Hii habari imekaa kipropaganda na haishangazi imechapishwa kwenye gazeti la propaganda la serikali (Habari Leo). Kwanza ujiulize kwa nini usafirishaji kwa njia reli umekuwa hapewi kipaumbele na serikali katika miaka ya hivi karibuni? Na mazingira yaliyopelekea hii hali iwepo sasa yamebadilika? Nani kasema "uchawi" wa kuepukana na utegemezi wa malori katika usafirishaji mizigo ni kujenga reli ya "standard gauge (SG)"? Na kwa nini reli ya Tazara nayo haitumiki kikamilifu na hakuna mpango wa kuigeuza kuwa ya SG? Hoja yangu hapa ni kwamba njia za reli zilizopo zimetelekezwa makusudi na siyo kwamba haziwezi kuendelea kutumika "economically" kama zikikarabatiwa inavyotakiwa kuwa na mabehewa ya kutosha. Sana sana ukizingatia gharama kubwa ya hiyo reli ya SG hakika itakuwa "white elephant" kama uchambuzi wa kitaalamu ulivyothibisha kwa reli inayojengwa Kenya.