Siku ya wanawake duniani kwa wengine ni mapumziko na sababu zipo za msingi

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Nchini Ukraine na katika baadhi ya mataifa duniani, leo tarehe 08.03.2016 ni siku ya mapumziko, kwa sababu ni siku ya wanawake duniani. Kwetu inachukuliwa kwa heshima lakini sio kama wengine wanavyoichukulia. Mfumo dume ni tatizo la maisha ya muafrika, hawezi kuielewa thamani na umuhimu wa siku kama hii. Malezi yanayomfanya mtoto wa kike ajione mnyonge na asiye na umuhimu kwenye jamii na yenyewe ni sababu inayoifanya siku ya leo ionekane ni ya kawaida tu.

Mama wa kifrika akizaa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi anaambiwa kaleta mkosi kwenye familia. Akishindwa kupata watoto kwa sababu zilizo juu ya uwezo wake anaambiwa anajaza choo.
Akifumaniwa na mme wa mtu anachapwa viboko hadharani mpaka anaishiwa nguvu.
Akifiwa na mume wake, ananyang'anywa mali zote za wakwe zake, na kinachofuatia ni kufukuzwa kama vile mnyama asiyestahili chembe ya ubinadamu.
Akipewa ujauzito wakati bado yupo sekondari upo uwezekano mkubwa huo ukawa ndio mwisho wake wa kuendelea na masomo.
Kwenye baadhi ya makabila, akimaliza darasa la saba ndio mwisho wake wa elimu, kinachofuatia ni ndoa wakati akiwa katika umri mdogo.

Zipo sababu nyingi zenye kuipatia umuhimu wa kipekee siku ya leo, na sio dhambi ikiwa kuanzia mwaka ujao kila tarehe nane mwezi wa tatu ikawa ni siku ya mapumziko. Mataifa makubwa kiuchumi kama Russia na Ukraine kwa siku ya leo ni mapumziko. Tanzania ina kila sababu ya kuiheshimu siku hii, na sio iishie kwa waziri mwenye dhamana ya maendeleo ya kinamama kuyapokea maandamano ya kinamama waliovalia sare zenye kuelezea mapambano ya mwanamke. Ni maoni yangu, natumaini yatasomwa na kuleta tafakari ndani ya vichwa vya walio wengi, haswa wale wenye madaraka ya juu serikalini.
 
Back
Top Bottom