Siku Walimu tutakapojitambua

Kuna mwalimu kaenda kusimamia mitihani mahali... Mvua zinanyesha gari limekwama mita kadhaa kutoka shuleni! Ikabidi aanze kubebeshwa maboksi ya mitihani kichwani... Yaani yeye anadondoka anaamka... kalowa kila kona ...viatu na soksi vimeenda na maji lakini boksi lipo salama kichwani...
Yote ni anapambana apate hiyo posho ya 60K kwa siku!
 
Walimu ni watu Bora sana kwenye Nchi hii, maslahi hupangwa na serikali.ulipaswa kuisema serikali kwa kutowapa kipaumbele walimu. Leo teuzi nyingi zinaenda kwa waandishi na watangazaji. Wakati ni watu walio na ufaulu wa chini. Walimu wamesoma ndg. Hata hao walimu wa s/m wamesoma kuanzia deploma na kuendelea. Leo tunaanza kuona vitoto vya s/m vinaongea kiingereza. Haya ni mafanikio makubwa sana kwenye Taifa letu. Mada zibadilike ziwe
1. Ni wakati Sasa wa kurudisha teaching allowances
2. Ni wakati wa kuwajengea walimu nyumba
3. Ni wakati wa serikali kuwekeza kwenye elimu Bora
4. Ni wakati wa kuwainua walimu kiuchumi.
Roho zenu mbaya ndio zinaondoa baraka kwenye Nchi hii. Bariki walimu uone kama Mungu hataibariki Nchi.
 
Wakijua kusema HAPANA watairudisha heshima yao.
 
Tatizo pekee la walimu ni kukubali kujifungamanisha na ccm!
 
Nursing na Pharmacy levels za certificate na diploma wanaenda kwa ufaulu upi? Hebu weka hapa. Maana najua Kuna watu wako kule hata sikutarajia kama walipaswa kuwa kule.
 
@Mpwayungu Village huyu nae alikuwepo
 
Hizi porojo za Walimu kutumiwa kuhujumu Chaguzi naona zimezidi na zinaletwa na wapuuzi wasio na ABC zote za namna wizi unavyofanyika. Ninachoshangaa ni makundi mengine kutolaumiwa kwa jambo hilo?

Viongozi wa Upinzani wanajua wanaowahujumu sana kwenye Chaguzi ni hawa wafuatao. Na hutasikia wamemlaumu Mwalimu hapo.

1.Ti Ai SS.
2.Jeshi la Wananchi wa Yanga - rejea kule Zanzibar (Walimu hawakutajwa kabisa)
3.Geshi la Polish.
4.Wakurugenzi wa Halmashauri.

Kwahiyo basi, wenye kushinikiza huo uhuni wanafurahi sana wanapoona lawama zenu mnazipeleka off target. Wapinzani huhesabu kura pure kutoka moja kwa moja vituoni, ambalo wizi unakuwa haujafanyika (anakosimamia Mwalimu). Ila wizi unaanza kufanyika kwenye compiling stations (centers) ambako Mwalimu hayupo. Kumbukeni: January Mamba hakucheza mchezo na Walimu kusababisha goli la mkono. Alishirikiana na watu msiowajua kabisa kenge nyie.
 
Tatizo kubwa linasababishwa na umoja wao kulala na kutoshughulia maslahi ya wanachama wao. Hii inatokana na serikali kupandikiza hao viongozi wa umoja wa waalimu ila kuweka kizibo kwa juhudi za kuimarisha hadhi na maslahi ya waalimu.
Haya pia yapo kwenye vyama vya umoja vingine kama chama cha wafanya kazi n.k.
 
Nchi hii walim wa miaka hii kujitambua ni ngum sana, wamemezwa na mfumo, ukitaka jua hili angalia kwenye halmashauri mbalimbali namna afisa elim anavyowapelekesha kama vile ndo mwajiri ,wakati mwajiri na Mkurugenzi

Yani unakuta eti mwalim anakua chahwa wa Afisa elim ,takataka sana
 
Kama wewe ni mbishi na hupendi mshahara wako ukatwe na hiyo misiwitii umeshindwa vipi kupambana na afisa utumishi wako kwa kumkomalia liwe jua au mvua mpaka akutoe?Kama wewe ni mwamba na unajiamini fikisha malalamiko yako kwa RAS nako wakishindwa kukusaidia mwamba Mchengerwa anakusubiri Dodoma umpelekee hiyo kero au mpigiea simu uone hapo halmashauri kama patakalika.Unachotaka kufanyiwa ni haki yako kisheria isipokuwa hao maafisa utumishi wanapewa rushwa na siwitiii.Wake up

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Shi
Shida mawasiliano
 
Ni kweli hao walimu licha ya mambo ya ovyo wanayoyakubali kutoka kwa viongozi uchwara ambapo imefika mahali wanaamurishwa wachangie mpaka mbio za mwenge kwenye halmashauri zao walimu hawana mandate yoyote ya kuweza kuchakachua matokeo ya uchaguzi.Uhuni huo hufanyika kuanzia ngazi ya halmashauri ambako kuna mteule wa mgombea wa sisiyemu ambaye ajabu na kweli ndiye msimamizi wa huo uchaguzi ngazi ya jimbo

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…