Sikulazimishi ila huu ndiyo mtizamo wangu wa Kiufundi baada ya Kariakoo Derby

Kotei si mbaya ila nafikiri namna anavyoambiwa acheze.

Kwangu Mimi nilivyomuona Mwanjali yupo ndani nikajawa Na wasiwasi.Namba NNE angeweza kucheza hata Kotei,Mwanhali ni mzuri ila hawezi kukimbizana Na watoto Kama Mwashiuya.Atafeli tu.

Pia Omog kiukweli Hana mbinu zaidi pale aachwe aende zake tu.
 
Referee.

Nadhani kama kuna mwaka ambao Tanzania imewahi kupata Mwamuzi / Refarii bora na anayeijua vyema Kazi yake hasa awapo Uwanjani basi ni huyu Kijana Eli Sasii. Ubora na umakini wake ndiyo umeweza kumfanya hadi Wachezaji wamuheshimu na wampende na kama akiongozwa vyema kabisa na TFF basi sitoshangaa kumuona siku moja akichezesha michuano mikubwa kabisa ya Kimataifa na kuiletea sana Sifa Tanzania yetu.

Simba SC.

Nikiri wazi kabisa kwamba ndiyo Klabu yangu ambayo naishabikia na naipenda ila katika mtizamo na uchambuzi wangu huu hapa naweza mapenzi yangu yote pembeni na nasema ukweli mtupu bila unafiki na kama ilivyo kawaida yangu.

Nilichogundua ni kwamba siku zote Simba SC inapokuwa inakaribia tu kucheza na Yanga SC basi yenyewe huwa inaweka mno mkazo katika ' ushirikina / uchawi / ndumba ' na siyo kujiandaa ' Kisayansi ' kabisa na hiyo mechi.

Ukiiangalia Simba SC kwa jicho la ' Kiufundi ' kabisa utagundua ya kwamba ilipocheza ' derby ' yake jana pale Shamba la Bibi Timu ilikuwa na tatizo kubwa sana la ' Stamina ' na kuna muda hata Wachezaji wetu wa Simba SC ' upepo ' ulikuwa unakata hadi wengine wengine kule ' majukwaani ' tunashika mioyo yetu kwa ' uwoga '.

Huko nyuma nilikuwa ni Mtu ambaye nilikuwa nikimtetea sana ' mitandaoni ' Kocha Joseph Maurice Omog asifukuzwe ila kwa nilichokiona jana pale Uwanja wa Uhuru nadhani hata nikisia leo hii Simba SC imeachana nae sitoshangaa wala sitohoji na sana sana hata Mimi nitafurahi na kuunga mkono.

Kwanini?

Tukatae tukubali kuna mechi ambazo baadhi ya Wachezaji hata kama ' unawachukia ' lakini hizo mechi ndiyo zao na hata wakiwa wanacheza dhidi ya Yanga SC tumeshuhudia wakileta ' madhara ' makubwa kwa Yanga SC.

Katika ' derby ' ya jana nilishangaa na kusikitika sana kuona Kocha Omog amemuanzisha James Kotei katikati huku akimuacha mwenye ' hati miliki ' na hiyo namba Kiungo mkabaji mdogo wangu Jonas Gerald Mkude na sikushangaa kabisa pale nilipomuona Kiungo wa Yanga SC Papy Kabamba Tshishimbi akilitawala muda wote dimba la katikati hadi ' kuwapoteza ' kabisa akina James Kotei, Muzamiru Yasini na Haruna Niyonzima.

Niliwahi kusema huko nyuma kwamba kama kuna Kosa la Kiufundi kabisa ambalo Klabu ya Simba SC ilifanya ni kumuacha Mshambuliaji ambaye Mimi binafsi nina uhakika wa 100% kwamba angekuja kutusaidia mno Simba SC aitwae Fredrick Blagnon na tukambakisha Mchezaji ambaye Mimi mpaka sasa sioni ' tija ' yake katika Timu na naona ni kama tu vile anakula mshahara wa bure ambaye ni Laudit Mavugo.

Fredrick Blagnon alikuwa na sifa zote za Mshambuliaji na ndiyo maana kila alipokuwa akipangwa Mabeki wa Timu pinzani nyingi walikuwa wanamkaba wawili wawili huku hata wakiogopa kupanda mbele kushambulia tofauti na ambavyo Laudit Mavugo akicheza mabeki humfanya wanavyotaka na ndiyo maana hata jana ' Mshkaji ' wangu wa Mwanza Beki Kelvin Patrick Yondan alikuwa anapanda na anarudi kumkaba Mavugo na ' Limavugo ' likiwa limenywea tu utadhani ' Teja ' la Bwimbwi / Unga.

