Siku simba itakapoipigia yanga makofi

Siku simba itakapoipigia yanga makofi

NAPITA

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
5,077
Reaction score
2,250
tofauti.jpg
Hii sheria nayo sasa imefika mda nayo itumike huku kwetu ili kuleta ushindani zaidi katika soka letu timu zetu zitakuwa zikijitaidi kushinda kabla ya ligi kuisha ili zipigiwe makofi kama tulivyoona katika mechi ya juzi kati ya Man u na Asenal. Kama ingekuepo huku kwetu basi tungeshuhudia Simba wakijipanga kuwasubilia Yanga wawapigia makofi kama mabingwa wa Tanzania sijui ingekuaje ha!ha!........!!(WATANI WA JADI RAGE AMPIGIE MAKOFI MANJI)
 
Kuna umuhimu wa kuwasiliana na muheshimiwa Supika hii sheria itungwe for future use au kama vipi ianze May 18 kisha tutunge sheria kikao kijacho, kwa sheria za nchi yetu hili linawezekana kabisa kama tutaona linafaa.
 
Tarehe 18 Mei 2013 Lazima Kaseja ampigie makofi Mustapha 'Barthez' huku Kapombe akimpigia makofi Domayo, pairing nyingine, nanyi wekeni. Simba akikaidi kupiga makofi, atashushwa daraja.
 
Mla ni mla leo, mla jana kala nini? Mavi ya kale hayanuki.
Lakini ndo yanayofaa kwa mbolea, halafu mmekomaa mpigiwe makofi na Simba kwa nini msipigiwe makofi na Coastal union ambao mnacheza nao mapema kabla yetu?
 
Naikumbuka sauti ya Ahmedi Jongo enzi zile za RTD "ni yule yule wa May 18 Said Suweid Scud anapachika tena bao zuri kweli kweli, Yanga moja Simba hawajapata kitu. Chale embu elezea hapa" kwa kweli hii tarehe sio nzuri kwa mxyama.
 
Lakini ndo yanayofaa kwa mbolea, halafu mmekomaa mpigiwe makofi na Simba kwa nini msipigiwe makofi na Coastal union ambao mnacheza nao mapema kabla yetu?

Wanaanza Coastal Union, Simba ni 'next'.
 
Msimu ule tuliowapiga mkono mpaka mkaanza kulia kwenye Tv ndio ulikua muafaka kwenu nyie kuwapigia simaba parade and not otherwise
 
Tano zinalipwa lini???

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Tano zinalipwa lini???

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

WE HUTAKIWI KULIPA 5-0 ... HIZI 5-0 UMELIPWA WEWE... WEWE LIPA 6 -0... Salamu zako mtani :A S 103:
 
Back
Top Bottom