcraft oriented?
Mtu angeniambia LEMA ana Power ningekaa kumsikiliza.

Naomba mwenye kujua hata hiyo Prestige mnayoisema huwa anaidisplay akiwa wapi, wakati takwimu za wafuatiliaji wa Bunge zinaonyesha kuwa ni wa tatu toka mkiani kwa Ububu katika Bunge!

Kukaa mfukoni mwa mtu inataka mtu mwenye roho saba kama za Pakashume.
 

mkuu hujamung'unya maneno , umemaliza na asante sana .
 
Mnapochangia mada humu jamvini ni vizuri mkatoa prior kwenye vivid evidence tafadhali... usafi au uchafu wa mwanasiasa yeyote mnauleta na vigezo na ushahid. Tusifuate ushabiki. Tulitumie jamvi kuelimishana kwa maendeleo ya taifa letu. Chuki binafsi na shabiki binafs hazitotusogeza mbele. Proof alongside comments plz!! Tusiropoke...
 
Lowasa hakuwa na ukaribu na JK bali alikua karibu na rostam. Ilikua mawili apewe upm au ahamie upinzani.
 
Mkuu Rock City Angelikuwa Mh Lowasa Kiongozi Mzuri kwanini alijiuzulu? Kwa kashfa za Serikali? angalisafisha machafu waliyokuwa wanafanya hao Mafisadi. Mh Lowasa na Marehemu Aliyekuwa Waziri Mkuu ndugu Edward Moringe Sokoine nani zaidi?

Kipimo rahisi ya ufanisi tz siku hizi ni kuwa "wakikuongelea sana halafu wasikufanye kitu, we dhaifu ila wakila sahani moja nawe, basi we ni zaidi"
 
Mtu makini anapima mawazo yake kabla ya kuzungumza au kuaandika,anajaribu kuingia katika mawazo ya hadhira yake.Ni dhahiri hata mtoto mdogo atatambua ni kwa jinsi gani sentensi tata na yakuchekesha KUMFAHAMU MTU KAMA RAFIKI NA KUMTEUA KWA UFANISI.JE ufanisi huu ndio genge la mikataba mibovu ya kuumiza wananchi.Nimeamini mwizi ampigi mwizi mwenziye bali usema ALIAMISHA TU HAKUIBA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…