Kwa mtizamo wangu jana Kocha Omog bila kuwaza mara mbili mbili alitakiwa ama amuanzishe John Boko Adebayor au Mghana Nicolas Gyan ili watengeneze ' striking force ' ya hatari kule mbele badala yake akamuanzisha Laudit Mavugo ambaye nikiri tu wazi kwamba hajui mpira na ikiwezekana hata Kipindi hiki kidogo cha Usajili aachwe tu kwani hana tija Kikosini.

Yako mengi ila haya nadhani ni makubwa zaidi na niwaombe tu wana Simba SC wote kwamba kama kuna Mtu ambaye tunapashwa kumshukuru tena mno tu ni Golikipa wetu ' Tanzania One ' kwa sasa Aishi Manula kwa juhudi zake za kuokoa ile michomo vinginevyo nina uhakika kwamba kama jana lingepangwa lile ' Puto ' jingine Said Nduda zile Goli 5 tulizowafunga Yanga SC zingerudi na pengine hata tungefungwa zaidi ya goli hizo 5.

Yanga SC

Bila unafiki wala kinyongo niseme tu kwamba jana Yanga SC wamecheza mpira mkubwa na wa kiwango cha juu kabisa kitu ambacho hata Sisi wana Simba SC hatukutegemea kwamba ' Jamaa ' wangekaza vile huku wakiwa wanatiririka na kuserereka utadhani Samaki aina ya Kambale ndani ya maji ya Ziwa Victoria.

Kiufundi

Yanga SC jana iliwazidi kwa kiasi kikubwa sana Kiufundi Simba SC hasa katika upangaji wa Kikosi chake ambapo Kocha wao George Lwandamina aliwapanga Watu wa Kazi tupu hasa katika Safu ya Kiungo na Ushambuliaji hali ambayo kila mara ilikuwa ikiwafanya Mabeki wetu akina Method Mwanjale na Juuko Murshid ' kuchanganyikiwa ' na kuchaza ' rafu ' za Kipuuzi na zisizo na maana.

Stamina

Ni ukweli ulio wazi kabisa kwamba nguvu kubwa ya Yanga SC jana ilikuwa ni katika Stamina yao na kiukweli Yanga SC kwa sasa hivi pamoja na Timu kama Za Prisons FC na Mtibwa Sugar ndizo zenye ' Stamina ' za kutosha. Simba SC tujitahidi mno kuwajenga ' Kistamina ' Wachezaji wetu kwani wanachoka haraka sana.

Ukweli Mchungu

Wana Simba SC wenzangu huu ni ukweli japo najua utatuuma ila laiti jana Yanga SC wangeongezeka tu pale akina Amis Tambwe, Thabani Kamusoko na Donald Kamusoko na kwa aina ile ya Uchezaji wa ' Kazi Kazi ' aliokuwa nao jana Mzambia James Chirwa akisaidiwa kwa nyuma na Ibrahim Ajib jana tulikuwa tunakula goli kuanzia 7 mpaka hata 9 kwani jana Yanga SC walikuwa ' watamu ' sana na sijui kwanini hawakushinda.

Mwisho nizipongeze tu Timu zote kwa kuweza kutoka Sare vile na kidogo nawaona Yanga SC kama vile wana Kikosi cha kuwasaidia katika Michuano ya Kimataifa kuliko Simba SC yangu ambayo imesajili kweli Wachezaji wazuri n wakubwa ila bahati mbaya sana Wote kumbe ni ' Pancha ' tupu ( namaanisha Wagonjwa )

Simba SC wenzangu pale tukiwa tunaambiwa na Yanga SC kuwa Sisi ni ' Wapumbavu ' tusiwe tunakataa au kukasirika kwani kwa Mtu mwenye akili ' timilifu ' kabisa hawezi kupoteza Pesa yake na kwenda kuwasajili Wachezaji ' pancha / wagonjwa ' kama Shomari Kapombe, Kipa Said Nduda na hata John Boko Adebayor ambao wote hao Klabu yenye ' akili ' kwa sasa nchini Tanzania na inayoongozwa ' Kiueledi ' kabisa ya Azam FC iliachana nao baada ya kugundua kuwa Kwanza Umri wao umeshawatupa mkono ( tayari Saa 12 jioni ) halafu tena wana ' pancha ' nyingi lakini Sisi kwasababu tu tunawashwa na Pesa zetu za ' utakatishaji ' tukakurupuka kuwasajili. Mchezaji pekee ambaye Simba imelamba dume ni ' Kiraka ' Erasto Nyoni na Golikipa Aishi Manula kwa wale Wachezaji tuliowasajili kutoka Azam FC.

