gfsonwin
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 18,272
- 20,692
Wanabodi,
Herini ya mwaka mpya na hongereni sana kwa majukumu yenu ya kila siku.
Baada ya kimya kirefu leo naona nije na mada juu ya siku ya wanawake duniani.
Mie napenda zaidi niiongelee kwa hali halisi ya hapa kwetu Tanzania. Hivi kweli siku hii inayo mantiki yeyote kwetu?
Herini ya mwaka mpya na hongereni sana kwa majukumu yenu ya kila siku.
Baada ya kimya kirefu leo naona nije na mada juu ya siku ya wanawake duniani.
Mie napenda zaidi niiongelee kwa hali halisi ya hapa kwetu Tanzania. Hivi kweli siku hii inayo mantiki yeyote kwetu?
- Hivi inamsaidia nini mwanamke aliyeko kule kijijini ambaye upande wa khanga ni shida, achilia mbali hali ngumu ya maisha na manyanyaso ya kijinsia?
- Mbona hii siku inawika zaidi mjini na ni kama vile ni ya watu wa caliber fulan hivi, sijaona wanawake wakulima, wafugaji, wakiwekwa humu. wengi utakuta ni wanawake wanaofanya kwenye maofisi tena ya maana ambao hata hizo khanga na vitenge wakivaa siku hiyo huziweka adi kuliwa na panya?
- Hivi hao wa vijijini ambao upande wa khanga hawana hawastahili kuvaa hivyo vitenge na tshirt za siku ya wanawake duniani?
- Cha ajabu sherehe hizi hufanyika mjin tu kwann basi kitaifa zisifanyike kijijini huko Haneti ama Kyeleme ili izo khanga na tshirt na wao wavae?
- Hivi uwepo wake umesaidia jamii yetu hasa maswala ya kunyanyuliwa kiuchumi na kupata mianya kufanya biashara na kumiliki uchumi?
- Je kuna uwiano katika uhuru wa kumiliki uchumi kati ya wanawake wanaotafuta hela kwa kufanya kazi katika mazingira magumu na wale ambao wanafanya katika mazingira mazuri?
- Hivi siku hii imewasaidiaje wana wanawake ambao wanafanya kazi kwenye mazingira yanayoruhusu kunyanyasika kijinsia? hasa wale wanaohudumu kwenye baa na kazi za majumbani?