Sikubali majibu ya DNA


mkuu nikutoe wasiwasi hiyo DNA (Deoxyribonucleic acid) haibahatishi hata kidogo, unachopewa ndiyo hicho ulichonacho. Yawezekana mtoto alibadilishiwa kama watu wengi hapa wanavyoongea au ni kweli yeye ni mama wa huyo mtoto lakini baba siyo huyo. wanawake wana siri sana yawezekana alichepuka lakini hajui ni linialipata mimba. Mathalani mwanamume alikuwa safarini kwa muda wa miezi 6 halafu mwanamke akawa anachepuka lakini akaacha kuchepuka miezi miwili kabla ya mume wake kurudi na mwezi mmoja kabla ya mume kurudi akapata hedhi. kwa namna hii akajiridhisha kuwa kwa vile amepata hedhi basi hakuna shida. ikumbukwe kuwa kupata hedhi siyo kwamba huna ujauzito. kuna wanawake wanapata mimba na bado wanapata hedhi. akubali alichepuka ila hajui ni lini kitu kiliingia.

Mfano hapo chini nilipozungushia nyekundu ni vinasaba vya mama na mtoto na namba zenye rangi nyekundu ni mtoto na baba.


 
sawa tukija na hiyo kesi ya pili ikitokea majibu walikupakuwa toto ni wako na baada ya miaka kadhaa ukaenda na mtu mwingine wakasema mtoto sio wako unaweza kudai fidia hapo.....
 
km mtoto kabadilishwa hospitalini vipimo vya DNA vitaonyesha hata mama yule mtoto sio mwanae. Kwa hiyo iko solved ila kinachobaki labda alikalia genye ya mtu mwingine kwa bahati mbaya!
 
Nimeuliza sijibiwi.
Ni nini kilipelekea kuanza kutafuta uthibitisho kwa njia ya DNA?
 
mmmhhhhh una uhakika ocean road kuna hicho kipimo? huyo mwanamke nae ana mambo anakiangaisha kiumbe cha tumboni hivyo ili iweje?mwanamke ndie mwenye uhakika kuwa mtoto ni wa nani aachane na hiyo DNA
 
mmmhhhhh una uhakika ocean road kuna hicho kipimo? huyo mwanamke nae ana mambo anakiangaisha kiumbe cha tumboni hivyo ili iweje?mwanamke ndie mwenye uhakika kuwa mtoto ni wa nani aachane na hiyo DNA

maabara ya mke mkuu wa serikali kwa ajili ya DNA kwa kanda ya mashariki zipo hospitali ya ocean road. maabara nyingine ipo mwanza na nyingine mbeya kama sijakosea.
 
Mwenye uhakika mtoto ni wa nani huwa ni mama. Ila kama yeye anajiamini kuwa hakuwahi kuchepuka katika kipindi chote cha ndoa, labda kuna namna ambayo aliingiliwa kimwili bila ya yeye kujua. Au labda alibadilishiwa mtoto hospitali baada ya kujifungua... DNA scanner, is very efficient. sio rahisi ikamuonea mtu...
 
maabara ya mke mkuu wa serikali kwa ajili ya DNA kwa kanda ya mashariki zipo hospitali ya ocean road. maabara nyingine ipo mwanza na nyingine mbeya kama sijakosea.

kama ni hivyo sawa coz nasikia lazima uwe na kibali cha kufanya hicho kipimo
 
hakuna kitu kinatisha kama kutojua baba wa mtoto.

Huwa naimagine mtu akikalia sperm bila kujua afu kikatick ni nightmare.

Wewe unaleta utani. Hakuna kitu kama kukalia sperm hlafu mtu apate mimba. Sperm zina uratatibu wake wa kwenda kwenye yai la mwnamke. Ni lazima kuwepo na presha Fulani ya kuzisukuma. Lazima zenyewe ziwe katika volume inayoziwezesha kuswim kuelekea kwenye yai la kike. Halafu huyo mama anabisha kiunafiki tu lazima anajua mpango mzima ulivyokwenda. Tunawajua sana wanawake wa kibongo. Yeye angekubali tu kama ni aibu imeshamfika na kama mume atamuacha basi au lah kama atamsamehe yote kheri. Bora yeye aliyezaa.Kuna mke wa ntu ni jirani yangu alichepuka kikanasa wakati mume akiwa short course india. Huyu mama alijaribu kutoa umauti ukamfika.
 

Kuna uwezekano mkubwa wa kubadilishiwa mtoto hasa katika enzi zile za zamani kidogo.

Unaweza kupima DNA ya mama ili ucheki kwamba kweli inalingana na ya mtoto (sawasawa na kupima ya baba).

Ikiwa ya mama na baba hazikulingana na huyo mtoto ina maana mumebadilishiwa.
Ikiwa ni baba tu tafauti lakini imelingana na ya mama ina maana huyo mama amekubambikizia mtoto.

Sijawahi kusikia kesi ya DNA imelingana ya baba lakini mama tafauti.
 
DNA ni 99% accurate. Swali ni kweli imefanyika. Maana bongo hii acha kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…