Hii ndiyo tamati yangu ila narudia tena kusema kama nikisikia ama leo au wiki ijayo inayoanza Kesho kwamba Kocha Omog wa Simba SC amefutwa Kazi / Kibarua chake sitoshangaa sana na nadhani nitapongeza kwani kuna uwezekano uwezo wake wa Kufundisha umefikia Kikomo au ana matatizo yake binafsi na Wachezaji au anakubali kupangiwa Timu kitu ambacho ni very ' unproffesional ' kwa Kocha mkubwa na anayejitambua kama Yeye.

Kuna mahala nimeona Msemaji wangu wa Simba SC Haji Manara ' anawananga / anawachamba ' Yanga SC kwa kuwaambia wanashangilia ile draw / sare ya jana lakini hapo hapo tena huyu huyu Haji Manara amesahau au amejisahaulisha kwamba mwaka 2013 hata Sisi Simba SC tulipocheza ile derby yetu na Yanga SC ' iliyotimia ' huku Makocha wetu wakiwa ni Mzee Kibaden na Julio mpaka ' half time ' Simba SC tulikuwa tumeshakula tayari goli 3 ila Kipindi cha pili tu baada ya kuingia Vijana akina Said Ndemla na William Lucien Gallas wakishirikana vizuri na Jonas Mkude waliweza ' kukichafua ' sana pale katikati hadi tukarudisha zile goli zote 3 na mpira ulipomalizika tu Simba SC wote ( hadi Mimi GENTAMYCINE ) nikiwepo tulishangilia utadhani tumebeba Kikombe cha VPL vile tukaishia kukisikia tu kwa Yanga SC hadi mwaka jana tulipoenda kukiulizia Uswisi kwa FIFA na bado vile vile ' ikala ' kwetu.

Haji Manara Msemaji wa Simba SC atawachekaje Yanga SC kushangilia ile sare jana wakati ni ukweli ulio wazi kabisa kwamba Simba SC yetu ya ' Bilioni ' jana ilipelekeshwa ' puta ' na Vijana wadogo tu akina Patrick ( Pato ) Ngonyani, Raphael Daud na Pius Buswita na bado Wachezaji wetu wa Simba SC ' ulimi ' uliwatoka hadi tukawa tunaomba mpira umalizike tu haraka ili ' Wazee ' wa ' Bilioni ' tusiadhirike / tusiumbuke?

Kila la kheri.

GENTAMYCINE nawasilisha.
Mmmh
 
38ae67493123d83a3557431e40f1e8b6.jpg
56f89d11da3ec67db9fe846b9d4ce299.jpg
.....kweli simba ilituzidi KISHIRIKINA......PAMOJA NA YONDANI KUVAA FURUSHI KIUNONI lakini WAMEPATA SULUHU......simba noma sana
 
Asante kwa kuwa mkweli

Huo uchambuzi si sahihi kwa sababu ume base kwenye Kotei na Niyonzima ukiwalinganisha na Mkude na Ndemla. Kwa mtizamo wa watu wa simba kwa ujumla, watu walioonekana hatari kidogo jinsi ligi ilivyokuwa inaenda ni Ajibu na Chirwa, kwa vipaji vyao binafsi na kwa Ajib siyo kwa mpira mkubwa bali kwa potential ya scandal.

Ajib angefunga lisingekuwa jambo la ajabu kwani kafanya hivyo tangu akiwa Simba na mpaka ana a.k.a kwa hilo, bali ingekuwa fursa ya kuikejeli Simba kwa sababu ambazo mtu yeyote anaweza kuelewa. Ajib alikuwa zaidi ni kero na si tishio. Upana wa kikosi cha Simba unasaidia mengi, kuziba mapengo kwa aina pana za mechi na mazingira.

Wakati mwingine unahitaji wazoefu, wakati mwingine stamina, wakati mwingine watu wa jihad. Hapo ndiyo suala la tactics linakuja, yaani the right time ya kuwatumia wote hao.

