Siku ya kimataifa ya Saratani duniani 2018

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Siku hii ya saratani inaadhimishwa kila mwaka Februari 4 na ya mwaka huu inakuja wakati ripoti zinasema imeshakatili maisha ya watu milioni 14 duniani.

Shirika la afya duniani-WHO linasisitiza kuwa karibu kila familia duniani inaguswa na saratani kwa njia moja au nyingine lakini wakati huu kuna maendeleo fulani ambayo yamepatikana kuhusu tiba ya saratani.

Licha ya hivyo WHO inasema mbali ya kupatikana maendeleo katika juhudi za kuzuia, kutibu na kutoa tiba shufaa kwa wagonjwa wa saratani, lakini maendeleo hayo hayapatikani kote duniani.

Katika tarifa yake kwa ajili ya siku hii shirika hilo linasema matibabu katika nchi nyingi baado ni ghali mno au hayapatikani kamwe na pia huduma za tiba shufaa hazipo.

Kwa mujibu wa takwimu za WHO, saratani ndio iliongoza dunaini kama chanzo cha magonjwa na vifo mwaka 2012 na kulikuwa na visa vipya takriban milioni 14. Aidha mwaka 2015 saratani ilishika nafasi ya pili kwa kusababisha vifo 14 milioni huku asilimia 70 ya vifo vyote vya saratani hutokea katika mataifa yenye vipato vya nchini na wastani.

Mbali na tiba wataalamu wanasema kuwa theluthi moja ya vifo vya saratani hutokea kwa sababu 5 muhimu za kitabia pamoja na aina fulani ya vyakula zikiwemo mwili mnene kupita kiasi, ulaji mdogo wa matunda na mboga za majani, kutofanya mazoezi, utumiaji wa tumbaku na pombe.

WHO inaamini kuwa mwaka 2018 utakuwa mwaka muhimu ikifafanua kuwa mataifa wanachama yatakuwa yakitekeleza miongozo ya azimio la kikao cha afya duniani ,pamoja na ripoti ya maendeleo ya kupatikana kwa ratiba ya utekelezaji wa azma za mataifa katika mkutano wa ngazi za juu wa tatu wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa, katika kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukiza , ambao utakafanyika katika nusu ya pili ya mwaka 2018.

Chanzo: Redio ya UM

========

Takwimu za kansa kidunia kwa mwaka 2016
Kansa.jpg
 
Back
Top Bottom