Unachotakiwa kujua ni kuwa Simba imekuwa pia ina tatizo la wachezaji wenye vipaji bali wasiojituma na wenye nidhamu mbovu. wengi tunajua tofauti ya nidhamu kati ya wachezaji toka nchi za nje hasa West Africa na hapa kwetu hata jirani zetu.

Kwa kifupi Omog alikuwa hajapata first 11 ya ukweli kwani ni bado mapema ktk na hajakutana na timu za kusaidia hilo. Kwa mechi ya watani, first 11 inaweza kuwa na sehemu kubwa ya wachezaji waliokuwepo baada ya kuingia Mkude, yaani Mavugo awe out, mzamiru na ndemla wa interchange kutegemea na mechi. Ndemla wakati mwingine anafaa hata ku exchange na Kichuya etc. Ila Mavugo anai cost sana Simba anaipotezea opportunity nyingi sana.

All in all, composure ya Simba ilikuwa kubwa na confidence kubwa. Swali? Ball Possession ya 55 dhidi ya 45 unawezaje kuruhusu mpira unaanza na kenda moja kwa moja golini. Hapo panataka dawa kubwa hasa ya saikolojia, vinginevyo Simba waliizidi yanga ingawa mpira ni magoli. MANULA aongeze seriousness, MWANJALI mmh, lile goli la Azam pekee mwaka jana lilitunyima ubingwa, off course na yale mawili ya yule kipa mu ivory. MANULA AMESHAFUNGWA MAGOLI MABAYA KULIKO YOTE YA MSIMU ULIYOPITA WANAOHUSIKA WAMWELEZE UKWELI.
 
Mara paap Ngoma,Tambwe na Kamusoko ndani...watu wangepotea mjini kama tausi wa Ikulu

Mpira hauko hivyo ukiona hata Ajib anayeujua mpira alikuwa anarandaranda uwanjani, tambwe angepata wapi mpira? simba walikuwa wanapiga pasi uwanja mzima! ilinikumbusha Al ahly ya egypt ya kina Tareek Abu Zeid iliyocheza na Yanga Taifa miaka ya 90 afu Ajib ndiyo kama alivyokua Mar. Selestine Sikinde Mbunga. wakatoka sare 1-1. Kwenda Egypt walipigwa sijui ngapi? sasa sijui duru la pili ila viwango tofauti. Haifai kuongea sana mtasema mbona hamkufunga hata Everton walitoka sare na Gor.
 
Niatumia sana simba wakikosa ubingwa mwaka huu halika nitaimia saaaana na sitaki hata kufikiria japo naanza kuona simba hawajagundua sababu ambazo zina wakosesha ubingwa.ikiwa hawajagundua defenetly watarudia kosa
Naumia sana
 
Huo uchambuzi si sahihi kwa sababu ume base kwenye Kotei na Niyonzima ukiwalinganisha na Mkude na Ndemla. Kwa mtizamo wa watu wa simba kwa ujumla, watu walioonekana hatari kidogo jinsi ligi ilivyokuwa inaenda ni Ajibu na Chirwa, kwa vipaji vyao binafsi na kwa Ajib siyo kwa mpira mkubwa bali kwa potential ya scandal.

Ajib angefunga lisingekuwa jambo la ajabu kwani kafanya hivyo tangu akiwa Simba na mpaka ana a.k.a kwa hilo, bali ingekuwa fursa ya kuikejeli Simba kwa sababu ambazo mtu yeyote anaweza kuelewa. Ajib alikuwa zaidi ni kero na si tishio. Upana wa kikosi cha Simba unasaidia mengi, kuziba mapengo kwa aina pana za mechi na mazingira.

Wakati mwingine unahitaji wazoefu, wakati mwingine stamina, wakati mwingine watu wa jihad. Hapo ndiyo suala la tactics linakuja, yaani the right time ya kuwatumia wote hao.

Unachotakiwa kujua ni kuwa Simba imekuwa pia ina tatizo la wachezaji wenye vipaji bali wasiojituma na wenye nidhamu mbovu. wengi tunajua tofauti ya nidhamu kati ya wachezaji toka nchi za nje hasa West Africa na hapa kwetu hata jirani zetu.

Kwa kifupi Omog alikuwa hajapata first 11 ya ukweli kwani ni bado mapema ktk na hajakutana na timu za kusaidia hilo. Kwa mechi ya watani, first 11 inaweza kuwa na sehemu kubwa ya wachezaji waliokuwepo baada ya kuingia Mkude, yaani Mavugo awe out, mzamiru na ndemla wa interchange kutegemea na mechi. Ndemla wakati mwingine anafaa hata ku exchange na Kichuya etc. Ila Mavugo anai cost sana Simba anaipotezea opportunity nyingi sana.

All in all, composure ya Simba ilikuwa kubwa na confidence kubwa. Swali? Ball Possession ya 55 dhidi ya 45 unawezaje kuruhusu mpira unaanza na kenda moja kwa moja golini. Hapo panataka dawa kubwa hasa ya saikolojia, vinginevyo Simba waliizidi yanga ingawa mpira ni magoli. MANULA aongeze seriousness, MWANJALI mmh, lile goli la Azam pekee mwaka jana lilitunyima ubingwa, off course na yale mawili ya yule kipa mu ivory. MANULA AMESHAFUNGWA MAGOLI MABAYA KULIKO YOTE YA MSIMU ULIYOPITA WANAOHUSIKA WAMWELEZE UKWELI.

Kama uchambuzi wangu siyo sahihi je wako huu ndiyo umeoana ni sahihi? Pumbavu mkubwa Wewe halafu jifunze kuheshimu mawazo ya Mtu. Kwahiyo ulikuwa unavizia Mtu aje na ' uchambuzi ' au ' mtizamo ' wake juu ya hiyo ' derby ' kisha ndipo useme siyo sahihi? Pumbavu mkubwa Wewe. Mwisho jiulize ni kwanini ' nimekushambulia ' Wewe halafu kuna Members wengine ambao wamepingana na huo mtazamo / uchambuzi wangu na nimekubaliana nao Kimsingi / Kihoja. Mwisho mtafute Mtu hapo ulipo ambaye amekuzidi ' akili ' kisha muulize ni kwanini katika hii ' mijadala ' ya Mtandaoni Mtu anatakiwa kufanya ' critique ' na siyo kufanya ' criticize ' labda unaweza ukajifunza zaidi. Pumbavu.
 
Nashangaa hadi saiz sijaskia habari za Omog kutimuliwa! Au wanasubiri hadi tukadondoshe point zote tatu nyanda za juu wiki ijayo?! Alafu manara amezidi uropokaji, hana tija yoyote!!
Nakubaliana na wewe, inaelekea Simba wanaona ligi hii bado sana. Ligi ilishaanza kitambo na ninachokiona watajichanganya kidogo tu either na vidroo au kufungwa na itakuwa ndio mwisho wao.

Naona Yanga wanaimprove kila leo wakati Simba wanashuka kila leo, wasipofanya mabadiliko ya kocha sasa hivi wasije wakaanza kutafuta rufaa FIFA.

Inaniuma sana tena sana kumuweka bench one of the best midfielders in Eastern and Southern African football, Jonas Mkude. What has this young man done to deserve all this. Alipoingia yeye kama dakika kumi na kitu katikati pakabadilika kabisa. Namshauri Mkude atafute klabu nyingine msimu mwingine aachane na uswahili wa klabu ya Simba, japo roho itaniuma sana.
 
Kama uchambuzi wangu siyo sahihi je wako huu ndiyo umeoana ni sahihi? Pumbavu mkubwa Wewe halafu jifunze kuheshimu mawazo ya Mtu. Kwahiyo ulikuwa unavizia Mtu aje na ' uchambuzi ' au ' mtizamo ' wake juu ya hiyo ' derby ' kisha ndipo useme siyo sahihi? Pumbavu mkubwa Wewe. Mwisho jiulize ni kwanini ' nimekushambulia ' Wewe halafu kuna Members wengine ambao wamepingana na huo mtazamo / uchambuzi wangu na nimekubaliana nao Kimsingi / Kihoja. Mwisho mtafute Mtu hapo ulipo ambaye amekuzidi ' akili ' kisha muulize ni kwanini katika hii ' mijadala ' ya Mtandaoni Mtu anatakiwa kufanya ' critique ' na siyo kufanya ' criticize ' labda unaweza ukajifunza zaidi. Pumbavu.

mimi nimetumia msemo si sahihi na kujaribu ku elaborate, lakini wewe umenitukana mpumbavu! sasa sioni kama una moral authority ya kuni guide kuhusu tofauti kati ya criticism and critique, nafikiri tuachie hapo, time will tell.
Thanks.
 
Back
Top Bottom